Rais Uhuru Kenyatta amepunguza bei ya umeme, Tanzania vipi?

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,154
3,797
Katika kusherehekea sikukuu ya Jamuhuri nchini Kenya Rais Kenyatta amepunguza bei ya umeme ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake na pia kusaidia viwanda na wawekezaji kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji.

Kenyatta amepunguza bei hizo kwa 30% kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ya 15% itatekelezwa mwezi huu wa Disemba na awamu ya pili ya 15% nyingine itatekelezwa mwezi Machi mwakani.

Je,viongozi wetu na tanesco wana cha kujifunza kutoka kwa jirani zetu?
 
Mkuu mbona kichwa cha uzi wako hakieleweki? Amepunguzaje umeme huku Tanzania?
 
Kila taifa Lina taratibu zake

Si lazima kuiga Kila kitu

Kuna tozo,ambazo tunakatwa Kila tunapofanya miamala , Kenya hakuna

Tuna kodi za majengo Kila tunaponunua umeme, Kenya hakuna

Tuna miradi mikubwa tunaijenga kwa pesa zetu za ndani,e.g JNHP bwawa la Nyerere Kenya hakuna,

Kwahiyo tulizana bwamdogo
 
Umeme wa Tanzania ni bei rahisi sana kuliko nchi zote za afrika mashariki.

Umeme wa kenya una bei ghali sana.
 
Acha uongo, unit moja ya umeme Kenya ni Shs. 9 za Kenya sawa na Shs. 180 za Tanzania wakati hapa Tanzania unit moja ni zaidi ya Shs. 350!
Ebu tuwekee bei za umeme za Kenya sababu hapa kwetu nadhani kuna watu wananunua umeme kwa Tsh. 100 kwa unit.

Inawezekana hiyo ya Kshs. 9 wanaouziwa uko Kenya hapa kwetu Tanzania ndio tunauziwa Tshs. 100
 
Wewe unashindwa nini kufanya utafiti huo? Nimekupa bei ya wastani ambayo watu wengi wanalipa na siyo hiyo danganya toto ya kutoza bulbs 3!
 
Katika kusherehekea sikukuu ya Jamuhuri nchini Kenya Rais Kenyatta amepunguza bei ya umeme ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake na pia kusaidia viwanda na wawekezaji kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji.

Kenyatta amepunguza bei hizo kwa 30% kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ya 15% itatekelezwa mwezi huu wa Disemba na awamu ya pili ya 15% nyingine itatekelezwa mwezi Machi mwakani.

Je viongozi wetu na tanesco wana cha kujifunza kutoka kwa jirani zetu?
Watapunguza vipi wakati January na genge lake wanataka Ma-generator yaanze kazi? Huoni JNHPP inasuasua. Na kikaragosi anachema bodi zote zilizokuwepo lazima zibadilishwe. Yaani kutoka kwenye NGO hadi kuongoza nchi sio bure, analipa fadhila sasa ngoja Togolani oops ...... janga la taifa, chijui amalize kuipeleka Tanzania kizimu.
 
Na pia wana vyanzo vichache vya umeme kulinganisha na sisi.
Tuangalie data za access to electricity mkuu
IMG-20211105-WA0038.jpg
 
Katika kusherehekea sikukuu ya Jamuhuri nchini Kenya Rais Kenyatta amepunguza bei ya umeme ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake na pia kusaidia viwanda na wawekezaji kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji.

Kenyatta amepunguza bei hizo kwa 30% kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ya 15% itatekelezwa mwezi huu wa Disemba na awamu ya pili ya 15% nyingine itatekelezwa mwezi Machi mwakani.

Je viongozi wetu na tanesco wana cha kujifunza kutoka kwa jirani zetu?
Nchi ya Hangaya wanajali mambo yao tu akina Jenister a.k.a Sugacane tycoons
 
Back
Top Bottom