Standards Person
JF-Expert Member
- Apr 22, 2021
- 673
- 859
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amekua akizunguka maeneo mbalimbali akisisitiza ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha hizo, amewataka viongozi waliopo chini ya wizara yake kuzingatia taratibu zote katika utumishi wa umma. Mbaya zaidi alipokua ziarani Tanga alimtolea mfano Martin Shigela ambaye alikua RC Tanga. Akamsifia eti hagombani na wasaidizi wake.
Mh. Rais ninakupa taarifa kwamba Tanga kuna migogoro ya ardhi iliyosababishwa na Shigela, Mkurugenzi na watu wa ardhi. TAKUKURU wanajua na Ummy anajua.
Mh. Rais baadhi ya watu waliokua wanaidai halmashauri na mkurugenzi Daudi Mayeji kukataa kulipa na kupeleka malalamiko yao TAKUKURU,wameishia kuwekwa rumande. Wengine kudhalilishwa, Ummy anazo taarifa
Tanga kuna ukandamizwaji mkubwa unaofanywa dhidi ya watumishi kunyanyaswa, kudhalilishwa, kukataliwa kazini. Aliyekua RAS anajua lakini hakushuhulikia kwani akielezwa mapungufu ya mkurugenzi hachukui hatua wala hamuulizi na kama amemuuliza hakuna mrejesho. Ummy anajua
Mh. Rais Tanga Jiji baadhi ya watu wameacha kazi kutokana na manyanyaso, ukandamizwaji, udhalilishwaji na majaribio mengine ya kutaka kudhuriwa usalama wa maisha yao. Ummy anajua
Mh. Rais rushwa Tanga chini ya mkurugenzi huyu imetamalaki wala sio jambo la siri. Ummy ameamua kuwasimamisha kazi wakurugenzi wengine huyu wa Tanga amemuacha, kwanini? Kuna nini hapo? Ummy anafanya wana Tanga na Watanzania hawaoni? Kama anajua wanaona basi amewadharau kwamba hawana akili.
Mh. Rais huyo Daudi Mayeji anakikundi chake cha watumishi ambacho kazi yake ni kutishia, kuchafua na kuhonga watu ili tu wakubaliane na matakwa yake. Watu hao wamejivisha vazi la ukada. Ushahidi upo na Ummy anajua
Mh. Rais ingilia kati suala la utawala usiobora na kupotezewa muelekeo kimaisha kwa watumimishi waliokua tofauti na mkurugenzi kwa sababu za kuendesha ofisi anavyotaka kama vile rushwa. Waliokua waadilifu wamenyanyasika. Ukifuatilia utajua mengine mazito mno
Mh. Rais baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na ubabe wa viongozi. Viwanja vyao vimechukuliwa wakauziwa wenye fedha. Mtu ameingiza maji kwenye kiwanja lakini anakuja kiwanja kauziwa mtu mwingine. DC Mwilapo anajua na aliunda kamati lakini hakuna jipya. Ummy anajua na leo anawasifia.
Mh. Rais pasipo shaka yoyote ninaamini unayo hofu kuu ya Mungu ndani yako. Wasaidie watu wa Tanga. Unda tume huru ya kuchunguza madhila wanayopitia watu wa Tanga. Usimtegemee Ummy kutatua changamoto za watu wa Tanga tena hasa zilizosababishwa na hawa viongozi waliopo Tanga,Ummy hana ubavu hata kidogo.
Mh. Rais ninakuombea afya njema na ninasema KAZI IENDELEE