Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,469
- 1,697
- Thread starter
- #41
Hakuna nchi kwenye ulimwengu huu inatawaliwa bila vyama. Hicho ni kitu kinacho eleweka. Labda kama nchi inatawaliwa kifalme. Kwa maana hii namaanisha kuwa viongozi wote kwenye karne hii ambao nchi zao ni member wa UN wamekuwa elected democratically.Mkuu uwezi kusema jambo lolote linaloikumba nchi hii kwa sasa ukawasahau CCM na siasa kwa ujumla kwasababu ata Rais uliyempa hizo nondo apo juu anafata ilani ya chama......
Sasa nikija kwenye maelezo ya hoja yako kuhusu vyama, ninachoweza kukueleza ni kuwa kiongozi yoyote anapochaguliwa na nchi yake kuwa kiongozi wa serikali, yeye kuanzia hapo anakuwa ndiye mwajibikaji kwa mwenendo mzima wa maendeleo ya nchi yake kwa mujibu wa katiba, sheria za nchi na pia utashi wake, usilisahau hili.
Nikupe tu baadhi ya mifano ambayo pengine inaweza kukusaidia kunielewa vizuri;
1. Watendaji wa serikali kama mawaziri, manaibu waziri, makatibu, wakurugenzi na kadhalika wanachaguliwa na Rais mwenyewe na sio chama.
2. Policy ya serikali yeye ndiye anaamua iwe ya aina gani na sio chama.
3. Priorities ya mambo ya kufanya, yeye ndiye anayeamua nini kifanyike kwanza na kipi baadae na kama kweli kitafanyika.
Niendelee zaidi. Nikimchukulia Hayati Rais Magufuli, ndiyo chama chake kilipendekeza au kiliweka sera ya kununua ndege. Hakikuweka sera ya kununua ndege za aina gani. Tumepata ndenge kutokana na utashi wa Hayati Rais Magufuli mwenyewe.
Chama kilipendekeza kuwa na SGR lakini hakiku-specify SGR ya aina gani. Ni maamuzi ya Hayati Rais Magufuli na serikali yake kuwa na SGR ya umeme. Bwawa la Nyerere na miradi mingine mingi kama; daraja la Kigongo-Busisi, Ubungo Flyover, Newe Surrender Bridge na kadhalika na kadhalika. Ningeweza kuendelea hivi kwa mifano mingi zaidi lakini naona ngoja niishie na hiyo, nikitegemea kuwa umenielewa, kwanini sijazungumzia mambo ya chama wala itikadi za chama. Kwani maamuzi mengi yanafaywa na Rais aliyepo madarakani