Baraza la Katiba Senegal lafuta kura ya kuahirisha uchaguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Baraza la Katiba la Senegal limebatilisha tangazo la kuchelewesha uchaguzi wa rais uliokuwa ufanyike mwezi huu likisema kura ya bunge ilikuwa kinyume na katiba.

Baraza hilo Katiba la Senegal limesema kuwa muswada uliopitishwa na bunge wa kuchelewesha uchaguzi ulikuwa kinyume na katiba, kulingana na nyaraka iliyothibitishwa na chanzo ndani ya taasisi hiyo.

Soma pia: Uchumi wa Senegal kuzorota kutokana na mkwamo wa kisiasa

Aidha, taasisi hiyo ya katiba pia iliwahi kubatilisha agizo la Rais Macky Sall la Februari 3 ambalo lilirekebisha kalenda ya uchaguzi wiki tatu tu kabla ya kupiga kura. Baraza hilo linasema kwamba "ni vigumu kuandaa uchaguzi wa rais katika tarehe iliyopangwa hapo awali" lakini likapendekeza "mamlaka zinazofaa kufanya uchaguzi huo haraka iwezekanavyo."

Rais Macky Sall wa Senegal, mapema mwezi huu alitoa tangazo la kuchelewesha uchaguzi ambao awali ulikuwa ufanyike Februari 25. Uamuzi huo umeitumbukiza Senegal katika mzozo mbaya wa kisiasa na kuchochea hasiara kubwa ya umma na maandamano ya vurugu.

Baadae bunge la nchi hiyo liliidhinisha tangazo la kuchelewesha uchaguzi hadi Desemba 15, lakini baada ya vikosi vya usalama kuvamia majengo ya bunge na kuwaondoa baadhi ya wabunge wa upinzani waliokuwa wakipinga muswada.

Kura hiyo ilipisha njia kwa rais Sall, ambaye mamlaka yake ya muhula wa pili yanatarajiwa kumalizika mwezi Aprili, kuweza kusalia mamlakani hadi mrithi wake atakapopatikana, pengine si kabla ya 2025.

Akiwa amekabiliwa na hasira ya umma inayozidi kuongezeka, Rais Sall ameonyesha nia ya kutafuta njia za kupata "maridhiano".

Uamuzi huo wa Baraza la katiba umetolewa wakati wapinzani kadhaa wa serikali waliokuwa wanazuiliwa wakianza kuchiliwa huru kutoka gerezani, katika juhudi zinazoashiria kwamba Rais Sall anatafuta kutuliza hasira ya umma.

Ousmane Sonko, ambaye ni mmoja wa wapinzani wakuu wa Sall, amezuiliwa tangu 2023 lakini hapajakuwa na taarifa za uwezekano wa kuachiliwa kwake.
 
Katika Afrika Magharibi ni hiyo Senegal peke yake ambayo haijawahi kutawaliwa kijeshi toka ilipopata uhuru mwaka 1960 kutoka Ufaransa lakini kwa huu ujinga unaofanywa na huyu rais Macky Sall huenda siku moja historia ikaandikwa upya.

Ujinga unaofanywa mara kwa mara na watawala wa kiafrika, Tanzania ikiwemo, utafanya mataifa yote ya kiafrika yaonje tawala za kijeshi.
 
Back
Top Bottom