Agizo la Rais Samia kwa "Trumpa" na "Tapsea" latekelezwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuandaa mkutano wa Watunza Kumbukumbu na Makatibu Mahsusi, limetekelezwa. Serikali imewaagiza waajiri, taasisi za umma na binafsi nchini, kuwaruhusu watumishi wa kada hizo ambao ni wanachama wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRUMPA) na Wanachama wa Chama Cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) na kuwagharamia kushiriki mkutano huo.

Agizo hilo, lilitolewa jijini hapa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo.

Simbachawene alisema kwamba, mgeni rasmi katika mkutano huo, anatarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkutano huo, utakaowakutanisha washiriki zaidi ya 8,000, utaanza leo hadi Mei 27, mwaka huu katika Viwanja vya Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi. Itakumbwa Novemba 27, 2022, katika mkutano wa 10 wa TRUMP na TAPSEA, Rais Samia kwa kutambua umuhimu wa wanachama wa kada hizo mbili, alielekeza uandalive mkutano na kwa mara ya kwanza ufanvikie Zanzibar.

"Nataka kuwafahamisha wanachama kuwa, maandalizi ya mkutano huo yamekamilika, na Serikali za pande zote mbili, zimeshiriki kikamilifu katika maandalizi.

"Tayari usafiri na nyumba za kulala wageni hao, zimeandaliwa, hivyo tunawasihi kujitokeza kwa wingi na waajiri watakaofanikisha kupelekea wanachama wengi, watapewa tuzo za pongezi na Rais Samia," alisema Simbachawene.

Alisema lengo la mkutano huo ni kujadili majukumu mbalimbali ya kitaaluma ya wanachama wa vyama hivyo viwili, kuleta ufanisi wa kada hiyo katika Sekta ya Umma.

"Rais Dkt. Samia mwenyewe, akiwa Arusha alielekeza mkutano huo ufanyike Zanzibar, akaelekeza waajiri wawaruhusu wanachama hao kushiriki kwa wingi kujadili majukumu yao na umuhimu wa kada hiyo katika Ustawi wa watumishi" alisema Waziri​
 
Back
Top Bottom