Rais Samia: Watunza kumbukumbu mnapaswa kutunza siri za Serikali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano Mkuu wa Kumi wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) katika Ukumbi wa AICC, ARUSHA leo tarehe 27 Novemba, 2022



Akifungua mkutano huu, Rais amewashauri wanataaluma wa kada hii kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili haki za watu siziende kudhurumiwa kwani wao ndiyo roho ya serikali.

Kuhusu kumbukumbu za serikali kuonekana mitandaoni mfano barua, wale wa mahakamani kesi ilivyohukumiwa na nyaraka zingine, Rais amesema “Sasa unajiuliza, huyu aliyetoa hizi taarifa anataka umaarufu, rushwa au kitu gani, kwa sababu ulichokifanya, kama kumbukumbu ile inakwenda kumtoa mtu kwenye hatia, au inakwenda kusababisha lolote lile kule nje, chanzo ni wewe uliyekubali kuchukua pesa kutoa hiyo kumbukumbu”

Akifafanua zaidi, Rais Samia amesema kuwa pesa hizo haziwafikishi mbali, bali kuleta uchonganishi ndani ya nchi. Kutoa taarifa za Serikali nje pasipo kufuata taratibu sahihi unakuwa hujafanya jambo la maana.

“Niwaombe sana na niwaase, watunza kumbukumbu wenzangu, mimi mama yenu, sisi wazazi wenu, hatukufanya hivyo. Na ninyi tunzeni siri za Serikali. Nendeni mkafanye kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa” amesema.

Pia, Rais ametoa hakikisho la kuwalinda wafanyakazi wa kada hii kwa kutambua kuwa wao ndiyo kitovu cha kazi zote za Serikali.
 
Hata sheria ukitoka kwako ukaenda mahakamani na kusikiliza kesi unaweza kuwa mwanasheria mzuri tu na ukawa unasaidia watu everything need experience na exposure, same to nursing, medical doctors na n.k


Nyie ndio Bashiru kasema hamna maana.
 
Kigogo alipokua anatoa siri za serikali awamu ya tano mlifurahia.
 
Back
Top Bottom