Rais Samia aendelea kukuza Mahusiano ya Kidiplomasia

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Nchi ya Tanzania imeendelea kufungua milango ya kidiplomasia kwa Mataifa ya nje tangu serikali ya awamu ya sita ichukue kijiti. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan azidi kuonesha umahususi wake katika kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea. Leo anaenda kupokea ugeni uzito kutoka Ujerumani kwa kumpokea kiongozi wa nchi hiyo, Rais Frank-Walter Steinmeier, atakayefanya ziara ya siku tatu kuanzia Oktoba 30 hadi 01 Novemba 2023.

Rais Steinmeier ataambatana na viongozi wengine wa serikali, pamoja na wawekezaji wa makampuni makubwa 12.Moja ya malengo ya ziara hiyo ni kudumisha uhusiano wa kidiplomasia uliyodumu kwa zaidi ya miaka 60 na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kwenye kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Matarajio ya ziara hiyo ni pamoja na kushiriki katika jukwaa la Biashara, litakalohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo mbili, lililoandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania.Hii ni kutaka kufungua fursa za kibiashara baina ya Tanzania na Ujerumani pamoja na kufungua mianya ya uwekezaji kwa nchini. Tanzania imekuwa ikiuzia Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka huku ikiagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa dola za Kimarekani milioni 237.43.

Nchi hizi mbili ukiachia mbali kuwekeza katika biashara, pia zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususan biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni. Kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini.Hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.

Kufanyika kwa ziara hii ni ushahidi tosha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza diplomasia ya serikali anayoiongoza. Tanzania inazidi kunufaika na utendaji kazi na siyo maneno maneno. Tunayo kila sababu ya kuendelea kufanya kazi kulijenga Taiifa letu, kwani Tanzania ni yetu sote.
IMG-20231030-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom