Rais Samia: Wananchi walipe gharama halisi ya kuunganishiwa umeme

Rais Samia amesema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa gharama ya Shs. 27,000/= kwa wananchi wote wa vijijini kwa sababu gharama zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo amesema kuna sehemu watalipa Shs. 27,000/= na sehemu zingine watalipa gharama halisi.
Nikiwa nimekaa hapa nikiota moto, imenijia akilini kuwa maadui wetu wa maendeleo TZ ni watatu tu.

• Uchawa ProMax wa Viongozi na Vijana wa UVCCM
• Kipaumbele Ni kwenye Next Election na sio Next Generation
• Presence of many Clueless Citizens

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhitaji wa 3f ni kwa wenye uhitaji wa ziada fulani. Lakini basically single inatosha. Kumbuka uhitaji ni nia na uwezo. Angalia unafiti wapi single au 3f.

Unatoa offa ya single fes, bac toa na offa ya 3fesi, co kwamba kila mhitaji wa 3fesi ni tajili, laa hasha.
 
Unatoa offa ya single fes, bac toa na offa ya 3fesi, co kwamba kila mhitaji wa 3fesi ni tajili, laa hasha.
Kuna benefit inapatikana na 3f kama ni hivyo tuzame mfukoni. Offer zinatakiwa kwenye vitu vya lazima. Ndiyo sababu vijijini wamepewa 27. Angalia watu wengi katika makazi wanaotaka 3f tiles zao wanazoweka ni za gharama kubwa. Laki 9 katika commercial siyo kitu.
 
Hivi hizo luku, nguzo n.k. ni mali ya Tanesco au ya mtu anayeunganishwa?

Na hizi gharama kila nikinunua Luku ninazokatwa kwa ajili ya hii miundombinu bado itaendelea kukatwa?

Huyu Mama anashindwa kuelewa kuunganisha wengi gharama itarudi baadae kwa watu kulipia gharama za matumizi...., Mambo yanakuwa mengi mpaka tunaanza kuharibu....
Mtanyooka
 
Kama gharama za umeme zitapanda basi hakuna haja ya kuwa na tozo za REA kwenye kununua umeme na Petrol & Deisel... Maana hatuwezi kuchangaia REA huku kijijini wanaunganishwa kwa 320,000
Kwanza wangepunguza tu hizo kodi maana kwa taarifa zao karibia vijiji vyote wameweka umeme.

Kihalisia makato wangeyapunguza hata kwa nusu,maana lengo limeshafikiwa.

Ibakie kuongeza usambazaji mdogo mdogo tu.
 
Rais Samia amesema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa gharama ya Shs. 27,000/= kwa wananchi wote wa vijijini kwa sababu gharama zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo amesema kuna sehemu watalipa Shs. 27,000/= na sehemu zingine watalipa gharama halisi.
Mimi naona mama yuko sahihi kwa hili swala la umeme. tufike mahali tuache sera za kijaamaa ambazo hazina maana. Wananchi wahimizwe kufanyakazi ili waweze kulipia huduma. baadala ya kuwapa ruzuku kila wakati. Swala a ruzuku lifanyiwe tadthmini na wapewe wananchi wale ambao uwezo wao ni mdogo. Mrfano, mtu amejenga nyumba ya milioni 50 anshindwaje kuunganisha umeme kwa laki 3?

hata swala la rusuku kwa unit kwa watu wa vijijini kulipa sh 100 kwa unit na wa mjini kulipa sh 300 kwa unit ni la kinyonyaji na kibaguzi liondolewe kila mtu alipe kwa usawa. kuna watu wanaishi vijijini lakini wanauwezo mkubwa kiuchumi kuliko waliopo mjini. Mini naishi kenya huku hakuna ruzuku ya kuunganishiwa umeme wala ya unit kila mtu analipa sawa na mwingine, lakini umeme umsambaa sehemu kubwa zaidi kuliko huko kwetu na umeme haukatiki hovyohovyo. tuachane na sera za kijamaa zilizopitwa na wakati.
 
Kwamba wewe ndo unajua kuniliko Mimi? Wewe bado unaishi kwa wazazi wako utakuwa Nini wewe?
Acha kukurupa mkuu kama hujui kitu kaa kimya, kwenye ushabiki ya mpira ndio hata ukibisha sana, hakuna atakaye kuona wa ajabu lakini sio kwenye mambo ya facts.Haya katika muongozo huo mpya wa gharama za kuunganishiwa umeme wapi kuna kundi la wateja walioko mita 300 (nguzo 10)kutoka kwenye miuondo mbinu ya tanesco?etiii hata mtu ana taka nguzo 10, naye alipe 27, 000?hapa sio fb.
Muungwana kama hajui kitu anapoelekezwa anakubali na anakuwa amejifunza kitu.
Mwisho wa mteja kuomba nguzo ni nguzo 3 tu umbali wa mita 120, zaidi ya hapo huo ni mradi tanesco ndio watajenga endapo kuna sababu ya kiuchumi ya kufanya hivyo,
 
Mtanyooka
Wewe na ndugu zako sio watanzania ?

Au unadhani umeme usio wa uhakika au gharama rafiki haukuathiri in one way or the other hata kama wewe unatumia solar ? Nishati inatumika kwenye shughuli za kila siku na impact ya nishati isiyo rafiki (gharama na uhakika) inamuathiri kila mtumiaji na mzalishaji
 
Ni sahihi kabisa, hii itaondoka sintofahamu iliyokuwepo, haiwezekani mtu ambaye anahitaji nguzo 10 eti aunganishwe kwa gharama ya sh 27,000/= hakuna uhalisia kabisa.

#Kazi iendelee
Acha kudickride ujinga kwani yeye sio mtanzania sio mtanzania akiumwa magonjwa kumi hatibiwi anatakiwa atibiwe moja
 
Kiuhalisia gharama za kuunganisha umeme ni kubwa sana. Mimi ilivotangazwa kuwa imepunguzwa mpaka 27K nilishangaa sana nikasema kimoyo moyo kwamba serikali/TANESCO haitaweza kubeba the rest of the cost, very soon itachemsha!! Mafuta ya gari tu kufika site ni zaidi ya 27k, so vifaa vyote ni bure na hapo bado kuwalipa vibarua.

Pili, TANESCO yenyewe bado haijiendeshi kibiashara. Bei ya umeme tunaouziwa watumiaji siyo halisi kulinganisha gharama halisi za uzalishaji na usambazaji wa umeme. Kwa hali hii Serikali huwa inatoa ruzuku kwa TANESCO.

So anachosema mama ndo uhalisia inavotakiwa kuwa.

Kuendelea kuwafungia watu kwa 27k eti kucreate customer base ni kujidanganya coz hao hao customers hawalipi bei halisi ya umeme.

Halafu kiuhalisia, anayeweza kujenga nyumba then akashindwa kuweka umeme wa 321k, wengi wao ndo wale wanaotumia umeme wa elfu 5 kwa mwezi mzima. This is not a significant market worth 321k exemption.

Isitoshe kikwazo cha wengi kushindwa kuweka umeme ni gharama za wiring, na siyo 321k

Wairudishe tu kama zamani. Mjini 321k halafu vijijini walau 50k
Ujinga ndio sifa yako kubwa kwani tanesco malengo yao ni nini je tanesco wanafanya biashara au wanatoa huduma?
 
Ni sahihi kabisa, hii itaondoka sintofahamu iliyokuwepo, haiwezekani mtu ambaye anahitaji nguzo 10 eti aunganishwe kwa gharama ya sh 27,000/= hakuna uhalisia kabisa.

#Kazi iendelee
Siku akihama ahame na hizo nguzo zake kumi au arudishiwe hizo gharama za nguzo kumi ?au watakaokuja baadae wasihitaji nguzo basi wamlipe yeye ?

Unajua kwamba usambazaji ni moja ya kazi ya Tanesco na hio miundombinu ni mali yao wewe unalipia tu hio service ?, Sasa unaona ni bora watu wengi wasiunganishwe au Tanesco ifanye initial investments (kuunganisha watu wote) ili ivune mazao ya Service (matumizi) ambayo otherwise huenda mtu angenunua mafuta ya taa kuwasha karabai ambayo mafuta ya taa hayo yanaagizwa na yanahitaji dollar ?
 
Kaongea ukweli kuhusu hili. Kwani nguzo bei gani kutoka kwa wazalishaji? Weka transport then fanya hesabu kuwa inawezekana vipi wewe kupata umeme wa 27
Kwani nguzo ikisimikwa ni ya nani mwananchi au tanesco .. hivi watanzania mbona mnapenda kushadadia mambo hata kama yanawaumiza ili mradi tuu muonekane mpo upande wa rais
 
Siku akihama ahame na hizo nguzo zake kumi au arudishiwe hizo gharama za nguzo kumi ?au watakaokuja baadae wasihitaji nguzo basi wamlipe yeye ?

Unajua kwamba usambazaji ni moja ya kazi ya Tanesco na hio miundombinu ni mali yao wewe unalipia tu hio service ?, Sasa unaona ni bora watu wengi wasiunganishwe au Tanesco ifanye initial investments (kuunganisha watu wote) ili ivune mazao ya Service (matumizi) ambayo otherwise huenda mtu angenunua mafuta ya taa kuwasha karabai ambayo mafuta ya taa hayo yanaagizwa na yanahitaji dollar ?
Umeongea poa sana tatizo watanzania wengi ni watu wakushadadia mambo hata kama yanawaumiza . Yani nilipie nguzo halafu nguzo iwe mali ya tanesco halafu wanasema tanesco haipati faida kwani tanesco inafanya biashara au inatohuduma ?
watanzania tumekuwa watu wakupenda umbea na kushadadia mambo hata kana yanatuumiza.. hangaya ametunyonga kwasababu huko mchamba wima umeme kwao bure
 
Wewe na ndugu zako sio watanzania ?

Au unadhani umeme usio wa uhakika au gharama rafiki haukuathiri in one way or the other hata kama wewe unatumia solar ? Nishati inatumika kwenye shughuli za kila siku na impact ya nishati isiyo rafiki (gharama na uhakika) inamuathiri kila mtumiaji na mzalishaji
RIP MAGUFULI
 
Rais Samia amesema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa gharama ya Shs. 27,000/= kwa wananchi wote wa vijijini kwa sababu gharama zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo amesema kuna sehemu watalipa Shs. 27,000/= na sehemu zingine watalipa gharama halisi.
Shangingi la pwani
 
Rais Magufuli katuachia nani huyu??
 
Back
Top Bottom