Rakesh Rajani-Twaweza Campaign Itawafikia Wengi Zaidi Kupitia SupaMix (East Africa Radio)

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Hivi karibuni nimeanza kuwapata Clouds FM hapa Bukoba. Mida ya asubuhi kwenye kipindi cha Breakfast wanaendesha campaign ya Twaweza-Ni Sisi! Ni campaign nzuri sana kwa somo la Uraia na kujitafutia majawabu ya matatizo yanayoizunguka jamii badala ya kulalama. Nina hofu kubwa na yenye uthibitisho kwamba hii campaign haitaweza kuwafikia waliowengi kwa sababu tu ya chombo cha habari kilichotumika. Jinsi inavyowakilishwa kupitia Breakfast ya Clouds FM, kimaudhui inarushwa kama campaign inayowahusu watu wa Dar es Salaam tu. Mara zote nilipoisikiliza, Bonge alikuwa akiibua matatizo ya Vitongoji vya Dar na kuiwakilisha kimaudhui "ki-bongo-bongo"

Nataka nitoe ushauri kwa Mkurugenzi wa Twaweza, Bw. Rakesh Rajani. Naomba ufikirie upya na kama bajeti ya campaign yako itaruhusu, basi campaign hii irushwe pia kupitia Kipindi cha SupaMix cha East Africa Radio. Hii Redio inafika hapa Bukoba kwa masafa ya FM 89.8. Natumaini pia kwa sasa wanasikika nchi nzima na wanavutia sana kwa rika la kati na juu na kwa yeyote asiyependa "ujana" uliopitiliza. Namaanisha ni kituo cha redio kinachotoa/tuma ujumbe wenye staha unaoweza kusikilizwa na mzazi akiwa na mwana. East Africa Radio wana kipindi kizuri sana kinachoongozwa na Zembwela. Kipindi kinaitwa SupaMix-Sahani ya Jamii. Ni sahani ya Jamii kweli kweli. Kinaibua kero, changamoto na matatizo yaliyo katika jamii husika na hakiishii hapo. Kinakwenda mbali zaidi kuwashirikisha wana Jamii na viongozi husika kuitatuta kero/changamoto au kupendekeza suluhisho kupitia maongezi redioni. Jana hiki kipindi kimenivutia sana. Wananchi waliibua kero, akapigiwa simu Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye ni mwana-ccm, badala ya kuzungumza ni hatua gani amechukua au suluhisho ni nini akaanza kulalamika, akamlaumu Mkuu wa Wilaya na akaomba asaidiwe. Mkuu wa Wilaya naye akatafutwa. Alipoulizwa suluhisho ni nini naye akaanza kulalamika na kutupia lawama serikali. Nikajisemea moyoni tukiendeleza mnyororo huu, tunaweza kufika hadi kwa Rais na yeye badala ya kutoa pendekezo au suluhisho akaishia kulalamika. Hawajui "Wanaweza-Ni Wao!"

Kuna sababu zaidi ya zilizotolewa hapo juu kwa nini kupitia SupaMix – Sahani ya Jamii ujumbe utawafikia wengi. Kwa SupaMix Wananchi huku chini ndiyo wanaoibua kero, changamoto, au mada. Njia ya utatuzi ni shirikishi zaidi, lugha inayotumika inaeleweka na kukubalika na wote (hakuna sheng/slang/lugha za mtaani), Waongozaji wa Kipindi wako makini na mjadala kufikia utatuzi wa kero au changamoto. Nikiyaunganisha haya yote kwa ujumla naona SupaMix – Sahani ya Jamii ikitumika kupitisha campaign ya "Twaweza- Ni Sisi" basi itawafikia wengi na kuonyesha matokeo chanya kwa jamii pana zaidi.

Kanusho:
Omutwale wa Kanyigo hana maslahi yoyote na East Africa Radio, hamjui na wala hajawahi kukutana na Mtangazaji yeyote wa Kipindi cha SupaMix – Sahani ya Jamii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom