Harakati ndiyo zinaleta demokrasia kwa tulipofikia Raisi Samia

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Raisi Samia leo anasema kuna tofauti ya wana demokrasia na wana harakati. Hiyo tofauti kwa sasa ni wewe tu mnufaikaji na genge la watawala mnalo liona hilo. Ukweli ni kwamba kwa watu wa kawaidia ni kitu kimoja.

Ukisema wanaharakati ni kama vile kuna watu wana andamana bila sababu lakini si kweli sababu zipo. Muda zaiidi ya mwaka mmoja umekuwa umejifungia na kuongea na upinzani kwa sehemu tofauti lakini matokeo yake hakuna chochote kinacho inekana kwa zaidi ya mwaka zaidi ya maneno matupu. Mikutano ambayo inafanyika ilikuwepo kisheria hivyo hakuna jipya?. Serikali za mitaa unataka mkwe wako na team yake ndiyo wasimamie, hutaki katiba mpya lakini unataka ubaki na madataka wewe mwenyewe tu. Hakuna tume huru wala chaguzi huru yeyote imefanyika toka uingine madarakani pamoja na kuongea sana. Polisi kutoa kusindikiza maandamano sio sera mpya au sijui ni “R” hapana hii ndiyo sheria ya sasa. Raisi Samia wewe ndiye umepoteza imani ya demokrasia kwa watu na hautaweza kusingizia wapinzani kwenye hili. Unaongea majukwaani lakini ukienda kuangalia Miswada ambayo mnataka kupitisha haina mabadiliko ya maana.

Kama kweli unataka kuwa mwana demokrasia na kudai unapenda demokrasia na sio harakati basi kwanini tusiwe na katiba kama za wenzetu wa Kenya au South Africa? Unajivuta kwa lipi? Je mzee warioba na wenzake nao ni wana harakati? Je mwana harakati gani atakaa mwaka mmoja wa maongezi bila kuandamana halafu aandamane sasa hivi.

Kama harakati za kukaa na kuongea zimejaa uongo, ubinafsi wako wa chama chako, kujali watu wachache na kikundi cha watawala badala ya kujali nchi na vizazi vijavyo. Wewe ndiye unageuza wana demokrasia kuwa wana harakati. Imefika sehemu demokrasia haitaweza kupatikana bila harakati kwasababu nia yako kwa sasa iko wazi mabadiliko unayotaka unataka yakunufaishe wewe na genge lako na sio nchi.

Raisi Samia ukitoka wewe na familia yako kwenye uongozi utajengewa ikulu yako watoto wako wakina Abdul watakuwa matajiri wa biashara wanazofanya na wakwe zao watakuwa na ubunge. Je Mtanzania wa kawaidia utakuwa umemuachia uhuru upi, Je utakuwa umeacha katiba bora na za kusifika kama za nchi nyingine kama South Africa na Kenya? Au utakuwa umeacha genge lako likiweka famia nyingine mifano ya ufalme hapa nchini huku wananchi wakiendelea kuchaguliwa wabunge badala ya kuwapigia kura, polisi iliendelea kuiba kura badala ya kulinda watu . Ulisema utakuwa mwazi zaidi kama ni kweli kwanini mkataba wa DP
World umekuwa wa siri pamoja na kelele zote?.

Ukweli ni kwamba Raisi unaongea kuliko vitendo na bila harakati hatutaweza kupata demokrasia hivyo usije kujaribu kupotosha kwa jamii kwamba hatuna wana demokrasia eti tuna wana harakati. Sisi hapa tumekuonga mkono kwa miaka kumbe wewe si mkweli na usije kufikiri kuongea makanisani itasaidia tena.

Sisi tutakusaidia lakini lengo ni lazima liwe demokrasia ya kweli na katiba bora bila kujali vyama. Kwa katiba ya sasa zaidi ya genge lenu dogo hapo CCM mwananchi wa kawaida hanufaiki kama inavyotakiwa.
 
Back
Top Bottom