NSSF fao baada ya ajira kuisha

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,339
5,574
Nilifanya kazi, nikawa nimefikisha miezi 192 ya kuchangia 2022 ingawa umri ulikuwa 46 years. Baada ya Mzee baba kuja na sheria za kuunganisha mifuko nikaogopa hivyo nikawithdraw FAO la kukosa ajira na fedha nikapata ila nikawa nasubiri umri wa 55 ufike ili nilipwe na pension.

Bahati nzuri baada ya kuwa nimetoa mafao nilipata kazi na nimefanya kwa mashirika mawili tofuati na kufanikiwa kuchangia miezi 36 kwa miaka 3 na ajira imeisha.

Sasa najiluiza utaratibu mpya wa kupata hizi nilizochangia baada ya kuwa nimetoa michango yangu huko nyuma ni upi?

Asanteni
 
Mzee ungeuliza kwanza kabla ya kufanya maamuzi, juzi kati nilikuwa nasoma soma taarifa ya hii mifuko miwili hasa huu wa NSSF nikaona kuwa kuna Pensheni iliyohairishwa yaani endapo mwanachama atakuwa ametimiza Credit 180 hata kama atakuwa na umri wa miaka 40 kwa mfano anaweza kuomba pensheni hiyo iliyo hairishwa, yaani atachukua Mkupuo wake 33% baadaye akifika umri wa miaka 55 kustaafu kwa hiari au miaka 60 kustaafu kwa lazima ndipo ataanza kupata Pensheni, hivyo unaweza omba mkuu, ndicho nacho jua
 
Hivi ukifanya kazi mkataba ukaisha NSSF wanakulipa? Wenye kujua waeleweshe
Jamaa wanasema kwa mujibu wa sheria inasema mafao ya kupoteza ajira yanatolewa kwa mwanachama aliyeachishwa kwa sababu yoyote isipokuwa kuacha yeye mwenyewe, jitazame kama upo kundi gani
 
Hapo unalipwa vizuri tu ili mradi uwe umefikisha miaka 55!
Mtu analipwa pension kama amechangia miezi 180 au miaka 15!
 
Hapo unalipwa vizuri tu ili mradi uwe umefikisha miaka 55!
Mtu analipwa pension kama amechangia miezi 180 au miaka 15!
What if umechangia miezi 170 na umeamua kustaafu miaka 55, je utalipwa pesa zako za michango zote? Kumbuka huqualify kwa pension
 
Back
Top Bottom