Rais Samia tukumbuke watumishi wa NIDA

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
3,134
3,571
Salamu za wazi kwako mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Kazi iendelee!

Ninakuomba mama utukumbuke watumishi 598 tuliopunguzwa kazi mara tu baada ya Rais Magufuli kuingia na kumtumbua mkurugenzi wetu Dickson Mwaimu na kuteuliwa Bw Modestus Kapilimba kisha kutupunguza wafanyakazi 598 wa NIDA nchi nzima kwa kisingizio cha mrundikano wa wafanyakazi na kuacha uhaba mkubwa wa watumishi wa NIDA na ndio mana utoaji wa vitambulisho vya taifa umekuwa tatizo kubwa sana.

Mama watumishi wengi waliopunguzwa walishajitolea kwa zaidi ya miaka mitano wakiahidiwa na wakitegemea ajira za kudumu lakini haikuwa hivyo baada ya utawala wa awamu ya tano.

Kwa sasa wengi wetu tunaishi maisha magumu sana kwani ajira ni ngumu sana kupata na wengi wetu tuna familia zinatutegemea na pia watanzania wanateseka hawapati vitambulisho kwani NIDA inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi.

Tunaomba utufute machozi na jasho letu Mheshimiwa Rais.

Ninatanguliza shukurani zangu kwako mama.

By
Anonymous from Dar es Salaam
 
Hamna kitu mnafanya nyie watu, since 2017 I've no original ID, Online Copy imenisaidia vinginevyo ningekwama
NIDA na UHAMIAJI ndo watu ambao huwa siwaelewi nchi hii
Tumepunguzwa 2016 unategemea nguvu kazi ya kutoa kitambulisho chako cha 2017 itatoka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ila mkirudi kazini muache dharau wafanyakazi wa NIDA wakati wa vitambulisho mimi naenda kupiga picha mtu ananiuliza jina nani huku yeye anachat na kunywa juice akimaliza ndio ananiuliza ulisema unaitwa nani? Yaani nilijieleza hadi nikachoka
 
Tumepunguzwa 2016 unategemea nguvu kazi ya kutoa kitambulisho chako cha 2017 itatoka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nida wafukuzwe wote! Mkiwa kwenye viofisi vyenu na madharau na kuwaona wanaokuja kuhudumiwa hapo kama ma takataka flani, mara muwagombeze, mara mututukane, hamjali hata umri wa mtu kabisa, nimeshuhudia kijana wa miaka kama ishirini na tano wa nida akimtukana bibi wa watu kisa yule bibi kushindwa kufuata maelekezo ya afisa,

nawachukia sana nyie
 
Sawa ila mkirudi kazini muache dharau wafanyakazi wa NIDA wakat wa vitambulisho mi naenda kupiga picha mtu ananiuliza jina nani huku yeye anachat na kunywa juice akimaliza ndo ananiuliza ulisema unaitwa nani? Yaan nilijieleza had nikachoka
unampiga boonge la kelb ni bora uweke tu, lockup kuliko dharau za ki kuda kama hizo nakiri hata mimi sijapata hiyo National Identity card mpaka leo hii since 2017 nilivyo jiandikisha ilikuwa kinondoni mpaka sasa wamehamishia kawe hakuna nilicho ambulia zaidi ya Namba ya NIDA pekee hiyo Card nimesha waachia tu bado suala la passport sasa maana nasikia nahuko ngoma ni nzito sana
 
Nilijisajili 2014 ili kupata kitambulisho, kwa ile jeuri na dharau mliyonionyesha siku ile sitawasahau.
Mlifikiri sijui sijasoma, hivi huwa mnawaza kila anayekuja kwenu kujiandikisha hajasoma?
Kumbe mlifukuzwa eeh? Safi Sana na mfukuzwe tena huko mlipo
Ila siku nyingine punguzeni dharau na jeuri
 
Back
Top Bottom