Rais wa Senegal atangaza msamaha wa jumla kwa wapinzani wa kisiasa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Taifa hilo la Afrika Magharibi linakabiliwa na mzozo mbaya wa kisiasa katika kipindi cha miongo kadhaa baada ya Sall kuahirisha gafla uchaguzi wa rais wa Februari 25 saa chache kabla ya kampeni ya uchaguzi huo kuanza.

Sall ameitangaza hatua hiyo ya msamaha kama njia ya kuiunganisha nchi, baada ya msururu wa maandamano kuua watu kadhaa katika miaka mitatu iliyopita.

Mamia ya wapinzani, au zaidi ya wapinzani 1,000 kulingana na makundi ya haki za binadamu, walikamatwa tangu mwaka wa 2021 kufuatia mvutano wa kuwania madaraka kati ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na serikali.

Sonko na mgombea wa chama chake, Bassirou Diomaye Faye wanafungwa jela.

“Katika ari ya maridhiano ya kitaifa, nitawasilisha mbele ya bunge Jumatano hii katika baraza la mawaziri muswada wa msamaha wa jumla kwa vitendo vinavyohusiana na maandamano ya kisiasa yaliyofanyika kati ya 2021 na 2024”


DW
 
Ni jambo jema, amani ni tunda la haki.

Msamaha huo uendane na uchaguzi huru na haki, akishindwa akubaliane na matokeo.
 
Ni jambo jema, amani ni tunda la haki.

Msamaha huo uendane na uchaguzi huru na haki, akishindwa akubaliane na matokeo.
Nikuelimishe kidogo. Sall hagombei Keshamaliza 2nd term. Aliahirisha uchaguzi ili aendelee kuwa madarakani Hadi Oct.
 
Hivi hawa viongozi wa Afrika ikifika mwisho wa mihula yao huwa wanakuwa wamesahau nini mle kwenye uongozi ndio waanze kungangania madaraka? Damu zinamwagika wala hawahofii wanajipiga upofu ilimradi watawale.
 
Back
Top Bottom