Rais Samia: Tutaendelea kukopa tumalizie miradi inayoendelea

Ndugai ana point tatizo haaminiki hasa ikizitangatiwa ana mgombea wake 2025. ..Mama siyo mbaya kukopa tatizo anapeleka zenji halafu wadanganyika ndio wanalipa. ...way forward bunge liwe linajadili aina ya mkopo na namna ya kulipa ikiwemo masharti ndio tukope. ..ila sasa hakuna Bunge kwahiyo tuendelee na chukua chako mapema hadi siku wadanganyika wazinduke. ...
TRA kule zanzibar wanazileta bara ndio mnakula huko milo 3.,
 
Tanzania's debt cycle is weird. Being in a strategic debt is not bad, but seeing the Government and its mates getting fatter with it hapo ndo you get to know these people are really BadAss 😂😂

John Adams alipata kusema, "Two ways to conquer and enslave a country. One is by sword the other is by debt"
 
Rais yuko sahihi hapa. Kukopa ukala ni kosa, lakini kukopa ukawekeza kwenye miradi yenye uwezo wa kurudisha deni ni sawa sana.

Mfano mzuri ni reli mpya ya Nairobi hadi Mombasa. Kenya walikopa wakaijenga. Sasa direct benefits na spin off businesses zake zinachangia sana kuinua uchumi wa Kenya, na ina uwezo wa kulipa deni.

Mtu asifikirie kujenga reli ya kisasa Dar hadi Mwanza kipato chake kwa nchi ni nauli zitakazokusanywa na malipo ya kusafirisha mizigo tu. Kuna spin off businesses nyingi zitakua. Hilo litainua kiwango cha uchumi na makusanyo ya kodi za serikali. Mkopo utalipika vizuri sana na kuacha faida kubwa.

Pamoja na kwamba namshutumu sana Mama kwa kosa lake la kutokubali mchakato wa katiba mpya sasa (I posted some advice on this, right from the beginning. Nilisizitiza kwa kuandika the catch words : MAMA SEMA NENO MOJA TU NA NCHI ITAPONA), lakini yuko sahihi kwenye hili la mikopo.

Kwa mfano, kama unatafiti mapato na matumizi ya kuwa na basi la kusafirisha abiria kati ya Dar na Dodoma, na ukagundua kwamba gharama za kununua basi la kufanya kazi hiyo zinaweza kurudishwa baada ya miaka 3 na kisha ukaogopa mkopo wa kufanya huo uwekezaji basi wewe ni mbumbumbu. Inatakiwa ukae kimya uache watu wajenge nchi.
 
Mapumbavu na mashetani kabisa haya majitu. Yanatufanya sisi wananchi mazuzu.
Yanakopa hayalipi halafu yanaondoka madarakani inabidi utaratibu ufanyike kila rais akimaliza madaraka asiache deni lake.
Nchi inadaiwa tirion 70 halafu bado maskini? Huu ni upumbavu

Jiulize huu mzigo wote upo wapi mkuu!!! Daaah masikini Tanzania yangu..... hawa viongozi wanatuona wajinga sana
 
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono

======

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema zipo jitihada za kuivunja moyo Serikali kwenye Mikopo, akiongeza kuwa hakuna Nchi isiyokopa na hata Mataifa yaliyoendelea yana Mikopo mikubwa

Amesisitiza, "Tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee. Ukikopa unajenga sasa kwa haraka, ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa Matrilioni unasubiri za kwako utaumaliza lini"

Ameongeza, "Tumekopa Mkopo wa Masharti nafuu wa miaka 20, unakudhuru nini? Maendeleo yanakuja haraka, utakusanya polepole uende ukalipe"
 
Kama anakopa na speed ya ukamilishaji miradi ionekane,kwa maana miradi ikamilike kwa wakati!! Hapo hatutakuwa na nongwa!!, kwanza huko dar wanamdanganya Sana,arudi huku ikulu ya nchi iliko Dodoma,mbona anang'ng'ana na daisalama!!??, kituo Cha kazi yake Kiko Dodoma,yeye anang'ang'ania kukaa nje ya kituo chake Cha kazi, si utovu wa nidhamu ya kazi huu!!!

yeye ni mtumishi ,sawa na watumishi wengine,mbona waalimu, ma nesi n.k wanalazimishwa kubaki kwenye vituo vyao vya kazi!!?, arudi kituo chake Cha kazi,aachane na huo mji wa daisalama!! Ebo!!
 
Kama anakopa na speed ya ukamilishaji miradi ionekane,kwa maana miradi ikamilike kwa wakati!! Hapo hatutakuwa na nongwa!!, kwanza huko dar wanamdanganya Sana,arudi huku ikulu ya nchi iliko Dodoma,mbona anang'ng'ana na daisalama!!??, kituo Cha kazi yake Kiko Dodoma,yeye anang'ang'ania kukaa nje ya kituo chake Cha kazi, si utovu wa nidhamu ya kazi huu!!!

yeye ni mtumishi ,sawa na watumishi wengine,mbona waalimu, ma nesi n.k wanalazimishwa kubaki kwenye vituo vyao vya kazi!!?, arudi kituo chake Cha kazi,aachane na huo mji wa daisalama!! Ebo!!
Taarifa ni kuwa Dodoma bado haijakamilika ujenzi.
 
Back
Top Bottom