Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Mkali wa kipindi cha radio cha Planet Bongo na mkali wa kipindi cha TV cha Friday Night Live "Dullah Planet" wa kampuni ya utangazaji ya East Africa Radio & TV, siku ya leo ametangaza kuaga Rasmi Kituo hicho cha utangazaji. Kupitia Viwanja mlimani city mtangazaji huyo amefanya sherehe fupi ya kuaga na shukrani nyingi akizimwaga kwa wafanyakazi wenzake.
1696334871373.jpg

Alisema
"Naomba radhi kwa yeyote nitakayekuwa nimemkwaza katika miaka yangu 15 ya utumishi wangu pale East Africa TV/East Africa Radio kwa sababu binadam tunatofautiana kufikiria unaweza ukafanya kitu kwa nia njema mwingine ikamkera na ikapelekea kukuchukia kabisa" -

"Najua nimefanya kazi nzuri najipongeza mwenyewe. Kwa sasa nitaenda break kidogo najua maswali yatukuwa mengi kuuliza naenda wapi au radio gani? Ikifika time ya come back kila mmoja atajua na ataelewa Dullah anafanya nini" -

"Nimeinsipire watu wengi kufanya utangazazaji na watangazaji wanaochipukia wana la kujifunza kutoka kwangu. Nimefanya kazi kwenye Media moja miaka 15".

"Dullah haachi utangazaji ila anaondoka East Africa TV na East Africa Radio. Mimi ni mtangazaji na bado naudai kinoma utangazaji, nabadili tu mazingira ya kazi".

Dullah Planet akizungumza na waandishi wa habari Mlimani City
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom