Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Hassan Mwinyi, apongeza ripoti ya Finscope kwa kuakisi sekta ya fedha

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
● Asema upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha Zanzibar sasa zimekua kwa zaidi ya asilimia 80.

IMG-20240328-WA0008.jpg

Zanzibar Jumatano Machi 27, 2024: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Ripoti ya FinScope Tanzania 2023 kwa upande wa Zanzibar, ambayo imetolewa muda si mrefu, inaaksi hali halisi ya sekta ya fedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti kwenye Ukumbi wa Golden Tulip wa Uwanja wa Ndege, Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi ambaye aliwakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh. Hemed Suleiman Abdallah, alisema ripoti hii ni nyenzo muhimu inayoweza kutumika na wadau wote wa sekta ya fedha kama dira yetu ya kufanyia maamuzi sahihi ili kuendeleza sekta ya fedha nchini Zanzibar.

Alisema sote ni mashahidi wa namna ambavyo matokeo ya Utafiti wa Finscope Tanzania 2017 ripoti ya Zanzibar, yalivyosaidia michakato mbalimbali ya kuboresha na kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma jumuishi za fedha kwa wananchi.

"FinScope imesaidia watunga sera kufanya mapitio ya sera kikamilifu, kuunda zana za ufuatiliaji kwenye sekta ya fedha, na kuweka mikakati ya kuongeza ustawi na huduma jumuishi za fedha. Kwa wadau wa sekta binafsi, FinScope imewasaidia kubuni bidhaa na huduma za fedha zinazoendana na soko na kukidhi mahitaji ya wateja."

Alieleza kwamba sote tunafahamu kuwa kuna uwiano mkubwa kati ya maendeleo ya sekta ya fedha, ustawi wa huduma jumuishi za fedha, kukua kwa uchumi na kupatikana kwa maendeleo endelevu. Alisema tafiti mbalimbali zinadhihirisha kuwa maendeleo kwenye sekta ya fedha ni chachu ya shughuli za kiuchumi na hivyo ni njia ya moja kwa moja ya kupunguza umaskini.

"Nimefarijika kusikia kuwa tangu ulipotoka utafiti wa kwanza wa Finscope Tanzania ripoti ya Zanzibar mwaka 2017, upatikanaji na utumiaji wa bidhaa na huduma rasmi za fedha umeongezeka, hivyo kiwango cha huduma jumuishi za fedha kimeongezeka kutoka asilimia 45 kwa mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 82 mwaka 2023. Hii ina maanisha kwamba juhudi zetu za kutatua changamoto zinazopelekea ukosefu wa huduma jumuishi za fedha, hasa kwenye maeneo ya vijijini, zimeleta mafanikio."

Hata hivyo, alisema bado kuna kazi kubwa kuhakikisha Wananchi wa Zanzibar wenye umri wa kufanya kazi, hususan wanawake, wanafanikiwa kupata kipato binafsi ili kupunguza hali tegemezi na kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma mbalimbali za fedha ili kuboresha ustawi wa maisha yao ya kila siku pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

"Tunaposherekea mafanikio kwenye huduma jumuishi za fedha, sina budi kutambua nafasi ya taasisi za fedha na namna walivyo wajibika kwenye ubunifu wa teknolojia, bidhaa na vumbuzi za kukidhi mahitaji ya wateja. Kama mlivyosikia, ripoti inaonesha kuwa kuongezeka kwa matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi ndiyo kumechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa huduma jumuishi za fedha."

Alisema kampuni za simu zimeboresha mifumo yao ya biashara na kubuni bidhaa mbalimbali zinaosaidia ujumuishi kwenye sekta ya fedha. Alieleza kwamba kuna ubunifu kwenye karibu ya kila aina ya huduma ya fedha. Hata hivyo, alisema kama ilivyoainishwa na wawasilishaji wa ripoti hapo awali, bado tuna mengi ya kufanya ili wale wote waliofikiwa na huduma za fedha, watumie huduma hizo kwenye shughuli zao za kila siku, mathalani kufanya malipo kwa njia za kidijitali.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuhakikisha kuwa maendeleo ya sekta ya fedha na hali ya huduma jumuishi za fedha nchini vinaimarika.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum alisema anaamini kwamba wakati matokeo yalipokuwa yakiwasilishwa, wengi wetu tulikua tukilinganisha matokeo halisi ya FinScope Tanzania 2023-Ripoti ya Zanzibar na yale tuliyokuwa tukiyafikiria kinadharia.

IMG-20240328-WA0007(1).jpg

Hata hivyo, alisema baadhi ya matokeo tuliyoyasikia kutoka kwenye ripoti hiyo yalikuwa ya kushangaza, wakati mengine yalikuwa yanaendana na matarajio yetu. Baadhi ya matokeo ambayo yanaweza kuwa ya kushangaza kwa baadhi yetu, hasa watungaji na wasimamizi wa sera, pamoja na watoa huduma za fedha, ni yale yanayoonesha mambo yafuatayo: kwanza, kuongezeka kwa matumizi ya bima rasmi kutoka asilimia 4 mwaka 2017 na kufikia asilimia 8 mwaka 2023.

"Tunaweza kusema hiki ni kiwango kidogo ukilinganisha na takwimu za Bara, ila matumizi finyu ya bima rasmi, hususani bima ya afya, hutokana na kuwa Serikali ya Zanzibar inatoa huduma za afya bure katika hospitali na vituo vyote vya afya vinavyomilikiwa na serikali, hivyo kupunguza uhitaji wa bima mbadala. Hali hii inatarajiwa kuendelea haswa kufuatia kuanzishwa kwa Mfuko wa Bima kwa Wote," Alisema.

Pili, asilimia 36 ya walioshiriki kutoa maoni yao kwenye utafiti wa Finscope Tanzania 2023 ripoti ya Zanzibar walisema kwamba kipato chao hutegemea wengine aidha kwa kutumiwa pesa taslim au kugharamiwa mahitaji yao na ndugu, jamaa na marafiki.

Tatu, licha ya hatua kubwa iliyofikiwa kwenye upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha, bado kuna wananchi ambao wanashindwa kufikiwa na huduma hizi kwa kukosa Nambari au Kadi ya Utambulisho. Kwa mujibu wa ripoti hii, asilimia 72 tu ya Wazanzibari ndio wanamiliki kitambulisho cha ukaazi Zanzibar.

Nne, takriban nusu ya watu wazima wenye umri wa miaka 55 au pungufu, hawana pensheni ya uzeeni/mafao ya kustaafu.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango, Zanzibar,Mhe. Dkt. Juma Malik Akil alisema, "Sote tumeshuhudia juhudi kubwa na za makusudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kwa kushirikiana na watoa huduma za fedha kutoka sekta binafsi ili kuboresha miundombinu, bidhaa na huduma za fedha."
 
Asante kwa taarifa mkuuu
 
Back
Top Bottom