Rais Samia tukumbuke watumishi wa NIDA

Salamu za wazi kwako mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Kazi iendelee!

Ninakuomba mama utukumbuke watumishi 598 tuliopunguzwa kazi mara tu baada ya Rais Magufuli kuingia na kumtumbua mkurugenzi wetu Dickson Mwaimu na kuteuliwa Bw Modestus Kapilimba kisha kutupunguza wafanyakazi 598 wa NIDA nchi nzima kwa kisingizio cha mrundikano wa wafanyakazi na kuacha uhaba mkubwa wa watumishi wa NIDA na ndio mana utoaji wa vitambulisho vya taifa umekuwa tatizo kubwa sana.

Mama watumishi wengi waliopunguzwa walishajitolea kwa zaidi ya miaka mitano wakiahidiwa na wakitegemea ajira za kudumu lakini haikuwa hivyo baada ya utawala wa awamu ya tano.

Kwa sasa wengi wetu tunaishi maisha magumu sana kwani ajira ni ngumu sana kupata na wengi wetu tuna familia zinatutegemea na pia watanzania wanateseka hawapati vitambulisho kwani NIDA inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi.

Tunaomba utufute machozi na jasho letu Mheshimiwa Rais.

Ninatanguliza shukurani zangu kwako mama.

By
Anonymous from Dar es Salaam
Kama mlikua wengi hivyo na upatikanaji wa kitambulisho ulivyokua mgumu, endeleeni kukaa nje

Mimi mpaka leo nikifata kile kitambulisho napigwa kalenda
 
Hapohapo kama ulikuwepo, chang'ombe walikua wakijiona wao miungu kabisa. Kwenye kupanga foleni walikua wanafoka hao sijawahi kuona, alafu wanafokea wengine ni watu wazima sana sawa na baba na mama zao.
Hao waliobakizwa ndio wenye sifa hizo coz kuna wakubwa wanawalinda!
Sisi from peasant families ndio tuliopunguzwa wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu 2015 Mpaka leo nateseka na Nida,walikosea spelling moja ya jina langu.Nimelipa elfu 20 kufanya marekebisho tangu mwaka jana mwezi 8 mpaka leo hakuna marekebisho.Nikienda ofisini naambulia majibu ya dharau na kejeli.
Sina hamu na Nida
 
Tangu 2015 Mpaka leo nateseka na Nida,walikosea spelling moja ya jina langu.Nimelipa elfu 20 kufanya marekebisho tangu mwaka jana mwezi 8 mpaka leo hakuna marekebisho.Nikienda ofisini naambulia majibu ya dharau na kejeli.
Sina hamu na Nida
Tuombee turudi nitaanza kukurekebishia wewe free of charge coz hicho ndicho kitengo changu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom