Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,863
- 3,192
Kipekee nakushukuru kwa kuchukua hatua za dhati za kunusuru soko la kariakoo kwa kumtuma Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa. Kwa kweli amefanya kazi kubwa ya kunusuru uchumi wetu.
Pamoja na yote yaliyojadiliwa kuna kiu cha uwajibikaji. Imedhihirika baadhi ya watendaji wako wana uwezo mdogo na wengine ni wazembe na wenye zarau
Ni ombi letu na kama itakupendeza wachukulie hatua au wahamishe au wasimamishe kazi wote walioonekana ni kikwazo kwa wafanyabiashara na uchumi wetu. Na katika hili usiwaache kambare ukaondoa dagaa utakua haujafanya kitu.
Kwa macho yako umeona kiu cha wale ambao wanalalamikiwa ni kazi kwako kuwaondoa au kuendelea kuwafuga.
Nakukumbusha Mh. Jakaya alimuondoa Kalamagi, Nchimbi, Lowasa. Pia Chuma JPM aliwaondoa Kangi Lugola, Mwigulu, Simbachawene nk ili kuleta ustawi na kuonesha uwajibikaji kwa watanzania
Sasa kama hautakuwa na serikali ya uwajibikaji au hata kuhamisha watendaji na mawaziri au hata kuwaondoa basi madhara yatakayotokea ni juu yako na utawala wako.
Chukua hatua