Rais Samia nawa hii miswada iliyoko Bungeni tujenge nchi yetu!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Raisi Samia natoa ushauri tu. Wengi wetu sio wanasiasa hapa tunapenda maendeleo ya nchi yetu tu.

Tunakuomba uweke maslahi ya nchi mbele kuliko maslahi ya vigogo wa CCM na wewe binafsi.

Katiba nzuri ya kidemokrasia italeta maendeleo kwa nchi pamoja na ukweli kwamb itaongeza ushindani wa kisiasa. Lakini maendeleo hayatakuja na hii system ya sasa na demokrasia ya maneno na matakwa ya wachache. Hii hali itahatarisha usalama huko mbele. Suluhu kwa wote ni katiba nzuri bila kujali vyama.

Ukiangalia wenzetu kama South African na hata Kenya wanatuzidi kwasababu ya sheria nzuri.

1. Demokrasia inaleta uhakika wa uwekezaji zaidi hasa wa muda mrefu
2. Sheria za Ardhi zibadilishwe
3. Serikali irudishwe kwa wananchi ili kupunguza rushwa
4. Ushindani uwepo wa kisiasa kwa usawa.

Bila hivi utapata shida sana maana kwa hali ya sasa watu hawatarudi nyuma

Achana ni hii miswada ambayo haina tija

2251B923-861F-43CA-B963-D6BA0853F3CC.jpeg
 
Raisi Samia natoa ushauri tu. Wengi wetu sio wanasiasa hapa tunapenda maendeleo ya nchi yetu tu.

Tunakuomba uweke maslahi ya nchi mbele

Katiba nzuri ya kidemokrasia italeta maendeleo kwa nchi pamoja na ukweli kwamb itaongeza ushindani wa kisiasa. Suluhu kwa wote ni katiba nzuri bila kujali vyama.

Ukiangalia wenzetu kama South African na hata Kenya wanatuzidi kwasababu ya sheria nzuri.

1. Demokrasia inaleta uhakika wa uwekezaji zaidi hasa wa muda mrefu
2. Ushindani uwepo wa kisiasa kwa usawa.
Naunga mkono hoja
P
 
Kitendo tu Cha kutokutaka kufanya minimum reforms kwenye katiba ili Sheria za uchaguzi zikae fair, hiyo ni dalili kuwa ni Nia njema ya mdomoni. Wadau walioenda kutoa maoni Yao huko kwenye kamati ya bunge, walikuwa wanalazimishwa kutoa maoni kuendana na miswaada yenye Nia ovu, na sio kama watakavyo. Hakuna mswaada unaenda bungeni bila ridhaa ya rais. Nia ovu inavalishwa nguo ya wema na chawa wa mama.
 
Inahitaji ujasiri wa ujasiri kujitosa kunawa, yaani kuyageuka mafisi yakikuangalia yataka moyo
 
Mh Rais ,kwa manufaa na Maslahi makubwa ya Mama TANZANIA,sikiliza MAONI ya Wananchi,achana na hao WAFAHIDHINA wanaojali matumbo yao,
 
Hawezi kuikana miswada ambayo ndiyo itamsaidia kurudi madarakani kumalizia nngwe ya pili.
 
Back
Top Bottom