Rais Samia Unaibiwa Mama, Hamasa Haziwezi Kuibeba timu Mbovu

5 Nyingi

JF-Expert Member
Nov 15, 2023
247
594
Wakati nchi ya Ghana imeamua kuwekeza katika soka, serikali yao iliweka mazingira vutivu kwa wawekezaji wanaotaka kufungua academy, academy zikafunguliwa nyingi kama Makanisa ya jiji la Mbeya.

Miaka 10 baadaye timu ya taifa ya Ghana ikaanza kuimarishwa na vijana waliotokea kwenye academy zao, timu za ulaya zikaanza kununua wachezaji toka Ghana, academy zao zikawatafutia scholarship wachezaji wenye vipaji vikubwa ili wakapate ujuzi zaidi kwenye nchi za dunia yakwanza.

Mpaka sasa Ghana inashiriki kwenye mashindano mbalimbali na wanatumia madogo tu sio vikongwe.

Maajabu Tanzania inataka kuvuna isicho kipanda kwa kutumia hamasa. Huu ni wizi na uhujumu uchumi, najua timu ya Taifa haitavuka makundi abadani.

Wachezaji waambiwe kabisa wasipovuka makundi watazitapika fedha zote zilizo unguzwa ili iwe fundisho.

Rais Samia bibi yangu mpendwa tafadhali kaa mbali na wahuni na matapeli, mtafute Mh Polepole mzee wa Cuba akuelekeze jinsi ya kuwajua wahuni na matapeli kwa mbinu za Cuba.
 
Badala ya kununua magoli angedhamini mashindano kama yale ya Rolingstone yaliyokua yakifanyika Arusha kila mwaka kwa timu toka nchi za jumuia ya afrika mashariki kwa watoto wadogo.

Mashindano ambayo yaliibua watu kama kina Erasto Nyoni.
 
Hii ni point ya msingi, tatizo washauri wa mama ni akina Nape Nnauye na Ashatu Kijaji
 
Wakati nchi ya Ghana imeamua kuwekeza katika soka, serikali yao iliweka mazingira vutivu kwa wawekezaji wanaotaka kufungua academy, academy zikafunguliwa nyingi kama Makanisa ya jiji la Mbeya.

Miaka 10 baadaye timu ya taifa ya Ghana ikaanza kuimarishwa na vijana waliotokea kwenye academy zao, timu za ulaya zikaanza kununua wachezaji toka Ghana, academy zao zikawatafutia scholarship wachezaji wenye vipaji vikubwa ili wakapate ujuzi zaidi kwenye nchi za dunia yakwanza.

Mpaka sasa Ghana inashiriki kwenye mashindano mbalimbali na wanatumia madogo tu sio vikongwe.

Maajabu Tanzania inataka kuvuna isicho kipanda kwa kutumia hamasa. Huu ni wizi na uhujumu uchumi, najua timu ya Taifa haitavuka makundi abadani.

Wachezaji waambiwe kabisa wasipovuka makundi watazitapika fedha zote zilizo unguzwa ili iwe fundisho.

Rais Samia bibi yangu mpendwa tafadhali kaa mbali na wahuni na matapeli, mtafute Mh Polepole mzee wa Cuba akuelekeze jinsi ya kuwajua wahuni na matapeli kwa mbinu za Cuba.
This is Tanzania not Ghana, Bora hamasa kuliko mikakati ya muda mrefu, yaani tuache kushiriki tusubiri mikakati Yako duu, kwa hatua tuliyoifikia Hadi kushiriki naipongeza serikali ya Tanzania
 
Mipumbavu kama wewe ndo inatia hasara hii nchi.
 
Sijui sana mpira ila tz hatutoboi
Kumbe ni ngumu kuchukua lakini hatua ya makundi tunavuka.
Kuhusu kamati ya ushindi ni sehem ya kujionesha kua Tanzani, tofauti iliyopo kati ya msomi na asie soma ni vyeti tu, ila kimazo tuko sawa.
 
Nani kasema kuchukua hapo nimesema hatutoboi hata hayo makundi hatusogei
 
Back
Top Bottom