Rais Samia tukumbuke watumishi wa NIDA

Sawa ila mkirudi kazini muache dharau wafanyakazi wa NIDA wakat wa vitambulisho mi naenda kupiga picha mtu ananiuliza jina nani huku yeye anachat na kunywa juice akimaliza ndo ananiuliza ulisema unaitwa nani? Yaan nilijieleza had nikachoka
Isije ikawa huyo mtu ndio huyu mleta mada
 
Nilijisajili 2014 ili kupata kitambulisho, kwa ile jeuri na dharau mliyonionyesha siku ile sitawasahau.
Mlifikiri sijui sijasoma, hivi huwa mnawaza kila anayekuja kwenu kujiandikisha hajasoma?
Kumbe mlifukuzwa eeh? Safi Sana na mfukuzwe tena huko mlipo
Ila siku nyingine punguzeni dharau na jeuri
 
Comment ya mtu mmoja mwanzoni inaweza badilisha mwelekeo mzima wa wanaofuata.Wananchi wana stress sana...
Pole mtoa mada..
Japo ni kweli taasisi nyingi za serikali customer care ni kama hakuna

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Ila mlikuwa na nyodo Sana...kuna vijamaa pale Chang'ombe kalinijibu shit mwaka 2014, kisa nadai kitambulisho changu! Kulikuwa na namba za mabosi zao nikawapigia. Wakanipa haraka siku hiyo hiyo.


Poleni sana
Hapohapo kama ulikuwepo, chang'ombe walikua wakijiona wao miungu kabisa. Kwenye kupanga foleni walikua wanafoka hao sijawahi kuona, alafu wanafokea wengine ni watu wazima sana sawa na baba na mama zao.
 
Mnataka kurudi wapi wakati ni kama vile hakuna NIDA kabisa. Hakuna idara ya serikali mbovu kama hii. Bora mngefukizwa wote tu

Kazi kufokea watu, elimu ya uraia hamjui. Sheria za uraia hamjui. Yani ni pumbavu juu ya upumbavu.

Mama ungefukuza tu wote hawa!
 
Comment ya mtu mmoja mwanzoni inaweza badilisha mwelekeo mzima wa wanaofuata.Wananchi wana stress sana...
Pole mtoa mada..
Japo ni kweli taasisi nyingi za serikali customer care ni kama hakuna

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Katika taasisi zote za serikali NIDA ndio kulikua na watu jeuri sijapata kuona.
Wewe huoni mbosso alitunga wimbo akasema ".....ndio kwanza najidaiiiii, Kama afisa wa Nida..."
Hao jamaa wa Nida walikua wanajidai na lugha kali sana, na wafukuzwe tena huko walipo.
 
Hahahaaaaa huyu jamaa anajuta kuleta huu uzi siku kama ya leo, siku nzuri ijumaaa had jumapili watu wakiwa wametulia Wanapata moto baridi
 
Kweli na unategemea mheshimiwa Rais wa jamuhuri apitie hapa kwenye comment kama hii?

Ukweli ni kwamba watumishi wengi huwa mmeweka dharau kwa wananchi na hata kuwasikiliza ni kama mnalazimishwa.


Mimi nasukuru nilipata kitambulisho mwaka 2014 hapa nawaza miaka miwili iliyobaki nitakuwa sina kitambulisho kwa mujibu wa utaratibu wenu utaifa eti ni miaka kumi una expire, sasa itabidi niende somalia nikachukue kitambulisho cha kudumu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom