Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,105
- 136,775
- Thread starter
-
- #141
Watu wakisema hawaoni kwa sababu wamepewa Radio waves badala ya visible light, ukiwapa Gamma Rays unakuwa bado hujatatua tatizo lao.
Nyani Ngabu mimi nakuelewa vema sana mkuu, ID mpya ndio hazikuelewi.Nyuzi na mabandiko ya Kikwete kuitwa 'rais wa misiba' ni nyingi/ mengi mno humu.
Kwa sisi tuliopo muda mrefu humu na tulio na kumbukumbu nzuri tunayajua hayo.
Wengine hawajapita kwa ngariba hawa bado si bure.
Mshikaji anasema anapishana na mimi lakini hata sioni tunapopishana.
Ndo mambo ya [1] kusoma kitu bila kuelewa na [2] kusoma jambo bila kuwa na an open mind na badala yake kuongozwa na preconceived notions.
Some folks are really funny.
nipo tu nimekuja kumpa pakajimmy pole nyani.miss you
Hata mimi sielewi kwa nini hakwenda kwenye hiyo hafla ya kuwaaga hao maiti.Unajua kila nikifikiria ili jambo na wale wanaotetea Rais kutokuenda kwenye huu msiba nashindwa kuwaelewa. Tunazungumzia watoto thelathini maisha yao yamefupishwa na hii ajali. Rais hajaona umuhimu wa yeye kwenda kuwapa pole hawa wazazi. Hivi ni nini haswa maana ya kuwa kiongozi wa nchi kama hauwezi kushiriki na wananchi wako katika kipindi kama hiki?
Aisee. Nimesikitika sana baba mwenye nyumba kutokwenda
Nyani Ngabu mimi nakuelewa vema sana mkuu, ID mpya ndio hazikuelewi.
Yeye anasemaaa...."Ajali, vifo, misiba na matetemeko havijaletwa na serikali yake, na wala yeye hakuchaguliwa kuleta misiba, matetemeko na mengine yanayofanana na hayo"...inawaudhi tukisema ila haina budi kukumbusha alichowahi kutamka yeye mwenyewe kwa mdomo wake huo usio na breki!Binadamu ni kiumbe changamani sana.
Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.
Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.
Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!
Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.
Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.
Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.
Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.
Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.
Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.
Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.
Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!
Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.
Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.
Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.
Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.
Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.
Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.
Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.
Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.
Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
Mkuu Nyani Ngabu signature yako inajieleza wazi kabisa, hizi lawama za Mh Raisi kutohudhuria zimeanzia USA, na kwa kuwa wameambiwa basi utaonekana unabisha tu.Ni kweli, jamaa kwenye baadhi ya mambo yupo consistent sana....
Kitu gani ambacho ni cha kumlazimu sana rais kwenda pale ambacho hawezi kukifanya bilakwenda pale siku hiyo?Unajua kila nikifikiria ili jambo na wale wanaotetea Rais kutokuenda kwenye huu msiba nashindwa kuwaelewa. Tunazungumzia watoto thelathini maisha yao yamefupishwa na hii ajali. Rais hajaona umuhimu wa yeye kwenda kuwapa pole hawa wazazi. Hivi ni nini haswa maana ya kuwa kiongozi wa nchi kama hauwezi kushiriki na wananchi wako katika kipindi kama hiki?
Nyani Ngabu uko too defensive kwenye ulichokiandika, Otherwise ukiruhusu akili yako Kuwa Huru utaelewa Kuwa Kuna ninapoungana na wewe na Kuna ninapotofautiana nawe.
Mshikaji anasema anapishana na mimi lakini hata sioni tunapopishana.
Ndo mambo ya [1] kusoma kitu bila kuelewa na [2] kusoma jambo bila kuwa na an open mind na badala yake kuongozwa na preconceived notions.
Some folks are really funny.
Rais ana uchawi wa kufufua wafu na kutokuwepokwake kumefanya waliofariki wakose kufufuliwa?
Kimsingi, msiba wa raia wanasiasa hawatakiwi kujazana,hawatakiwi kutoa hotuba.
Kwa sababu wakijazana na kutoa hituba, watafanya msiba uwe ni jukwaa la siasa.
Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.
Al Watan upo vizuri mkuuKitu gani ambacho ni cha kumlazimu sana rais kwenda pale ambacho hawezi kukifanya bilakwenda pale siku hiyo?
Kama serikali imewakilishwa na Makamu wa Rais, kwa nini Rais alazimike kuwepo?
Rais ana uchawi wa kufufua wafu na kutokuwepokwake kumefanya waliofariki wakose kufufuliwa?
Kimsingi, msiba wa raia wanasiasa hawatakiwi kujazana,hawatakiwi kutoa hotuba.
Kwa sababu wakijazana na kutoa hituba, watafanya msiba uwe ni jukwaa la siasa.
Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.
Wewe hudhani.Sidhani kama umesoma ulichoandika...
Al Watan upo vizuri mkuu
Jiwe limerushwa gizani, kumbe limekupata mwenyewe . . ?!Watu ni wa ajabu sana aisee.
Kwa aliyenisoma vizuri ataona kabisa nimesema wazi kuwa naamini ingekuwa ni vyema kama yeye binafsi angeenda kwenye hafla ya kuaga hao maiti.
Lakini mijitu bado inakuja na habari sijui za ukabila...mara sijui za kutaka kuhalalisha matendo ya Magufuli kupitia matendo ya Kikwete...
Oh well...