Nimeshtushwa na habari kuwa wanawake kwenye kongamano lao lililokutana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, wamekuchangia sh 120,000,000 kwa ajili ya form ya Urais 2025.
Pamoja na kuwa form hiyo ina gharimu sh milioni 1 tu. Mama tunaujua fika kuwa Una uwezo wa kujilipia gharama ya form hiyo yaani sh milioni moja tu.
Wanawake hao wangekuchangia kiasi halisi sh milioni moja tu na zinazozidi waelekeze ziende ziwasaidie wanawake na wasichana Watanzania wenye uhitaji mkubwa zaidi lakini siyo wewe Rais Samia.
Mfano kwenye Radio Free Africa tarehe 10 March 2024 asubuhi, walirusha habari ya mama mmoja amelazwa hospitali ya Seketoure huko Mwanza yuko hoi.
Mama huyo hana pesa ya matibabu, hana chakula na hana hata mtu wa kumuudumia.
Mama huyo anaudumiwa na mtoto wake wa kiume wa miaka 10 kwa kila kitu hata kumuosha akijisaidia maana hajiwezi kabisa.
Kongamano hilo la wanawake lingemsaidia mama mwenzao kama huyo ambaye anakosa matibabu, chakula na huduma ya kujisitili.
Rais wangu Kataa pesa hizo ziende kwa wanawake wenzenu na wasichana wanaokosa ada vyuoni.