Rais Samia na Serikali yako mmejipangaje ili kukomesha watu wanaoendelea kumchafua Hayati Magufuli?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,897
12,340
Kwanz kbs napenda kumshukur mw/Mungu kwa kunijaalia uzima, akili, maarifa na afya, lkn pia napenda kutumia nafasi hii kuwasalimu member wote wa jamii forum mliopo humu.

Ndugu zangu watanzania kuna tabia imezuka kutoka katika makundi mbali mbali ya wachumia matumbo ambao wameamua kutengeneza umoja wao kwa lengo la kumchafua na kumdhihaki marehemu, ili ionekane kwamba kila alilofanya (liwe baya au zuri) halikuwa na manufaa au faida yoyote kwa watanzania.

Kila mwenye akili timamu anafahamu kwamba hayati Magufuli alifanya mambo mengi mazuri ktk nchi hii tangu alipokuwa waziri na mpaka alipokuwa raisi. Ni yeye aliefanya nchi hii ianze kujulikana kimataifa mpaka kufikia hatua nchi yetu ikaanza kulinganishwa au kushindanishwa na nchi zenye maendeleo na zinazojengwa kwa kasi kama vile Ghana, Nigeria, South Africa, Kenya nk. Lkn pia hata yeye alikuwa anashindanishwa na maraisi bora wa Africa tena ktk tatu bora.

Mambo mengi ya maendeleo ambayo yalishindikana kufanywa miaka zaidi ya 50 ya nyuma yeye aliweza kuyafanya kwa miaka 5 tu ya uongozi wake, ilifikia mpk nchi kama Nigeria, Kenya, Uganda, Congo nk wanaomba tungewaazima Rais wetu atawale ktk moja ya hizo nchi just kwa miaka 2 tu halafu waturudishie raisi wetu. Najua kwa mazuri mengi aliyoyafanya haikuwa kazi rahisi kwa yeye kukosa maadui wa nje na ndan ya nchi lkn hiyo haikumkatisha tamaa yeye kufanya aliyoyafanya.

Sasa ameshakufa na yale mazuri kayaacha kwa ajili yetu na vizazi vyetu, inakuaje makundi haya ya wauza unga, mateja, mafisadi, wapiga dili, wataka madaraka, wanywa viloba na wauzaji wao wanaanza kujitokeza kumshambulia alafu raisi na serikali yako mnakaa kimya kuangalia hali hiyo inavyoendelea.

Hivi Rais Samia hauoni kwamba hata na wewe siku ukitoka madarakani au Allah akikuchukua ukiwa bado upo madarakani (Mungu aepushie) makundi haya haya yataibuka kukuchafua? Hawa watu hawana nia nzuri na nchi hii na pia sio watu wazuri kwako na chama chako.

Agenda hii hii watakuja kuitumia mwaka 2025 kuichafua Serikali yako na chama chako, maana watakwambia kuwa na wewe ulikuwa mmoja wa washauri na watu wa karibu ya Hayati Rais Magufuli enzi hizo.

Sasa ili haya yasikukute anza kbs kupiga marufuku makundi haya yasiendelee kumchafua Hayati Magufuli maana inaonesha wazi kwamba wakimaliza kumchafua hayati Magufuli watakugeukia wewe na Serikali yako.

Chukua hatua aliyoichukua yeye alipoingia madarakani kwa kuwaonya wale wote waliokuwa wanawatukana na kuwasema vibaya Marais wetu wastaafu.

Kukaa kwako kimya kuna hatarisha uhai wa chama chako na ni hatari kwa usalama wa nchi. Kama taifa tunahitaji utulivu, amani na maendeleo sio majungu majungu yasiokuwa na faida
 
Zile propaganda ulizokuwa unalishwa kipindi cha Magufuli ndio unazitumia kujenga utetezi wako kwake hapa jukwaani? Ni hivi, hapa unawekwa ukweli wa Magufuli bila kujali ni hasi ama chanya.

Na ukweli huu sio kwamba umeanza alipofariki, bali ukweli huu amekuwa akipewa toka akiwa hai, na sasa ni marudio tu. Nakushauri ww mseme kwa namna ulivyokuwa unamuona ww, acha wengine waseme kwa namna walivyomuona wao.
 
Hamna mtu anayemchafua mwendazake, mwendazake anachafuliwa na matendo yake mwenyewe.
Ufunuo wa Yohana : Mlango 14

13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao
 
Acheni uhuru wa watu kutoa maoni

Jakaya, Mkapa, Mwinyi, Nyerere wote hapa wamchambuliwa na kila mtu kutoa maoni yake juu ya tawala zao!

Hata Samia akitoka nae atapata madongo yake

Hayati Mzee Sitta aliwahi kusema kuwa Mwanasiasa kunahitaji kuwa na 'ngozi' ngumu
 
So unataka wao ndio wa jihukumu kwa sababu wao ndio wanamchafua Hayati.
 
Kwanz kbs napenda kumshukur mw/Mungu kwa kunijaalia uzima, akili, maarifa na afya, lkn pia napenda kutumia nafasi hii kuwasalimu member wote wa jamii forum mliopo humu...
Upuuzi huu ungetafuta wakuna nazi wenzako hapo Lumumba ndiyo ingekuwa pahala pake.

FB_IMG_1593760875709.jpg
tapatalk_1576643810730.jpg
 
Kwanz kbs napenda kumshukur mw/Mungu kwa kunijaalia uzima, akili, maarifa na afya, lkn pia napenda kutumia nafasi hii kuwasalimu member wote wa jamii forum mliopo humu....
Umewahi kusikia maneno freedom of speech? Unajua kuwa Tanzania ni nchi huru na hatuishi kama korea?
 
Magofool ni zaidi ya OIL CHAFU alishajichafua mwenyewe kwa ushetani wake.

Mropokaji na muuaji kama yule tayari ni mchafu haihitaji kuchafuliwa tena.

ALIKUWA ANATUKANA HADI WAZUNGU WALIOMUWEKEA BETRI KWENYE MOYO WAKE, HUYO SI TAA.HI.RA KWELI?
 
Back
Top Bottom