FinScope Tanzania 2023 Yazinduliwa Rasmi Jijini Dar es Salaam

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Jumatatu Julai 10, 2023: Ripoti mpya ya FinScope Tanzania 2023, ambayo ni ya awamu ya tano
katika mfululizo wa tafiti bora zinazotambuliwa inchini, imezinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo imezinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Natu Mwambana
akiwa ameambatana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Ujumuishaji wa Huduma za Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba.

Utafiti huo hupima mahitaji, upatikanaji na matumizi ya huduma zafedha Tanzania Bara na Visiwani.

Utafiti uliozinduliwa mwaka huu ni mwendelezo wa tafiti zilizofanyika miaka ya 2006, 2009, 2013 na 2017, ambazo zililenga kufuatilia na kulinganisha mifumo yote ya matumizi ya huduma rasmi za fedha na zisizo rasmi kwa takriban miongo miwili.

Katika maelezo yake wakati wa uzinduzi huo, Dk. Natu Mwamba alisema, “Nimeridhishwa kuona
ripoti ikionyesha kwamba ujumuishaji wa huduma rasmi za fedha umeimarika kwa kiasi kikubwa tangu utafiti wa mwisho uliofanyika mwaka 2017, ambapo ripoti imeonyesha ufanisi umeongezeka kutoka asilimia 65 hadi asilimia 76 .

Pia kwamba tofauti ya uwiano wa ujumuishaji wa huduma za fedha baina za jinsia zote umepungua kwa kiwango kikubwa.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kusema kuwa "bado kuna kudorora kwa pengo jinsia katika
ujumuishi wa huduma zazinazotolewa na mabenki", ambapo aliitaja kuwa ni fursa kubwa kwa wawakirishi wa taasisi za kibenki.

Zaidi ya hayo, alitoa wito wa dhati kwa sekta ndogo ya bima kuchukua hatua maridhawa.

Tofauti na sekta nyingine ndogo, uenezaji wa huduma za bima umepungua (kutoka asilimia 15
hadi 10), hali ambayo pia ni kinyume na lengo la Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya
Fedha, ambao unakusudia kufikia asilimia 50 ya watu wazima kupata na kutumia huduma za bima ifikapo 2023,” alisema.

Juhudi madhubuti zinahitajika kwa watunga sera, wadhibiti pamoja na watoa huduma za fedha na wabunifu ili kukabiliana na changamoto za sekta kwa upana wake kwa kutoa bidhaa mpya zitakazokidhi mahitaji ya Watanzania ya kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Wakati huo huo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesisitiza
zaidi juu ya umuhimu wa tafiti kama FinScope Tanzania kwa ajili ya kuendelea kupima hali ya
ujumuishwaji katika huduma ya kifedha, na umuhimu wake katika upimaji na uundaji wa Mpango
wa Taifa ya Ujumuishwaji wa Huduma za Fedha kwa ujumla.

Aidha aliwahakikishia wajumbe hao kuwa mwelekeo ulioonyeshwa na FinScope Tanzania 2023, hususani mapungufu, ambayo yameonyesha wazi hitaji kubwa la matumizi ya mara kwa mara ili
kuongeza ukuaji wa fedha, utaarifu mabadiliko muhimu katika Mpango mpya wa Ujumuishwaji wa Huduma za Fedha wa 2023-2026, ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Katika maelezo yake, Bw. Eric Massinda, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) alisema, "Uzinduzi wa ripoti ya matokeo haya muhimu ni mwanzo tu wa ushirikishaji mkubwa wa sekta ya umma katika harakati za kuiwezesha sekta kufanya maamuzi kutokana na Ushahidi wa kina na uundaji wa bidhaa katika sekta ya fedha”.

Alisema kutakuwa na ushirikishaji na mazungumzo ya kina na wadau kwa ajili ya kupanua wigo
wa usambazaji wa matokeo ya FinScope Tanzania 2023 kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Kuhusu ripoti ya FinScope Tanzania 2023

FinScope Tanzania ni utafiti wa kina wa mahitaji ya sekta ya kifedha kwa watu wazima wa
Kitanzania wenye umri wa kuanzia miaka 16 na kuendelea.

Ripoti hii inatoa ufahamu wa hali ya matumizi ya huduma za kifedha nchini kote na ni kipimo cha kuaminika kwa mahitaji na matumizi ya huduma za kifedha katika makundi mbalimbali ya watu.

Zaidi ya hayo, ufahamu wa FinScope Tanzania unaonyesha wazi vikwazo na viwezeshi vya
ujumuishwaji wa huduma za fedha.

Utafiti huo una malengo makuu matano:

Kuelewa tabia (usimamizi wa mtiririko wa fedha, kuwekeza, kuweka akiba n.k.) na kufafanua
mahitaji ya huduma ya kifedha ya watumiaji (watu binafsi, wakulima, wamiliki wa biashara, nk).

Kuweka viwango vya kuaminika na kupima ufanisi wa ujumuisho wa kifedha na maendeleo
yaliyopatikana kuelekea malengo ya kitaifa chini ya NFIF, FSDMP, pamoja na mipango mingine ya
maendeleo ya kitaifa.

Kutoa ufahamu kuhusu vikwazo vya kisera, udhibiti na soko katika upatikanaji na matumizi ya
huduma za kifedha.

Kutoa maarifa ambayo yatachangia katika ubunifu ndani ya sekta ya fedha na uchumi halisi.

Kuangazia fursa za mapitio ya sera zinazohitajika ili kuendeleza sekta ya fedha.

FinScope Tanzania 2023 ni mwendelezo wa tafiti zingine tano katika mfululizo wa FinScope

Tanzania, ambapo imetanguliwa na nyingine zilizofanyika miaka ya 2006, 2009, 2013 na 2017.

Utafiti huo unatekelezwa na washirika wakuu wa utekelezaji wake ambao ni pamoja na; Wizara ya Fedha na Mipango Tanzania Bara na Zanzibar sambamba na Benki Kuu ya Tanzania, Taasisi ya Uimarishaji Sekta ya Fedha nchini Tanzania (FSDT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS).
 
Back
Top Bottom