Rais Samia: Wananchi walipe gharama halisi ya kuunganishiwa umeme

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,151
3,796
Rais Samia amesema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa gharama ya Shs. 27,000/= kwa wananchi wote wa vijijini kwa sababu gharama zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo amesema kuna sehemu watalipa Shs. 27,000/= na sehemu zingine watalipa gharama halisi.
 
Hivi hizo luku, nguzo n.k. ni mali ya Tanesco au ya mtu anayeunganishwa?

Na hizi gharama kila nikinunua Luku ninazokatwa kwa ajili ya hii miundombinu bado itaendelea kukatwa?

Huyu Mama anashindwa kuelewa kuunganisha wengi gharama itarudi baadae kwa watu kulipia gharama za matumizi...., Mambo yanakuwa mengi mpaka tunaanza kuharibu....
 
Rais Samia amesema tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa gharama ya Shs. 27,000/= kwa wananchi wote wa vijijini kwa sababu gharama zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo amesema kuna sehemu watalipa Shs. 27,000/= na sehemu zingine watalipa gharama halisi.

BBE8C20A-2A14-464D-9C65-F01009210CF1.jpeg
 
Aliye mshauri hili anambomoa wala hamtakii mema. Yako mambo ambayo si haramu serikali kutoa ruzuku. Mh Rais anashindwa kuelewa vipi kumuunganishia umeme mteja kwa bei rahisi ni kutengeneza base kubwa ya wateja kwa Tanesco ambao baadaye ndio watakuwa chanzo cha pato la kampuni. Kapigwa changa la macho na wenye matamanio ya 2025. Aone na hiyo listi mpya alifanyie kazi angalau ampangue kwenye namba aliyopo kama anampenda sana

Hapa mwishoni mwa hutoba yake kwa Taifa kasema kwa ujasiri Mkuu. Hongera Amiri Jeshi Tanzania ndivyo inahitajika kuendeshwa hivyo. Huwezi pendwa ama kumfurahisha kila mtu. Ukitaka kufanya hivyo utaishia kuitwa dhaifu.

Hongera nyengine ni kukataa kuukubali msamaha geresha wa maneno ya kuazima kutoka kitubio cha Kanisani. Ile ilikuwa ni kejeli na wala si kuomba msamaha. Bravo Madam President.

Hivi kwa nini TARURA iwe TAMISEMI? Ili hali kuna Wizara ya Ujenzi? Liko tatizo pahala mulione.
 
Back
Top Bottom