Rais wa ZANZIBAR akiwa kazini

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume ameushauri uongozi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, kuchukua hatua kutatua tatizo la kujaa kwa maji katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar, taarifa ya Ikulu imeeleza.

Rais Karume alitoa ushauri huo jana, wakati akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua kubwa katika mji wa Zanzibar.

Rais Karume katika ziara hiyo alifuatana na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Mabrouk Jabu na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi, pamoja na wataalamu wa Michirizi katika mji wa Zanzibar.

Alisema kuwa amesikitishwa sana na mtatizo yaliyowakumba wananchi waliofikwa na maafa hayo, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa wastani wa masaa 35, kuanzia juzi hadi jana asubuhi.

Aidha Rais Karume, katika juhudi zinazopashwa kuchukuliwa, alisisitiza uongozi wa Baraza la Manispaa, kwa kushirikiana na taasisi nyengine, kuhakikisha kuwa hatua zinachukuliwa kudhibiti tatizo la mripuko wa maradhi yanayotokana na maji machafu yaliyotuwama pamoja na tatizo la kuwepo kwa takataka nyingi katika mitaa zilizochanganyika na maji yanayoingia katika nyumba za makaazi ya wananchi.


http://www.zanzibargovernment.org/
 
Maeneo yenye kero kubwa kwa kujaa maji ni kama vile Uwanja wa Mnazi Mmoja! Barabara ya Benjamin Mkapa sasa ina nafuu kubwa, shukrani kwa awamu ya kwanza mradi wa Michirizi...

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa anapaswa kuangalia tena uwezekano wa kushawishi awamu ya pili ya Mradi wa michirizi kutatua matatizo ya maji ya mvua na hasa sehemu za Ng'ambo
 
Kama alivyokwisha sema siku za nyuma kuwa uchumi ameunyanyuwa na ukitaka kujuwa hilo alisema angalieni kila mtu sasa amekuwa na Mobile
 
Kama alivyokwisha sema siku za nyuma kuwa uchumi ameunyanyuwa na ukitaka kujuwa hilo alisema angalieni kila mtu sasa amekuwa na Mobile

My God!!! Just a mobile???????? Nakumbuka enzi zangu za utoto kupata kitoweo kama nyama ilikuwa nadra sana ikitokea hivyo tulidhani ni sikukuu. Kasumba hiyo hadi leo watoto wengi wanayo kukiwa na mlo kama wali kwa kitoweo watoto watatembea kwa majirani zao na kuwaambia sisi leo sikukuu. Sasa je Mobile ni kigezo cha kuinuka uchumi??????
 
Kama alivyokwisha sema siku za nyuma kuwa uchumi ameunyanyuwa na ukitaka kujuwa hilo alisema angalieni kila mtu sasa amekuwa na Mobile
Duh!!!
labda sijaelewa fresh hapa.... umesema "kila mtu amekuwa na mobile" kwamba anamiliki simu ya mkononi au "Kila mtu amekuwa mobile" kwamba anamiliki kifaa cha kusafiria kama Gari, pikipiki, vespa au baiskeli n.k??

Huyu Karume yawezekana anafanya kazi kubwa ila hana interpersonal & communication skills nzuri ili kuufanya uma kujua kazi zake. Anyway his time will be up in 2yrs! May be atatoa ripoti kabla hajaondoka...
 
Vipi Balahau. Wau;ize watu wa CUF. Watakuedleza. Lakini usiwaulize hadharani kwani weatakup;[iga makofi uanguke.
 
Hivi kuna mtu anajua huyu mtu tangu awe rais keshaifanyia nini Zanzibar?

...'nasikia' kamalizia yale majumba ya michenzani (mbele ya polisi madema na kisima majongoo), ambayo maraisi walomtangulia kina Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi, Babu Idrissa Abdulwakil na Komandoo Salmin Ibn Amour waliyashindwa kuyaendeleza!

Sijafika Zbar mwaka wa tatu sasa, ila naskia 'maghorofa' ya wawekezaji alhamdulillah huko, mji wabadilika na mahoteli ya kitalii ya hadhi ya nyota tano yanajengwa na kufunguliwa katika fukwe za Unguja.
 
Ah Balahau we. Waulize watu wa CUF. Wanayajuwa fika maendeleo tuliyopata, na Karume anaendela kufanya nini katika kuleta maendeleo ya Zenj. Lakini (indhari). Uwaulize pembeni kwenye vijiwe vya kahawa. Ukiwauliza hadharani, jihadhari na kuchapwa makofi ukaanguka chini. Ndivyo Ilivyo Abaa!!!!!!
 
Back
Top Bottom