Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,543
- 664
Kwanini huyu rais hatulii ofsini yeye muda wote anawaza kupaa angani tu. Juzi katoka Marekani kumtafutia Diamond promota jana kapaa kwenda Tabora kuzindua mradi wa tiba ya saratani ina maana kazi kama hii angefanya hata katibu mkuu wa wizara lakini inafanywa na rais wa nchi hivi ni lini atakaa ofsini atulie na atafakari jinsi ya kushughulikia matatizo ya nchi, kutwa kucha yupo angani hata akirudi nchi hataki kutulia ofsini hivi ni muda gani ambao wasaidizi wake humpa ripoti na kuweza kushughulikia matatizo hayo au nchi umemkabidhi nani?Watanzania tumeula wa chuya kwa uvivu wa kuchaguasiamini akili za watanzania eti wakamuacha Prf Lipumba na Dr slaa wakamchagua Kikwete.
Nadhani atakaa ofisini (kwake) atakapokuwa ametoka Ikulu kuangalia malimbikizo (miradi yake binafsi) aliyotufisadi kwa kutoitumikia vyema fursa aliyopewa na wananchi kuwatumikia. Hakika huyu ni rais wa aina yake katika nchi yetu. Nadhani hakiki hatutapata rais wa viwango hivi. Du, hii kali kweli!