Rais uendapo Tanga jaribu pia kufatilia shida ya maji Handeni hasa mji mdogo wa Kabuku

Marathon day

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
573
893
Katika Wilaya ya HANDENI tatizo kubwa ni shida ya maji, niliwahi kununua shamba Kijiji cha KABUKU, Nimepitia sehemu nyingi za maeneo hayo, kwakweli watu wanaishi kama wanyama, huwa najiuliza mbunge wa pale hii kero haitambui?

Sijawahi kusikia akiizungumzia bungeni, kule Kila mtu anaejenga nyumba kabla ya yote lazima kuchimba kisima cha kuvuna maji ya Mvua, bila Hilo huwezi ishi mji ule, Kulikua na mchakato wa kufanya mji ule uwe Halimashauri, kinachosemekana Madiwani qalihongwa na baadhi ya matajiri wa mji wa mkata, wakapitisha Halimashauri ikapelekwa Mkata.

Sasa kumekua na Bifu kubwa San kati ya wananchi wa pale na viongozi, najua hata CCM Wilaya wanalijua Hilo lakini wanalificha. Kama CCM Mko makini lisemeeni Hilo kwa viongozi wa juu, hasa kero ya Maji na Hilo la Halimashauri. Muheshimiwa Raisi na hili lichukue uingiapo Mkoa wa Tanga.
 
Katika Wilaya ya HANDENI tatizo kubwa ni shida ya maji, niliwahi kununua shamba Kijiji cha KABUKU, Nimepitia sehemu nyingi za maeneo hayo...
Handeni Trunk Main ilifia wapi? halafu eti wamasai wamependa wenyewe kuhamishiwa huko
 
Kule maji hakuna ni usanii tu unafanyika, na hata ukichimba kisima chini maji yake ni chumvi hataree!! Swala la msingi ni maji yatokayo Ruvu yafike kule, lakini mradi unakwenda mwendo wa Kobe, itachukua huenda miaka 30 kuwafikia wanachi
 
Kule ni maeneo mazuri ya kuwekeza, machungwa yamejaaa,, kiwanda hakuna. Mihogo inakubali sana wawekezaji hakuna, mashamba kule bado yapo Sana tena kwa Bei rahisi, nilishangaa sehemu ambayo unaweza kupata Hadi Ekari 50 Hadi 100 kwa pamoja na Bei rahisi tu, Dunia ya Leo unapata shamba kwa 150,000/ mpaka 200,000/ kwa heka? Tatizo maji na umeme wa uhakika kwa pembezoni.
 
Back
Top Bottom