Uhuru wa tume hauthibitishwi kwa kuhubiriwa,ulipaswa ujidhihirishe wenyewe.Kuwaambia watu kuwa tume yako ni huru wakati tume yote kuanzia ngazi ya juu hadi chini imesheheni makada wa chama na usalama wa Taifa ni kutugeuza watanzania wote ni wajinga.
Figisufigisu za kiuchaguzi huwa tunazishuhudia kwa macho yetu,hila na udanganyifu unaofanyika na maelekezo wanayopewa wasimamizi ili wayatekeleze ndani ya chumba cha kupigia kura tunayafahamu,nawafahamu hadi wasimamizi waliopata misukosuko baada ya kuonekana wamekataa kufuata maelekezo ya kukibeba chama tawala,wengine wamefikia hadi kuitwa na wakuu wa vituo vyao vya kazi na kuombwa watoe maelezo kwa nini wanaunga mkono upinzani,hivyo kukurupuka na kusema tume ni huru ni upuuzi mtupu.
Wakati nipo serikalini niliwahi kunyimwa nafasi ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2005,niliachwa nje katika michakato yote,sababu kuu niliyoelezwa ni kuhisiwa kuwa ninauunga mkono upinzani,lakini baadae nilijumuishwa katika masuala fulani ya kiusimamizi na huko ndipo nilipobaini michezo yote michafu ya kuvuruga matokeo,tangia hapo kiongozi yeyote wa uchaguzi asimamapo na mkuhubiri Uhuru wa tume huwa namchukulia kama mchekeshaji tu,mchakato wa uchaguzi haujawahi kuwa huru hata siku moja.
Alaaniwe yule aliyekuwa anatangaza matokeo kadiri alivyokuwa anayapokea bila kujiridhisha matokeo hayo yalikuwa yanapitia wapi kabla ya kumfikia.