Rais Samia nikuombe sikiliza vilio vya wananchi wewe mwenyewe, usilishwe maneno kwamba ni harakati za pro Magufuli. Unachonganishwa

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,362
5,809
Ninadhani kuna watu wanabeba ajenda na matamanio ya wananchi na malalamiko ya wananchi kama ni harakati za wafuasi wa Magufuli.

Hali ambayo Mh.Rais na baadhi ha viongozi wenzie wanaziba masikio kwa makusudi kabisa kwa kudhani wanawakomoa hao wanao dhani ni wafuasi wa Magufuli.

Mh.Rais, manung'uniko mengi sana ni kutoka kwa wananchi ambao sio wafuasi wa magufuli kabisa bali ni hali na uhalisia wa wanacho kutana nacho huko kwenye heka heka zao za maisha

Mh. Rais nikuombe sana wasikilize wananchi wako kwa umakini sana usiwapuuze ,usiwapuuze tena nakuomba sana USIWAPUUZE, wasikilize na ushughulike na yale wanayo yalalamikia wewe mwenyewe kwa ukaribu mkubwa sana.

Wengi wa viongozi ulio wateua ni wanafiki sana kwako sio wakweli kwako hata kidogo, kila mmoja ana ajenda yake ya siri na wengine wana ajenda zao katika kundi lao, kuwa nao makini hasa wanapo tajwa tajwa kwenye kukuhujumu.

Usizibebe tuhuma hizo kama ni visa dhidi yako au dhidi ya hao wanao tajwa tajwa, bali zibebe kwa uzito na uzifanyie kazi kwa usiri mkubwa na nina hakika utabaini mambo mengi ya sirini na yanayo endelea kwa siri

Mh.Rais nikuombe sana ujue kuwa watu wako wewe ni wananchi wako na ndio wafuasi wako halali kabisa na sio viongozi wenzio ambao wengi wao wapo na mission zao za uongozi mkubwa zaidi au kujilimbikizia mali na maandilizi ya uchaguzi hapo baadae.

Wananchi ndio kundi lako unalo takiwa kuwa nalo bega kwa bega na kutafua yale wanayo ya lalamikia.

Simaanishi viongozi wenzio sio watu wako la hasha bali hao ni watumishi wenzio mnao shirikiana kuwapambania hawa wanachi hivyo ninyi nyote kwa pamoja wafuasi wenu wa haki kabisa ni wananchi na mpo hapo kwa hisani yao MSIWAPUUZE na msi yapuuze malalamiko yao hasa yenye tija.
 
Back
Top Bottom