Rais wa Romania, Klaus-Werner Iohannis kufanya ziara ya Kiserikali Nchini Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,782
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Daily news, Rais huyo wa Romania atawasili Nchini tarehe 16 Kwa ziara ya siku 3 ambapo pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais Dk Samia.

==========

Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya kiserikali ya siku nne.

Ziara hiyo, inayotarajiwa kuanza Novemba 16 hadi Novemba 19, 2023, ni sehemu ya ziara kubwa inayojumuisha nchi nne za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, Cape Verde, na Senegal, ikisisitiza azma ya Romania ya kukuza uhusiano imara na bara la Afrika.

Ziara ya Rais Iohannis imeundwa kwa mkakati ili kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi, na kitamaduni kati ya Romania na Afrika.

Rais Iohannis atashiriki katika mashauriano muhimu ya kisiasa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake nchini Tanzania.

Hii inaashiria dhamira mpya ya kukuza upya mahusiano ya Romania na bara la Afrika, ikilinganishwa na juhudi kubwa za kufufua mahusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika.

Chanzo: Romania President to visit Tanzania - Daily News

My Take
Hakika nyota ya Mwandiplomasia namba 1 wa Tanznaia Rais Samia inawaka manaa wanapishana wenyewe huko angani kuja Tanzania 🔥🔥

Karibu sana Tanzania

20231114_153456.jpg

a.JPG

aa.JPG
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa Romania mh Klaus Werner lohannis anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi Nchini Tanzania kuanzia Tarehe 16 hadi 19 mwezi huu.ambapo masuala mbalimbali yanatarajiwa kuzungumzwa katika kuimarisha ushirikiano na mwenyeji wake Rais mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika,jasiri muongoza njia,simba wa nyika,nuru ya wanyonge,Sauti ya Afrika,mtetezi wa wanyonge na tumaini la watanzania.

Tanzania inaendelea kuwa kivutio cha wengi na kila mtu anatamani kufanya kazi na Tanzania, kushirikiana na Tanzania Na kuungana na Tanzania Katika masuala mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa, kidiplomasia,n.k. hii inakuja ndani ya muda mfupi wa kuwa madarakani kwa Rais samia ambapo ameipaisha sana Tanzania na kuiweka katika kilele cha macho ya Dunia , ambapo sasa inatazamwa na kila Taifa kama Taifa la kuheshimika na kuigwa kabisa kutoka barani Afrika.

Ndio maana tunaona ndani ya muda mfupi tumeweza kama taifa kupokea viongozi mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali,ujumbe wa viongozi kutoka kila sehemu,.tuliona makamu wa Rais wa Taifa kubwa kabisa hapa Dunia yaani Marekani akiitembelea Tanzania,tumeona juzi juzi tu hapa tumetoka kumpokea Rais wa Ujerumani.

Tanzania imekuwa ni kama maji tu usipoyanywa utayaoga tu.ndio maana tunaona mafuriko ya watalii, wafanyabishara wakubwa, wawekezaji wakimiminikia na kufurika Tanzania.hii yote ni kazi ya Rais samia,ni mikono ya Rais samia,ni juhudi za Rais samia,ni maono ya Rais samia,ni ushawishi na nguvu za Rais samia,ni matunda za ziara ambazo amekuwa akifanya Rais samia nje ya nchi,ni mikakati na mipango ya Rais samia katika kuhakikisha tunakuwa wakwanza katika kuzoa fursa zote zinazopatikana katika uso wa Dunia na hii yote inatokana na kukubalika kwa kiwango cha juu kwa Rais samia na namna anavyoheshimika ,kupendwa na kukubalika ndani na nje ya Taifa letu.

Tuendelee kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa kituo cha Biashara,uwekezaji na utalii barani Afrika vitu vitakavyotupatia fursa nyingi za kiuchumi na kukuza uchumi wetu kwa kasi ya upepo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Mnafurahia mabeberu kuja nchini na hamjui nd tunazidi kunyonywa unaomba msaada wao wanakuja kukomba utajiri alafu unasema tunafumisha uhusiano inabidi ije itokee tupate raisi mzalendo kama jpm au Museveni hawana shida na misaada ya nje lakn bado nchi zetu zinazalisha viongozi ambao bado ni dependacy
 
Wasije tu kumpiga mazeli wetu

Tu,maama hawa janjajanja tu

Ova
 
Mnafurahia mabeberu kuja nchini na hamjui nd tunazidi kunyonywa unaomba msaada wao wanakuja kukomba utajiri alafu unasema tunafumisha uhusiano inabidi ije itokee tupate raisi mzalendo kama jpm au Museveni hawana shida na misaada ya nje lakn bado nchi zetu zinazalisha viongozi ambao bado ni dependacy
Wazungu magharibi wenyewe wanawaogopaga hawa waromania

Ova
 
Mnafurahia mabeberu kuja nchini na hamjui nd tunazidi kunyonywa unaomba msaada wao wanakuja kukomba utajiri alafu unasema tunafumisha uhusiano inabidi ije itokee tupate raisi mzalendo kama jpm au Museveni hawana shida na misaada ya nje lakn bado nchi zetu zinazalisha viongozi ambao bado ni dependacy
Romania inakunyonya kipi wewe.Ulitaka nani aje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom