Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume ameushauri uongozi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, kuchukua hatua kutatua tatizo la kujaa kwa maji katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar, taarifa ya Ikulu imeeleza.
Rais Karume alitoa ushauri huo jana, wakati akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua kubwa katika mji wa Zanzibar.
Rais Karume katika ziara hiyo alifuatana na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Mabrouk Jabu na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi, pamoja na wataalamu wa Michirizi katika mji wa Zanzibar.
Alisema kuwa amesikitishwa sana na mtatizo yaliyowakumba wananchi waliofikwa na maafa hayo, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa wastani wa masaa 35, kuanzia juzi hadi jana asubuhi.
Aidha Rais Karume, katika juhudi zinazopashwa kuchukuliwa, alisisitiza uongozi wa Baraza la Manispaa, kwa kushirikiana na taasisi nyengine, kuhakikisha kuwa hatua zinachukuliwa kudhibiti tatizo la mripuko wa maradhi yanayotokana na maji machafu yaliyotuwama pamoja na tatizo la kuwepo kwa takataka nyingi katika mitaa zilizochanganyika na maji yanayoingia katika nyumba za makaazi ya wananchi.
http://www.zanzibargovernment.org/