Rais Samia ungemteua Jerry Muro kuwa Mwenezi wa CCM Taifa ungekuwa Umeupiga Mwingi zaidi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,032
Ana kila Kitu tena huyu ni zaidi hata ya alivyokuwa Nape Nnauye na alivyo huyu Uliyemteua sasa Dada Sofia Mjema ambaye kwa Uzito wa hiyo nafasi sioni kama ana amsha amsha na Ubavu wa Kutema Cheche.

Mtu mwingine ambaye nafasi hii ingemfaa sema tu kwa sasa ni Mbunge ni Livingston Lusinde Mtoto wa Kawe Ukwamani kwani nae ana Vitu vingi vya Kiushawishi na hata Kimvuto katika Kumsikiliza.

Rais Samia na Mwenyekiti CCM Taifa bado hujachelewa Kumtengua Dada Bi. Sofia Mjema na kumpa hiyo Nafasi ya Uenezi Taifa Mtani wangu wa Yanga SC, Mdau wangu katika Tasnia na Mtoto wa Mwalimu ( Mama ) Muro wa Ubungo Maji Jerry Muro.
 
Back
Top Bottom