Kusanya Kiasi Maalum cha Pesa Kwa Kipindi Maalum kupitia "Capital Campaign"

Feb 5, 2022
31
48
1700769734087.png

Mpango Jumuishi wa Harambee (Integrated Fundraising Plan) ni nyenzo muhimu katika kuiwezesha Taasisi kufikia malengo yake. Mpango huu huiwezesha Taasisi kutekeleza Programu zake na kuiwezesha kujitegemea kiuchumi. Mpango huu unapaswa kujumuisha mipango midogo midogo ifuatayo;
  • Annual Giving Plan (Mpango kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya gharama za uendeshaji wa Taasisi)
  • Major Gift/Special Gift Giving Plan (Mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi/Miradi mikubwa)
  • Capital Campaign (Kampeni ya kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya miundombinu ya Taasisi)
  • Planned Giving or Endowment Campaign (Kampeni kwa ajili ya kutafuta mali za WAKFU kwa Taasisi)
"Capital Campaign" ni kampeni ya kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya miundombinu ya Taasisi. Utekelezaji wa kampeni hii unapaswa kufanyika kwa kipindi maalum na uwe na lengo la kukusanya kiasi maalum cha fedha. . Aina ya miradi inayoweza kutekelezwa kupitia kampeni hii ni kama ifuatavyo;
  • Ujenzi wa ofisi ya Taasisi
  • Ukarabati wa jengo la ofisi
  • Ununuaji wa ardhi kwa ajili ya Taasisi
  • Ununuaji wa fenicha n.k
Taasisi nyingi hutekeleza "capital campaign" kila baada ya miaka 5, 10 mpaka 15. Kiwango cha pesa kinachoweza kukusanywa kupitia kampeni hii hutofautiana kutoka Taasisi na Taasisi, utafiti mdogo uliofanywa na GivingMatters.com unaonyesha kwamba kiasi kinachoweza kukusanywa kupitia kampeni hii huanzia Dola za Kimarekani 100,000 mpaka 2,000,000.
Ili kampeni hii ifanikiwe, vitu vifuatavyo vinapaswa kuzingatiwa;
  • Ushirikishwaji wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi. Wajumbe wa bodi wanapaswa kuonyesha mfano katika kufanikisha kampeni. Ijapokuwa wajumbe wa bodi hutumika kuunganisha wafadhili na Taasisi husika, kwenye uchangiaji, nao pia wanapaswa kushiriki kikamilifu kwenye uchangiaji kabla ya kuwafata wafadhili wengine (other constituencies)
  • Kutumia "one-on-one solicitation" . Kampeni hii hushughulika na wafadhili walio karibu na Taasisi (first and second level constituencies) hivyo basi katika kutekeleza kampeni, Taasisi inapaswa kumtumia mtu maalum kwa ajili ya kukutana na mfadhili husika.
  • Kuwa na watendaji wenye ujuzi na uzoefu. Kufanikiwa kwa kampeni hii kwa kiasi kikubwa kunatagemea watendaji wenye ujuzi na uzoefu. Ikiwa Taasisi ina uhaba wa watendaji wenye sifa na ujuzi stahiki, inashauriwa kutumia rasilimali kutoka nje ya Taasisi (Consultancy Service)
  • Kuandaa jedwali la viwango vya ufadhili unaohitajika (Table of Gifts Needed). Katika uandaaji wa jedwali hili ni vyema kufahamika kwamba asilimia 15-20 ya wafadhili huchangia asilimia 80 ya kiasi kinachohitajika na asilimia 80 ya wafadhili huchangia asilimia 20 iliyobaki.
  • Kuwafuata wafadhili waliofadhili Taasisi kupitia mipango mingine midogo midogo kama vile "Annual Giving Plan" na "Major Gift/Special Gift Giving Plan". Kuwa na mpango jumuishi (integrated fundraising plan) kunaiwezesha Taasisi kusajili wafadhili (donors recruiting) hatua kwa hatua. Usajili wa wafadhili katika Taasisi huanzia katika kampeni ya Mwaka "Annual Giving Plan", kisha wafadhili hawa huingizwa kwenye "Major Gift/Special Gift Giving Plan" baada ya hapo ndipo wanaweza kuwa engaged kwenye "Capital Campaign"
  • Kuandaa " case for support" Mpango wowote wa harambee unapaswa kuandaliwa "case for support". Case for Support inaweza kuwa mchanganuo wa mradi (Project Proposal) Mpango wa Biashara (Business Plan). Case of Support inapaswa kuonyesha kwa namna gani Taasisi itaweza kushughulikia tatizo husika na inapaswa kuandaliwa kwa ustadi.
  • Kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza utekelezaji wa kampeni . Kwenye upembuzi yakinifu maswali yafuatayo yanapaswa kuulizwa; case for support inaendana na dira pamoja na malengo ya Taasisi? kiasi gani cha pesa kinahitajika na kwa viwango vipi (gift's levels) ? , fedha hizi zitarajiwa kutoka kwenye vyanzo vipi ?; mtu mmoja mmoja, kampuni au Taasisi ? Je utekelezaji wa kampeni unaweza kuleta madhara kwa jamii ? kwa namna gani jamiii itahamasishwa kuunga mkono kampeni ?
Ahsante
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Back
Top Bottom