Rais Samia, unda tume huru ya kuchunguza madhila wanayopitia wananchi wa Tanga

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
855
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amekua akizunguka maeneo mbalimbali akisisitiza ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha hizo, amewataka viongozi waliopo chini ya wizara yake kuzingatia taratibu zote katika utumishi wa umma. Mbaya zaidi alipokua ziarani Tanga alimtolea mfano Martin Shigela ambaye alikua RC Tanga. Akamsifia eti hagombani na wasaidizi wake.

Mh. Rais ninakupa taarifa kwamba Tanga kuna migogoro ya ardhi iliyosababishwa na Shigela, Mkurugenzi na watu wa ardhi. TAKUKURU wanajua na Ummy anajua.

Mh. Rais baadhi ya watu waliokua wanaidai halmashauri na mkurugenzi Daudi Mayeji kukataa kulipa na kupeleka malalamiko yao TAKUKURU,wameishia kuwekwa rumande. Wengine kudhalilishwa, Ummy anazo taarifa

Tanga kuna ukandamizwaji mkubwa unaofanywa dhidi ya watumishi kunyanyaswa, kudhalilishwa, kukataliwa kazini. Aliyekua RAS anajua lakini hakushuhulikia kwani akielezwa mapungufu ya mkurugenzi hachukui hatua wala hamuulizi na kama amemuuliza hakuna mrejesho. Ummy anajua

Mh. Rais Tanga Jiji baadhi ya watu wameacha kazi kutokana na manyanyaso, ukandamizwaji, udhalilishwaji na majaribio mengine ya kutaka kudhuriwa usalama wa maisha yao. Ummy anajua

Mh. Rais rushwa Tanga chini ya mkurugenzi huyu imetamalaki wala sio jambo la siri. Ummy ameamua kuwasimamisha kazi wakurugenzi wengine huyu wa Tanga amemuacha, kwanini? Kuna nini hapo? Ummy anafanya wana Tanga na Watanzania hawaoni? Kama anajua wanaona basi amewadharau kwamba hawana akili.

Mh. Rais huyo Daudi Mayeji anakikundi chake cha watumishi ambacho kazi yake ni kutishia, kuchafua na kuhonga watu ili tu wakubaliane na matakwa yake. Watu hao wamejivisha vazi la ukada. Ushahidi upo na Ummy anajua

Mh. Rais ingilia kati suala la utawala usiobora na kupotezewa muelekeo kimaisha kwa watumimishi waliokua tofauti na mkurugenzi kwa sababu za kuendesha ofisi anavyotaka kama vile rushwa. Waliokua waadilifu wamenyanyasika. Ukifuatilia utajua mengine mazito mno

Mh. Rais baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na ubabe wa viongozi. Viwanja vyao vimechukuliwa wakauziwa wenye fedha. Mtu ameingiza maji kwenye kiwanja lakini anakuja kiwanja kauziwa mtu mwingine. DC Mwilapo anajua na aliunda kamati lakini hakuna jipya. Ummy anajua na leo anawasifia.

Mh. Rais pasipo shaka yoyote ninaamini unayo hofu kuu ya Mungu ndani yako. Wasaidie watu wa Tanga. Unda tume huru ya kuchunguza madhila wanayopitia watu wa Tanga. Usimtegemee Ummy kutatua changamoto za watu wa Tanga tena hasa zilizosababishwa na hawa viongozi waliopo Tanga,Ummy hana ubavu hata kidogo.

Mh. Rais ninakuombea afya njema na ninasema KAZI IENDELEE
 
Ummy anaendelea kuleta siasa hajajua bado kwamba huu niwakati wa kuendelea na kazi.
Kwakua serikali ni sikivu na inaomkono mrefu Amiri Jeshi Mkuu lazima amzingue mkurugenzi Hugo
Rushwa na ubabe kwa mkurugenzi na baadhi ya wakuu wa idara vipo wazi.
Vitisho vya kila aina na mashambulio ya aina mbalimbali vipo wazi
Ummy bado amelalatu,akijaamka tonge linamdondoka mdomoni
 
Ona sasa Shigela ameingia Moro na kishindo. Kujikalia kwake kama mtazamaji sasa mh. Rais amechukua maamuzi.
Hata Shigela hana muda atajitengua kama alivyojitengua Chalamila
 
Mkurugenzi huyo anakikundi au genge lake la watu wanaotishia usalama wa watu na kujaribu kuua kama Sabaya anavyotuhumiwa.
Mkurugenzi anatumia fedha za umma kuficha maovu yake. Watu wapo tayari kama serikali ikisikia kilio hiki, watanzania watashangaa namna ambavyo ofisi hiyo imetumika vibaya

Sio RAS,RC,DC wote hawakua na kauli kwa mkurugenzi huyo
TAKUKURU baadhi ya watumishi ndio wamekua watu wake wa karibu akiwemo aliyekua mkuu wa TAKUKURU mkoa ambaye alisimamishwa kwa tuhuma za rushwa
Mkurugenzi wa Tanga Jiji,TAKUKURU na rushwa ni kama mbuzi na kamba yake
 
Huyo DED ni ndugu yake na mwendazake hivyo hakuna namna tulieni
Hakuna kutulia, Ummy anamlea huyu na ninauhakika ataondoka nae maana anaendelea kushuhulikia wakurugenzi wengine na anaacha uozo kwake. Naomba mtunze kumbukumbu

Mpaka kieleweke. Hakuna kupoa
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amekua akizunguka maeneo mbalimbali akisisitiza ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha hizo, amewataka viongozi waliopo chini ya wizara yake kuzingatia taratibu zote katika utumishi wa umma. Mbaya zaidi alipokua ziarani Tanga alimtolea mfano Martin Shigela ambaye alikua RC Tanga. Akamsifia eti hagombani na wasaidizi wake.

Mh. Rais ninakupa taarifa kwamba Tanga kuna migogoro ya ardhi iliyosababishwa na Shigela, Mkurugenzi na watu wa ardhi. TAKUKURU wanajua na Ummy anajua.

Mh. Rais baadhi ya watu waliokua wanaidai halmashauri na mkurugenzi Daudi Mayeji kukataa kulipa na kupeleka malalamiko yao TAKUKURU,wameishia kuwekwa rumande. Wengine kudhalilishwa, Ummy anazo taarifa

Tanga kuna ukandamizwaji mkubwa unaofanywa dhidi ya watumishi kunyanyaswa, kudhalilishwa, kukataliwa kazini. Aliyekua RAS anajua lakini hakushuhulikia kwani akielezwa mapungufu ya mkurugenzi hachukui hatua wala hamuulizi na kama amemuuliza hakuna mrejesho. Ummy anajua

Mh. Rais Tanga Jiji baadhi ya watu wameacha kazi kutokana na manyanyaso, ukandamizwaji, udhalilishwaji na majaribio mengine ya kutaka kudhuriwa usalama wa maisha yao. Ummy anajua

Mh. Rais rushwa Tanga chini ya mkurugenzi huyu imetamalaki wala sio jambo la siri. Ummy ameamua kuwasimamisha kazi wakurugenzi wengine huyu wa Tanga amemuacha, kwanini? Kuna nini hapo? Ummy anafanya wana Tanga na Watanzania hawaoni? Kama anajua wanaona basi amewadharau kwamba hawana akili.

Mh. Rais huyo Daudi Mayeji anakikundi chake cha watumishi ambacho kazi yake ni kutishia, kuchafua na kuhonga watu ili tu wakubaliane na matakwa yake. Watu hao wamejivisha vazi la ukada. Ushahidi upo na Ummy anajua

Mh. Rais ingilia kati suala la utawala usiobora na kupotezewa muelekeo kimaisha kwa watumimishi waliokua tofauti na mkurugenzi kwa sababu za kuendesha ofisi anavyotaka kama vile rushwa. Waliokua waadilifu wamenyanyasika. Ukifuatilia utajua mengine mazito mno

Mh. Rais baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na ubabe wa viongozi. Viwanja vyao vimechukuliwa wakauziwa wenye fedha. Mtu ameingiza maji kwenye kiwanja lakini anakuja kiwanja kauziwa mtu mwingine. DC Mwilapo anajua na aliunda kamati lakini hakuna jipya. Ummy anajua na leo anawasifia.

Mh. Rais pasipo shaka yoyote ninaamini unayo hofu kuu ya Mungu ndani yako. Wasaidie watu wa Tanga. Unda tume huru ya kuchunguza madhila wanayopitia watu wa Tanga. Usimtegemee Ummy kutatua changamoto za watu wa Tanga tena hasa zilizosababishwa na hawa viongozi waliopo Tanga,Ummy hana ubavu hata kidogo.

Mh. Rais ninakuombea afya njema na ninasema KAZI IENDELEE
Kama umbea hivi!!!
 
That is true, angalia Makonda na Mnyeti
Hadi TAKUKURU Tanga ameiweka mfukoni maana ukimlalamikia mkurugenzi huyoTAKUKURU wanakuita kisha wanakuweka rumande.
Tanga chini ya mkurugenzi huyo na TAKUKURU iliyopo watu wanapitia mazingira magumu sana
 
kwanza tanga ni mkoa mmoja wa hovyo kabisa na unanuka rushwa hadi kero,akiletwa kiongozi muwajibikaji ataundiwa zengwe mpaka aondolewe ikishindikana kwa fitina za kawaida basi kwa uchawi lazima uondoke tu.

Fedha za maendeleo ya miradi wanakula viongozi huku wananchi wakizidi kuchangishwa michango na kulazimishwa kitu wanaita wenyewe msalagambo wakati kuna kodi za wananchi zinaliwa hovyo na ruzuku pia zinatolewa mfano kama ni kujenga shule n.k.Na hilo hasa liko wilaya ya muheza ambayo imeachwa nyuma kimaendeleo misalagambo ni tatizo ukizingatia wananchi wenyewe elimu yao ndo hiyo la saba D basi walishalizika na hali hiyo wao wanaona freshi.

Tena saivi kuna mchango wa elf 20 kila duka,nyumba,kibanda eti kuchangia ukarabati wa bonde sekondary kwa mnaoifahamu mi naomba kuelimishwa kodi zetu wananchi zinafanya kazi gani ikiwa hii michango inarejea kwa kasi ya 5G.Misalagambo ni ya nini ikiwa mradi kama ni wa kujenga vyumba kadhaa vya madarasa anapewa mkandarasi kwa zabuni maalumu kutoka halmashauri au na shule husika kutokana na ruzuku inazopokea kutoka serikalini.

Kiukweli Mh.rais aliangazie hilo tatzo sababu wananchi hatuna sehemu nyingine ya kulalamika ukizingatia halmashauri yote,vyombo vya dola na mahakama walishatekwa na aina ya mfumo uliopo.
 
Rc, Dc, Takukuru na Ummy wote wanafyata kwa DeD basi huyu si wakawaida.
Kuna halufu ya uongo kwa mbaaaali na Ukweli kwa ukaribu
 
Huo ndio ukweli na tunaomba mamlaka zitupe ground ya kuelezea ugumu watu waliopitia.
Kuna genge la wahalifu linatekeleza matakwa ya mkurugenzi.
Ukienda TAKUKURU kesho yake mkurugenzi anakuambia ulichosema huko na TAKUKURU wakisha yajenga na mkurugenzi unawekwa mahabusu kwanza.
 
Back
Top Bottom