Kwa asili Mwanawake amejaliwa kwa neema ya mwenyezi Mungu kuwa msikivu. Ni msikivu mzuri na hasa 'anaposomeshwa' na mwanaume. vinginevyo, ndoa zisingekuwepo duniani.
Tumeshuhudia siku za hivi karibuni mjadala mkali kuhusu bandari zetu zilizopo upande wa pili wa Muungano. Wabongo tumegawanyika ktk makundi kadhaa kwa mjadala huu unaohusu (kubinafsishwa/kuuzwa/ubia?) kwa bandari zote za baharini, maziwani, (na, mitoni, kama zipo) zilizopo Tanzania bara.
Mjadala huu umetufikia na hata umegusa mioyo na hisia zetu watu tuliopo mikoa, wilaya, tarafa, kata, na vijiji vya pembezoni mwa Bongoland kabisa. Inashangaza. Mitandao ni maendeleo ila imeleta mambo; utasikia mwanakijiji cha ndani kabisa uswekeni, ... Umemsikia profesa Shivji! ... Ulimsikia Jenerali! .... Mama Tibaijuka kaongea kwa hisia leo, yule mama ni moto wa kuotea mbali!... Leo nimemsikia Jaji mwanamke akimshutumu Rais, mmh, ni hatari! Umewasikia wapinzani wanavyo uchambua mkataba, hasara na faida zake? Mmh, huyu 'Mama' anataka kuiuza Nchi.
Maneno ni mengi; mengi kweli kweli. Tupo watu tunaoiunga mkono Serikali kwa kuchukuwa hatua hiyo na tuna sababu zetu nzuri; sasa kama bandari zetu zimegeuzwa kuwa 'shamba la bibi' tena na Watanzania "wazalendo' wenzetu kabisa, ndio wanaonekana kufaidi keki ya Taifa peke yao, Si tuwape waarabu labda taabu zetu za maisha zitapungua kama siyo kwisha kabisa. Wengine wanakwenda mbali kwa kusema eti, Serikali ishiishie kwenye bandari tu, ije ibinafsishe na hili 'Dubwana' Halmashauri za wilaya.
Ni jipu kama inawezekana wapewe 'waarabu'. Suala la mikopo ya vikundi vya wanawake (CRDB) kanjanja ktk Halmashauri na benki wamekwishatengeneza kamfumo kenye 'mifereji' ya kunufaika na mabilioni hayo. Walengwa hawafikiwi. Chezea wabongo weye! Mungu aiponye Nchi hii jamani.
Tupo tunaopinga kabisa kabisa hatua hiyo ya Serikali kwa hofu kwamba, ... sasa Nchi inauzwa sawasawa na alivyowahi utahadharisha umma Spika wa Bunge mstaafu hata ikamgharimu ajira yake. Kwamba, Serikali itupilie mbali Makubaliano hayo ya (awali?)
Tupo tunataka Serikali yetu sikivu iupitie IGA upya na kuuchambua tena kwa makini na kina ili kutenga mchele, mawe, pumba na kuviweka mahali pake stahili; Ili mwisho wa siku tuibuke na mkataba utakaokuwa na sifa zote za kuitwa MKATABA.
Tupo tunaojua faida na hasara za Makubaliano haya, lakini kwa sababu ya mazingira ya labda kulinda ajira zetu, au, tumefaidi, au, tutafaidi (isivyo haki - i.e. kupitia wizi na milungura) kuwepo kwa uwekezaji, tumekaa kimya boti liendelee majini.
Tupo tusiojua kabisaa juu ya kinachoendelea; akina tia mchuzi pangu pakavu.
Lakini kwa mukhtadha huo, mambo yoote yanamwangukia maskini Mama yetu huyu wa kizanzibari, ambaye alikubali kuichukuwa Nchi wakati ikiwa na changamoto lukuki za kufikwa na msiba mkubwa wa Rais, Uviko, madeni, miradi makubwa, hali mbaya ya uchumi, watanzania hawana pesa za kutosha kukidhi mahitaji yao ya kila siku, hali mbaya ya hewa, wizi na ufisadi Serikalini, na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.
Mimi sijui niwe upande gani jamani kwa maana nikisikiliza pande zote naona kama zote ziko sahihi na sawa tu; sasa si kuchanganyikiwa huku jamani? Nimechanganyikiwa!
Kwa hali yangu hii isiyofaa, Namshauri 'Mama' (lakini iwapo hakuna 'Jambo la mtu' bali ni uzalendo wa kupambana na Umaskini; watu 'vyuma vimekaza'), chonde chonde wasikilize wazee wako hawa (kwa umri) na tena inawezekana ni walimu wako pia wa Chuo Kikuu, akina Anna Tibaijuka ((Prof), Shivji (Prof); Jaji nani yule mwanamama nimesahau jina lake, akina Dr. Tibenda, akina Tundu, wakili Mwabukusi, n.k. Waalike na kuwasikiliza wanasheria na mawakili woote maarufu Nchini, wanaharakati na wanasiasa kama Dokta Slaa, Ulimwengu; woote nashauri kutoka sekta binafsi kwani wale wa Serikalini wao walikwishafanya kazi yao tumeiona.
Kwa nini wewe Mama? Rais kwa mujibu wa Katiba yetu ndiye Mbeba maono yoote ya Nchi; sasa, jahazi lisije hama na kugonga mwamba na kupasuka vipande vipande chini ya unahodha wako. Nchi na mbingu zitakulilia Mama yangu na hutokwepa adhabu ya mwenyezi Mungu, adhabu ya Jehanamu. Dunia hii pamoja na fahari yake vyote vinapita tutaviacha kwani tupo hapa duniani kwa kitambo kifupi tu. Sisi ni wapitaji na wasafiri ktk dunia.
Makao Mungu alotuandalia ni Mbinguni, jehanamu binadamu tunakwenda kwa ujinga wetu kama hivi. Mungu kwa mujibu wa Biblia ametupatia wanadamu miaka 70 ya kuishi, na tukiwa na nguvu 80, lakini miaka yoote hiyo haina furaha ya kweli bali imejaa huzuni, shida, na masumbufu kibao. Kwa hesabu hiyo ya Kimungu, piga hesabu mama umebakiza miaka mingapi duniani?
Iwapo IGA hii itatupeleka kama Nchi kwenye kufanya Makubaliano yatakayokuwa hayana afya kwa Maendeleo na ustawi wa Tanzania,. Utupie mbali! Hatuna cha kukosa kama Watanzania. Tutaendelea na Umaskini wetu, tulikwishazoea, mpaka pale kitakapokuja kizazi kitakachoona inafaa kuwekeza ktk bandari kwa namna hiyo.
Hili suala mama siyo la kisiasa hao wajasiriasiasa wanaokuzunguka akina nap, sukuma, bajaji, hamna kitu, nachelea kusema ni wachumiatumbo tu hao. Simama sasa na utembee na Watanzania mamangu. Utakaja kunikumbuka siku moja, kama si hapa duniani, itakuwa ahera.
Wasalaam!