Rais Samia: Vijana wahanga wakubwa wa ajali za barabarani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Akishiriki Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa Jijini Arusha, amesema takwimu zinaonesha zaidi ya 90% Ajali za Barabarani husababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwemo mwendokasi, kutovaa mikanda na kupita gari lingine bila tahadhari.

Amesema, "Uendeshaji wa Vyombo chakavu au vibovu huchangia 3.2% ya ajali na hali mbaya/ubovu wa barabara, hali ya hewa (vumbi, ukungu, utelezi au moshi) huchangia 1.3%"

Ameongeza kuwa, waendesha bodaboda bado ni miongoni mwa kundi kubwa linalosababisha ajali.
 
Vyanzo vya ajali za barabarani

1. Matendo yasiyo salama/makosa ya kibinadamu (88%) - kutofuata sheria za usalama barabarani, kutojua sheria za usalama barabarani, ulevi, mwendokasi, ku-overtake kwa kupita kushoto badala ya kulia, ku-overtake kwenye round-about, uendeshaji wa vyombo (vya moto) vibovu, mizaha barabarani...

2. Mazingira yasiyo salama (10%) - Vyombo vibovu au chakavu, barabara mbovu, utelezi, giza, mwanga mwingi, ukungu ...

3. Ajali zisizohepukika/Acts of God (2%) - Majanga ya asili.
 
Back
Top Bottom