Rais Samia: Sekta binafsi ndiyo itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara

Huwa mnachanganya, mnasema sababu ya kutafuta private waendeshe sekta mbalimbali ni sababu watanzania tumeshindwa, ni wavivu wezi wala rushwa, sasa hizo ajira wataajiriwa wapi ikiwa ni wezi na wavivu?
Nenda pale bulyanhulu au ggm ndo utaelewa tunachomanisha, pia tofautisha wasimamizi na wafanyakazi
 
Baada ya mzungu kuwaachia nchi ona sasa wanauwa mpaka waafrika wenzao
Umeme unakatika masaa 14 kwa siku Migahawa inafungwa nyaya za umeme zile za gridi ya taifa zinaibiwa way za umeme wa treni zinaibiwa South Afrika itakuwa kama Tanzania soon.
 
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Ni upungufu katika uwezo wa kuongoza serikali. Tanzania haijafikia kiwango cha kusema serikali haifanyi Biashara. Kama serikali za nchi zilizoendelea huko Norway, China, Sweden na Urusi bado zinamiliki na kusimamia baadhi ya biashara, kwa nini sisi tusiweze kama siyo kuogopa majukumu tu. Makampuni makubwa ya mafuta na gesi ya Norway, Finland na Urusi yanimilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali, viwanda vingi vikubwa vya China vinamilikiwa na serikali. Hii dhana ya serikali haiwezi kufanya biashara ndiyo iliyopelekea mashirika kuuzwa hovyo hovyo wakati wa Mkapa na yote yakafa.

Hiyo Bandari ilishaanza kunyooshwa na Kakoko, lakini safishasafisha ya watu wa JPM ikarudisha upuuzi huu. Kama serikali haifanyi biashara basi tujiandae TRC, ATCL, TANESCO na miradi mingine yote kuuzwauzwa tena.

Kama wanataka kubinasfiswa base waliweke kwenye soko la hisa, siyo kutafuta kampuni moja huko kwa mjomba na kuigawia kinyemela. Hatua moja mbele jumulisha na hatua mbili nyuma.

1686310137893.png
 
Fa
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Mbona serikali inanunua midege na yeye anaenda kukaa kwenye kiti cha rubani na kushangaa?
 
Samia ni freemason yeye pamoja na mawaziri wake maamuzi ya kuuza bandari ni amri wamepewa ili kuuwa uchumi wa Tanzania. Lakini nawapa onyo hata mfanye nini hamta shinda kwani Mungu yupo.

Na yeyote yule sellout anaye husika kuuza bandari kwa hawa freemason yatawakuta kama wale walioiba benki na kuchoma moto.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Ehee

Ova
 
Mbona Serikali ya Emirate Dubai inafanya Biashara kwani hao mliowauzia Bandari si ni Kampuni ya Serikaki DP Dubai hata Kampuni za China mlizowapa Bagamoyo ni za Serikali pia, huyu raisi wenu aisee, duh, mnakodisha Qatar Airways Serikali nzima kwenda USA Qatar Airways ni za Serikali pia, …
Muulize ATCL huwa wanasafirisha watu bure? Udart yenyewe serikali ni majority share holder je sio biashara?

Mbona hawa watu wanatuona mafala?
 
Back
Top Bottom