Rais Samia, maisha ya vijana kwa sasa hayaridhishi. Nguvu kubwa itumike kubadili mfumo wao wa maisha

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,469
1,697
Mama Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa nasikitika leo kusema kuwa mpaka kufikia mwaka 2030 kama nguvu kubwa zaidi hazitatumika za kubadili mfumo mzima wa maisha yetu, nahofia vurugu tunazoziona hivi sasa huko Afrika ya Kusini zikitokea tutazishuhudia zikitokea hapa kwetu pia, tena kwa ukubwa mno.

Sababu zinazonifanya mimi kusema hayo ni very simple, kwani, hali halisi ya maisha ya vijana wetu nchini sio ya kufurahisha, na hasa ukiangalia uwiano wa ongezeko la watu na fursa zinazopatikana kila mwaka za ajira. Kuna watu kwenye hii nchi wakibahatika, wanakula mlo mmoja tu kwa siku. Hali hii haiwezi ikavumilika kwa mda mrefu, lazima iko siku kuna kitu kitatokea.

Japokuwa leo sina takwimu sahihi za wakazi wa Dar es salaam, hata hivyo, inakisiwa kufikia idadi ya watu milioni 8 mpaka milioni 10. Kwa hali hii tutegemee mpaka kufikia mwaka 2030 kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi, yaani idadi ya wakazi milioni 20 kwa Dar es salaam peke yake. Idadi hii ya watu kwa infrustructure ndogo tuliyo nayo, itakuwa maajabu makubwa Mama kama miaka kumi ijayo Tanzania itapita bila msuko suko wowote. Kwa mawazo finyu tuliyo nayo na utendaji kazi wa kusuasua tulio nao huu, naona tunajitengenezea bomu letu wenyewe.

Tukichukua idadi ya watu ya nchi nzima, inaweza ikafika hata takriban watu milioni 100 kufikia mwaka 2030. Hili ni ongezeko kubwa sana la watu kwa nchi ambayo ukuaji wa uchumi wake bado ni wa kusuasua sana.

Kwa mji kama Berlin, Ujerumani, wenye wakazi karibu milion 4 una infrastructure mara 10 zaidi ya Dar es salaam yenye wakazi milioni ~10, si elewi Rais wetu na wasomi wetu nchini mnapata wapi ujasiri wa kulala vizuri na kutoa hotuba za kwamba nchi yetu ni salama. Usalama huu tunaoupigia kelele hivi sasa hatujui kuwa ni latent?

Natambua kuwa kuanzia serikali ya awamu ya tano mpaka hii ya awamu ya sita jitihada kubwa zimefanyika katika kuboresha mazingira yanayo chochea uchumi wetu kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ya Usafiri na uchukuzi, nishati, Afya na elimu.

Haya yote ni mambo mazuri sana na sina budi kuwapongeza, lakini haya peke yake bila kutilia mkazo kwenye ujenzi, uzalishaji na uchakachuaji (processing) wa rasilimali zetu, nahofia kuwa hizi ni jtihada hafifu sana katika kuwawezesha vijana wetu kupata skills zitakazo wapa uwezo mkubwa wa kujiamini na kuthubutu kufanya mambo makubwa ya kuanzisha viwanda ambavyo vitawasaidia wao na wengine kuzalisha ajira za kutosha.

Mama Samia kama hujui nini hivi sasa kipo Tanzania, basi ujue kuwa nchini hakuna mtu anajua nini kinaendelea na coordination ya mpangilio wa kazi na uwajibikaji hauko kabisa. Nani atapata habari wapi na nani anahusika na nini? Hiyo ni changamoto kubwa sana nchini. Watu wamezoea kupata habari kuhusu kitu fulani, ni pale nyie viongozi wajuu mnapotoa hizo habari kwenye mikutano yenu.

Nikupe mifano miwili tu Mama ili unielewe nini namaanisha; watanzania wengi walipata kutambua kuwa chuma yetu mpaka hivi sasa haijaanza kutoa matunda kwa sababu ya kutokuwa na maelewano kati ya serikali na mwekezaji, pale wewe ulipotoa hilo tamko kwenye mkutano wako Mwanza. Jingine ni kuhusu maelezo ya zao la Alizeti kwenye kuhamasisha watu kulima hili zao baada ya Waziri mkuu kutangaza rasmi kweye mkutano wake Singida.

Kama mtu wa kawaida anapata maelezo muhimu kama haya mpaka pale viongozi wajuu wanapo hutubia umma, hiyo ina maana kuwa vyombo vya sekali vinavyo paswa kushughulika na maswala haya na kuihabarisha umma ukaelewa nini kifanyike, hivyo vyombo vimefeli kabisa. Na hii ndiyo sababu inayo pelekea mpaka miradi ya ndani ya mikoa na wilaya kusuasua, kwa sababu ya ziro uwajibikaji kwenye local authority.

Miradi karibu yote jijini Dar es salaam ina matatizo, tukianza na Machinjio Vingunguti, Magorofa ya Magomeni Quarters, Stendi Mwenge, mto Msimbazi, daraja la Segerea na kadhalika na kadhalika. Kwanini waziri aende akabaini kuwa mambo hayako sawa kwenye miradi iliyoko wilayani wakati vyombo vyenye mamlaka hayo vipo? Hakuna mtu anahoji. Waandishi wa habari ndiyo kabisaa, mambo kama haya wao hayawahusu. Kwao habari ni katiba mpya, wabunge wamefanya nini na udaku mwingii!

Mama hizo ni ishara kwamba serikali yako haiko in order. Tafuta tatizo liko wapi!

Kulingana na potential tuliyo nayo serikali yetu ilipaswa kuwekeza kwa nguvu kubwa sana kwenye sekta ya ujenzi, sayansi na teknolojia na uzalishaji ili kupunguza matatizo ya ajira kwa vijana wetu. Kutoa huduma za jamii kama Afya na elimu bila kujenga misingi madhubuti ya kuwafanya vijana wakapata skills na uzoefu wa kazi na badala yake kuwasweka kwenya biashara za uchuuzi (umachinga) za kuuza cheep comodities za kutoka Asia pindi wanapo maliza masomo yao, sijui kama in the long run ni busara. Hili ni bomu Rais wetu.

Ili tuweze piga hatua kubwa kwa mda mfupi nchi yetu haina budi kuwa na viwanda mama. Mpaka hivi sasa Tanzania kama nchi yenye chuma nyingi, gesi asilia nyingi na Helium nyingi ina uwezo wa kuanzisha hivi viwanda kwa nguvu zetu wenyewe. Lazima tuwe na viwanda vya kuzalisha steel, Liquified Natural Gas na Helium. Bila hayo Mama hata ufanye nini, hatutafika kokote.

Products hizi tatu (steel, LNG, Helium) zitakuwa chachu kwa vijana kuweza pata maarifa ya kubuni na ku-create products mbali mbali za kuwa manufactured nchini na hivyo kuzalisha ajira kwa vijana wetu. Tusipo fanya hivyo Mama, unafikiri watapata wapi uzoefu wa ku-practice knowledge walizo zipata kinadharia shuleni na vyuoni? Ni Lazima tuwe na viwanda ambavyo products zake zitatoa products nyingine kem kem. Chuma na LNG ndiyo products pekee tulizo nazo kwa sasa ambazo zinaweza toa products nyingine nyingi za kuzalisha ajira.

Mpaka hivi sasa nikiliangalia deni letu la nje ni ca. 30% ambalo ni sawa na TZS 12.3 Trilioni. Tukiongeza TZS 8.2 Trilioni ambalo ni sawa sawa na 20%. Na kwa mahesbu yagu ya haraka haraka tutakuwa na deni la jumla ya TZS 20.5 Trilioni, ambalo ni 50%. Bado litakuwa ni himilivu.

Ongezeko la deni hili la TZS 8.2 Trilioni tukijumlisha na reserve yetu ya USD 4.5 Bilioni, tunapata TZS 18.6 Trilioni.

Fedha hizi zitamaliza miradi yetu yote ya kimkakati tuliyo nayo kwa haraka zaidi na pia kujenga SGR zetu mpya (Mtwara - Mbamba Bay) (Dar - Arusha na Tanga) na hata kuwa na fedha za kuwekeza kwenye share ya Mtambo wa ku-process Helium yetu kwa ajili ya kuuza ili tupate hela ya haraka haraka.

Sijajua kwanini kuwekeza kwenye helium yetu nayo iwe kikwazo wakati sisi tunaingia ubia na mgunduaji?

Kulingana na takwimu za dunia katika soko la madini ya chuma (Iron ore), inaonekana chuma yetu haina market kabisa. Tunapoteza mda tukisema tumsubiri mwekezaji ndiyo aichimbe na kuiuza kwenye soko la dunia. Ningependa kuishauri serikali yangu kuachana kabisa kabisa na wazo hili. Mimi natambua kuwa hakuna mwekezaji mwenye interest ya kuchimba chuma yetu na kupeleka kwenye soko la dunia. Hayuko!

Hiyo kampuni ya Australia ambayo inatutesa mda wote huu, nina uhakika haina lengo hata moja la kuchimba madini yetu ya chuma, kwani huko kwao, kama ambavyo Mama mwenyewe umekuwa ukisema, kwamba kuna chuma nyingi sana. Na kama haitoshi, nchi yao inaongoza kwa kuuza chuma duniani na vile vile sababu nyingine zinazo mfanya asichimbe chuma yetu ni kukosekana kwa infrastructure ya kuisafirisha chuma yetu kuipeleka bandarini kwa reli.

Kwa hali hii sitegemei kuwa ana nia ya kuhangaika na uchimbaji wa chuma yetu na kuifanyia process tayari kwa kuisafirisha. Mwekezaji hatajenga reli ya kutoka Liganga mpaka Mtwara na hatajenga mtambo wa kufanya process ya kuitayarisha hii chuma kuwa kwenye Kocks hata siku moja. Tutasubiri sana, mpaka tuwe weupeee! Yeye anataka sisi tumjengee, yeye awe mtumiaji tu. Hayo makampuni makubwa yanawaza profit tu. Hayana fikra za maendeleo ya nchi wala watu.

Ndiyo maana haoni haja ya kuhangaika na chuma yetu kwa haraka kihivyo, wakati kwake tayari miundo mbinu hiyo iko. Tusipo chukua hatua za kuihangaikia chuma yetu wenyewe, itakula kwetu Mama. Yeye anazuga tu ili sisi tusichimbe chuma yetu na kumharibia soko. Hiyo ndiyo intention yake. Nashukuru umelitambua hilo Mama. Lakini Mama, kwanini sisi tusiingie ubia naye tukajenga mitambo ya ku-process chuma yetu wenyewe?

Mimi kusema kweli Mama, hata hivyo, hainiingii akirini kuona nchi kubwa na yenye contingent kubwa ya rasilimali watu, wasomi na walio bobea kama Tanzania kushindwa kuitumia potential hii kuupeleka mbele uchumi wetu wenyewe ili kuleta matokeo chanya ya maendeleo yetu? Kwanini unang'ang'ania viongozi ambao hawana vision kuwaweka madarakani Mama?

Kitendo cha kuwasweka vijana wetu kwenye mambo ya uchuuzi na kuifanya nchi yetu iwe jalala la wawekezaji wasio na tija, sidhani kama huo ni mpango wa maana ambao utatuwezesha sisi kufikia malengo tunayo yakusudia. Miradi yetu ya miundo mbinu ambayo serikali inaifanya kwa hivi sasa bado ni midogo sana na nathubutu kusema kuwa haina impact kubwa kwenye ku-ongeza skills au tuseme maarifa mapana katika uzalishaji wa products mbali mbali.

Hili wazo la kuuza chuma kama raw material Mama, kulingana na uzoefu wangu, utanisamehe sana, ni wazo potofu na lisilo na tija kweye maisha yetu. Sijui ni mtu gani ambaye yuko nyuma yako anaye kushauri vitu kama hivyo. Ningependa kumjua. Huyo mshauri wako katika maswala kama haya atakuwa, aidha, haelewi mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi duniani au ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu. Sina maelezo mengine zaidi ya hayo.

Kila mmoja anajua kuwa Australia ni nchi inayo uza chuma (Iron ore) nyingi duniani ikifuatiwa na Brasil, China na India. Lakini Australia na Brasil sio nchi tajiri dunia. China, Amerika, Germany na Japan ni nchi tajiri duniani, kwa sababu zinauza products ambazo zinatengenezwa kutokana na chuma. China sio tu inauza chuma (Iron ore) bali ni manufacturer mzuri wa products zinazotokana na madini ya chuma wanayo chimba wenyewe.

Na sisi tunafanya nini? Tunauza chuma yetu badala ya kuuza steel na products nyingine zinazo tokana na chuma yetu. Hivi nani Mama anatuzuia sisi kuwekeza kwenye Blast furnace yetu wenyewe? Kwanini hatuchukui mfano wa Uganda kuchimba mafuta yao wenyewe? Tanzania kwa bahati nzuri tunazo raw materials zote zinazo hitajika kwenye kuoka chuma yetu wenyewe (Iron Ore, coal, Crom, Nickel na Mangan).

Rais Samia Suluhu Hasanai nchi yetu inahitaji creativity na production of goods na sio mechants peke yake. Why?

Sijaona nchi ambayo imejikita kwenye uuzaji wa raw meterial na biashara peke yake imetajirika na kuwa na uwezo wa kutekeleza mambo mengi ya maendeleo bila msaada kutoka nje. Nchi yenye rasilimali nyingi kama yetu lazima iwe na uwezo wa kiteknolojia bila hili hatufiki mbali na ongezeko kubwa la watu tulilo nalo mwaka hadi mwaka.

Na vile vile hatuwezi tukawa tunaimba wimbo ule ule wa kuwategemea wafanya bishara wa sekta binafsi. Narudia tena kusema kuwa Sekta binafsi nchini haina uwezo wa ku-initiate technological transformation bila assistance ya serikali. Hicho kitu hakipo! Tumeona sisi wenyewe huko nyuma serikali ya Mkapa ilivyodiriki ku-privatize kila kitu. Matokeo yake tukajikuta hatuna ndege, wala treni, wala meli. Kwa maana nyingine watanzania tulibaki kuwa wachuuzi na watumishi.

Tuwachukue watu kama Mohamed Dewj na Barlsessa ambao ni matajiri wetu wakubwa nchini kwa mfano, technological transformation gani wameifanya mpaka sasa, mbali na kuongeza uzalishaji kwa ku-install automaic mashines? Natambua kuna ajira ndogo wamezalisha, sawa, lakini je, tujiulize ni ajira za aina gani hizo? Ni sahihi kuwa na asilimia kubwa ya wafanya kazi ambao maisha yao yote wako kweye production lines upande mmoja na umachinga upande mwingine ? Ndiyo tunataka taifa lenye nguvu kazi za aina hiyo, maadam ni ajira? Ina maana sisi hiyo mifano dunia hautuioni au tunajifanya sisi kuwa ni vipofu?

Mimi nafikiri wote tumeshuhudia, japo kwa kusoma vitabu, jinsi England karne ya 19 na ya 20 ilivyopanda kiuchumi na sasa je, iko wapi? England ilipanda kiuchumi na kiteknolojia kwa sababu ya chuma na uzalishaji wa bidhaa ambazo zinatokana, aidha, na chuma au kutegemea chuma. Toka England ijikite kuwa taifa la watu wafanya biashara la kutoa huduma za kifedha tunaona wapi sasa lina kwenda? Ina maana Wajerumani kiteknolojia wako better zaidi kuliko Waingereza? Sidhani, Waingereza wamepoteza ile spirit yao ya akina James Watt, George Stephenson na wengeineo

Hii clip hapa chini inaonyesha jinsi gani chuma ni muhimu katika productivity. Vitu vyote vinavyo zalishwa kwenye hii clip mtaona vinatokana na aidha, chuma yenyewe, (steel) au nyenzo zinazotokana na chuma. Lakini nyuma ya hivyo vyote ni technology ndiyo imejificha. Na hiyo technology imeletwa na watu ambao ni creative na wenye maarifa mapana (knowledge) ya kufahamu nini cha kufanya. Watanzania wangapi tuna uwezo huo ?

Je, hao wazalishaji wa kwenye viwanda vya matajiri wetu hao wawili wanauwezo huo? Mbali na kuoperate hizo mashine za uzalishaji? Jibu litakuwa hapana. Kwa sababu hatuna material. Lakini kama material ingepatikana nchini wangeweza ku-experiment vitu walivyo visoma na kuviona. Hii ndiyo njia moja wapo ya kuwajengea uwezo vijana wa kuthubutu.

Hakuna mtu anaweza akaleta technological transformation ulimwengu huu, hasa kwenye nchi changa kama yetu bila mkono wa serikali. Werner von Brown ambition yake ya kutengeneza rocket alisaidiwa na serikali ya Hitler na baadae waamerika Marekani. Huyo mwanzilishi wa kampuni ya HUAWEI mwenyewe anasaidiwa na serikali yake.

Nilitegemea matajiri wetu hao wawili kwa kushirikiana na serikali, kuja na ideas kabambe za kuwekeza kwenye teknolijia nchini kama; treni za mitaani, sky trains, utengenezaji wa maboti ya michezo na free style hata mtambo wa kuchakachua gesi asilia (LNG). Lakini kwa vile mawazo na fikra zao ziko katika profit maximization tu na sio kingine, sidhani kama wanahangaika na hayo.

Aliko Dangote kwa kushirikiana na serikali yake ya Nigeria anawekeza nchini kwake kwenye Oil refinary. Kwenye hii project, sio tu ajira zitazalishwa, bali technological transformation itatokea na hivyo kuufanya mfumo wa maisha kubadilika. Na hapa inaonyesha kuwa serikali ndiyo inawawezesha watu wake.

Hizi moves zote tunazo ziona kutoka Amerika, kwa mfano, na hasa actions za kijeshi, mnafikiri bila Pentagon kushirikiana na hayo makampuni ya kutengeneza hizo movies wangeweza peke yao? Amerika ina wekeza mabilion ya fedha kwenye hizo movies kama propaganda za kuitangaza nchi yao na kuwaattrackt watu wenye vichwa na pesa kuwekeza nchini kwao. Nilitegemea Mawaziri na watendaji kwenye serikali yako wanakuwa innovative kwenye maswala haya.

Kitu gani kinaizuia TANAPA kwa mfano, kuzinadi mbuga zetu kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kama; CNN, BBC, Al Jezeera, DW na kadhalika? Kwani kutoa matangazo ya kibiashara kwenye hiyo mitandao inacost kiasi gani? Huko ndiyo kukosa maarifa mapana. Ni kitu so simple. Lazima taasisi za serikali husika kuwekeza kwenye hili. Bila hivyo hatutavuna kitu. Tutabaki kuimba ngonjera kwenye majukwaa ya mikutano ya mbuga zetu ambazo hakuna atakaye zitambua. Nchi yetu yenyewe imetambulika dunia kwa hivi sasa kwa ujasiri wa Hayati Magufuli.

Ombi langu kwako Mama, tafadhali wahamasishe watendaji wa serikali yako wakishirikiana na sekta binafsi na Diaspora kuchukua hatua stahiki za haraka kuwekeza kwenye rasilimali watu (kwa kuzingatia swala la kuwa na watu wenye knowledge) na viwanda vya kuchakachua madini yetu ili kukabiliana na changamoto kubwa iliyoko mbeleni ya vijana kukosa ajira.

Naomba kuwasilisha!
 
Yaani nimesoma mpaka nimesisimka,ila Mama Samia anaweza shida mfumo alioukuta ni mgumu sana chini ya chama kimoja cha siasa ambacho kiko busy kuhakikisha wanasalia madarakani hata kwa uchumi mbovu.

Tunajikuta tuna concentrate na issue za kijinga tu na sio za msingi za kujega uchumi.CCM wamebaki kulindana na hawajawahi kuweka mfumo ambao hautegemei chama chao kabisa kwa sababu wanaona secta binafsi zikiwa imara wao wanaondoka madarakani bila kujua dunia inabadilika kwa kasi.Inahitaji raisi na viongozi wawe na fikra za KITAIFA na sio KICHAMA (ingawa CCM itakuwa ngumu sana kutenganisha) Mama Samia anaweza ila mpaka aue mfumo uliopo taratibu na inahitaji si chini ya miaka 10 mpaka 15.

Kwa sheria na mtazamo uliopo ,uwezi ku invest kwenye mazingira haya ya kitanzania kwa kuwa sheria haikulindi na kila Rais anaingia madarakani na mtazamo wake kwa kuwa hatuna sera za kitaifa rather za kichama.
 
Yaani nimesoma mpaka nimesisimka,ila Mama Samia anaweza shida mfumo alioukuta ni mgumu sana chini ya chama kimoja cha siasa ambacho kiko busy kuhakikisha wanasalia madarakani hata kwa uchumi mbovu...
Nitarudi kufafanua jinsi ya kufanya. Asante sana kwa mchango wako.
 
Mkuu hongera sana yaan watu km nyie ndo mnatakiwa kuwa bungeni maana unatoa mawazo mazuri sana.Tatizo Tanzania hatuna viongozi wenye vision wapo wapo tu hapo ndo tunakwama.

Ifike mahari hata liundwe bunge la wananchi kila wilaya watoke hata watu watano walio na idea ama mbinu za kuinua wilaya zao kwa mazingira ama rasilimali zinazowanzuguka waje waziwakilishe kitaifa yaan tutengeneze kipindi kinarushwa na tv zote kwa wiki nzima ili watu mbalimbali wapate kujua ni wapi wawekeze ama nn kifanyike.

Maana km kila mtu akaja na mawazo mapana yaliyo jitosheleza kama haya na pia tukazisema changamoto tutapiga hatua km taifa.Maana bunge letu kwa kweli limekwama sana.
 
Yaani nimesoma mpaka nimesisimka,ila Mama Samia anaweza shida mfumo alioukuta ni mgumu sana chini ya chama kimoja cha siasa ambacho kiko busy kuhakikisha wanasalia madarakani hata kwa uchumi mbovu.

Tunajikuta tuna concentrate na issue za kijinga tu na sio za msingi za kujega uchumi.CCM wamebaki kulindana na hawajawahi kuweka mfumo ambao hautegemei chama chao kabisa kwa sababu wanaona secta binafsi zikiwa imara wao wanaondoka madarakani bila kujua dunia inabadilika kwa kasi.Inahitaji raisi na viongozi wawe na fikra za KITAIFA na sio KICHAMA (ingawa CCM itakuwa ngumu sana kutenganisha) Mama Samia anaweza ila mpaka aue mfumo uliopo taratibu na inahitaji si chini ya miaka 10 mpaka 15.

Kwa sheria na mtazamo uliopo ,uwezi ku invest kwenye mazingira haya ya kitanzania kwa kuwa sheria haikulindi na kila Rais anaingia madarakani na mtazamo wake kwa kuwa hatuna sera za kitaifa rather za kichama.
Hamna anachoweza huyo mama zaidi ya kuongeza tozo tu
 
Binafsi nakushukuru Sana ndugu mleta mada. Hii mada kwangu Ni mada bora Sana karibu kuliko mada zote haswa kwa upande wa Nini kifanyike tutoke hapa tulipo.

Ningetamani mno mh rais akafikishiwa ujumbe huu, na ikiwezekana asome mwenyewe na kurudia mara nyingi kadiri ajaliwavyo.

Mada Kama hii haijawasilishwa na mtu mwenye kutaka interest, Bali Ni mwananchi mwenye vision na Nia njema kwa taifa lake.

Sio Kama Wanasiasa ambao kwamba wao kila leo hamasa yao kwa wananchi Ni kuigomea serikali mambo yake bila ya kutoa Nini kifanyike.

Huko serikalini nako kumejawa wasomi wengi katika nyanja zote lakini ama wameshindwa kuonyesha vision yao kwa sababu zilizo juu ya uwezo wao au nje ya uwezo wao.

Lakini mada Kama hii inatakiwa ingaliwe kwa jicho la tatu na viongozi wa Uma na kuja na namna ya kufanya tuweze kutoka hapa.

Hii nguvu kubwa ya vijana inayo potea kwa kufanya umachinga wakati mmoja tutakuja kuikumbuka Kama taifa.
Serikali Kama serikali inatakiwa ifanye vyovyote vile kuitumia nguvu ya vijana iliopo Leo kwa manufaa ya taifa letu kesho.

Kwangu ninaamini Jana Ni njema kadhalika na leo, lakini kesho ni Bora zaidi. Lakini pia kesho Bora huundwa na leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kubwa ni kufuata mkumbo, unawezaje kusema kwamba unataka kuwajaza noti wananchi au kuongeza mzunguko wa pesa bila kuweka vipaumbele vya kufanya kazi? Wezi wa mafuta Kigamboni wameachiwa huru kwa sababu tu wezi hao walikuwa wanafanya hayo kwa maelekezo ya viongozi. Utawala wa kuachia madawa ya kulevya ndio tunakokwenda, huu uswahili swahili unalichelewesha taifa. Rais anaamuru BOT kufanya uchunguzi wa Crypto currency kutumia pesa za walipa kodi wakati hata nchi kubwa zilizoendelea zinazuia utakatishaji wa pesa na usiri wa crypto. Nani Tanzania wanatumia crypto kama sio wauza unga na watakatishaji wa pesa?

Vijana wa Tanzania wasitegemee uongozi huu kuwavusha kwa sababu wanaoangaliwa kuvushwa ni watoto wao pekee na watoto wa matajiri. Tena muda si mrefu mtaanza kufukuzwa mjini kuwapisha wawekezaji kutoka nje maana wamepata haki miliki ya kukaa nchini na kuwatumikisha kama punda. (Mnakuwa watumwa kwenye nchi yenu wenyewe).
 
Asante sana mkuu. Nimefarjika na kuguswa sana mchango wako. Watu kama nyinyi wenye mawazo mapana ya kujenga taifa ndiyo nchi yetu inawahitaji. Shukran sana kwa nyingine.
 
Tatizo kubwa ni kufuata mkumbo, unawezaje kusema kwamba unataka kuwajaza noti wananchi au kuongeza mzunguko wa pesa bila kuweka vipaumbele vya kufanya kazi? Wezi wa mafuta Kigamboni wameachiwa huru kwa sababu tu wezi hao walikuwa wanafanya hayo kwa maelekezo ya viongozi. Utawala wa kuachia madawa ya kulevya ndio tunakokwenda, huu uswahili swahili unalichelewesha taifa. Rais anaamuru BOT kufanya uchunguzi wa Crypto currency kutumia pesa za walipa kodi wakati hata nchi kubwa zilizoendelea zinazuia utakatishaji wa pesa na usiri wa crypto. Nani Tanzania wanatumia crypto kama sio wauza unga na watakatishaji wa pesa?

Vijana wa Tanzania wasitegemee uongozi huu kuwavusha kwa sababu wanaoangaliwa kuvushwa ni watoto wao pekee na watoto wa matajiri. Tena muda si mrefu mtaanza kufukuzwa mjini kuwapisha wawekezaji kutoka nje maana wamepata haki miliki ya kukaa nchini na kuwatumikisha kama punda. (Mnakuwa watumwa kwenye nchi yenu wenyewe).
Duh! Hiyo itakuwa ndiyo mwazo wa watumwa kwenye nchi yetu nini? Masikini Tanzania!
 
CCM na viongozi wake ni chama kilichofika ukoma wa kufikiri na hakifai kuendelea kuongoza hii nchi.
Itikadi za kisiasa peke yake hazitasaidia kutatua matatizo yajayo. Wapinzania wanalo moja tu kwenye fikra zao kubadili katiba ili wapate nafasi ya kuingia madarakani au kushika Dola. Sawa. Wakishika dola what commes next? Ajira?

Siasa sio solution, kwani sioni sera yao mbali na kubadili katiba. Tatizo tulilo nalo ninkubwa mno. Tunahitaji ushirikiano wetu wote.

Tukijifanya kuleta ubinafsi katika maswala muhimu kama haya tunaliangamiza taifa letu.
Vijana wetu wataishije baadae?
 
Mkuu hongera sana yaan watu km nyie ndo mnatakiwa kuwa bungeni maana unatoa mawazo mazuri sana.Tatizo Tanzania hatuna viongozi wenye vision wapo wapo tu hapo ndo tunakwama.

Ifike mahari hata liundwe bunge la wananchi kila wilaya watoke hata watu watano walio na idea ama mbinu za kuinua wilaya zao kwa mazingira ama rasilimali zinazowanzuguka waje waziwakilishe kitaifa yaan tutengeneze kipindi kinarushwa na tv zote kwa wiki nzima ili watu mbalimbali wapate kujua ni wapi wawekeze ama nn kifanyike.

Maana km kila mtu akaja na mawazo mapana yaliyo jitosheleza kama haya na pia tukazisema changamoto tutapiga hatua km taifa.Maana bunge letu kwa kweli limekwama sana.

Hivi rais SSH akilivunja bunge ghafla na kuitisha uchaguzi huru nini kitatokea?
 
90 ya wabunge hawatatoboa maana sio kwa kuwachoka huku ..mfano mtu yuko bungeni miaka 20 yy wazo analotoa ni kukata kodi kwenye miamala huyo nae ndo wakumchagua kweli wakati Tanzania tuna mali asili kibao tu mkuu km wangetunga sera safi leo Watanzania tusingekua tunalia na ajira wala makato ya miamala.
 
Mama Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa nasikitika leo kusema kuwa mpaka kufikia mwaka 2030 kama nguvu kubwa zaidi hazitatumika za kubadili mfumo mzima wa maisha yetu, nahofia vurugu tunazoziona hivi sasa huko Afrika ya Kusini zikitokea tutazishuhudia zikitokea hapa kwetu pia, tena kwa ukubwa mno.

Sababu zinazonifanya mimi kusema hayo ni very simple, kwani, hali halisi ya maisha ya vijana wetu nchini sio ya kufurahisha, na hasa ukiangalia uwiano wa ongezeko la watu na fursa zinazopatikana kila mwaka za ajira. Kuna watu kwenye hii nchi wakibahatika, wanakula mlo mmoja tu kwa siku. Hali hii haiwezi ikavumilika kwa mda mrefu, lazima iko siku kuna kitu kitatokea.

Japokuwa leo sina takwimu sahihi za wakazi wa Dar es salaam, hata hivyo, inakisiwa kufikia idadi ya watu milioni 8 mpaka milioni 10. Kwa hali hii tutegemee mpaka kufikia mwaka 2030 kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi, yaani idadi ya wakazi milioni 20 kwa Dar es salaam peke yake. Idadi hii ya watu kwa infrustructure ndogo tuliyo nayo, itakuwa maajabu makubwa Mama kama miaka kumi ijayo Tanzania itapita bila msuko suko wowote. Kwa mawazo finyu tuliyo nayo na utendaji kazi wa kusuasua tulio nao huu, naona tunajitengenezea bomu letu wenyewe.

Tukichukua idadi ya watu ya nchi nzima, inaweza ikafika hata takriban watu milioni 100 kufikia mwaka 2030. Hili ni ongezeko kubwa sana la watu kwa nchi ambayo ukuaji wa uchumi wake bado ni wa kusuasua sana.

Kwa mji kama Berlin, Ujerumani, wenye wakazi karibu milion 4 una infrastructure mara 10 zaidi ya Dar es salaam yenye wakazi milioni ~10, si elewi Rais wetu na wasomi wetu nchini mnapata wapi ujasiri wa kulala vizuri na kutoa hotuba za kwamba nchi yetu ni salama. Usalama huu tunaoupigia kelele hivi sasa hatujui kuwa ni latent?

Natambua kuwa kuanzia serikali ya awamu ya tano mpaka hii ya awamu ya sita jitihada kubwa zimefanyika katika kuboresha mazingira yanayo chochea uchumi wetu kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ya Usafiri na uchukuzi, nishati, Afya na elimu.

Haya yote ni mambo mazuri sana na sina budi kuwapongeza, lakini haya peke yake bila kutilia mkazo kwenye ujenzi, uzalishaji na uchakachuaji (processing) wa rasilimali zetu, nahofia kuwa hizi ni jtihada hafifu sana katika kuwawezesha vijana wetu kupata skills zitakazo wapa uwezo mkubwa wa kujiamini na kuthubutu kufanya mambo makubwa ya kuanzisha viwanda ambavyo vitawasaidia wao na wengine kuzalisha ajira za kutosha.

Mama Samia kama hujui nini hivi sasa kipo Tanzania, basi ujue kuwa nchini hakuna mtu anajua nini kinaendelea na coordination ya mpangilio wa kazi na uwajibikaji hauko kabisa. Nani atapata habari wapi na nani anahusika na nini? Hiyo ni changamoto kubwa sana nchini. Watu wamezoea kupata habari kuhusu kitu fulani, ni pale nyie viongozi wajuu mnapotoa hizo habari kwenye mikutano yenu.

Nikupe mifano miwili tu Mama ili unielewe nini namaanisha; watanzania wengi walipata kutambua kuwa chuma yetu mpaka hivi sasa haijaanza kutoa matunda kwa sababu ya kutokuwa na maelewano kati ya serikali na mwekezaji, pale wewe ulipotoa hilo tamko kwenye mkutano wako Mwanza. Jingine ni kuhusu maelezo ya zao la Alizeti kwenye kuhamasisha watu kulima hili zao baada ya Waziri mkuu kutangaza rasmi kweye mkutano wake Singida.

Kama mtu wa kawaida anapata maelezo muhimu kama haya mpaka pale viongozi wajuu wanapo hutubia umma, hiyo ina maana kuwa vyombo vya sekali vinavyo paswa kushughulika na maswala haya na kuihabarisha umma ukaelewa nini kifanyike, hivyo vyombo vimefeli kabisa. Na hii ndiyo sababu inayo pelekea mpaka miradi ya ndani ya mikoa na wilaya kusuasua, kwa sababu ya ziro uwajibikaji kwenye local authority.

Miradi karibu yote jijini Dar es salaam ina matatizo, tukianza na Machinjio Vingunguti, Magorofa ya Magomeni Quarters, Stendi Mwenge, mto Msimbazi, daraja la Segerea na kadhalika na kadhalika. Kwanini waziri aende akabaini kuwa mambo hayako sawa kwenye miradi iliyoko wilayani wakati vyombo vyenye mamlaka hayo vipo? Hakuna mtu anahoji. Waandishi wa habari ndiyo kabisaa, mambo kama haya wao hayawahusu. Kwao habari ni katiba mpya, wabunge wamefanya nini na udaku mwingii!

Mama hizo ni ishara kwamba serikali yako haiko in order. Tafuta tatizo liko wapi!

Kulingana na potential tuliyo nayo serikali yetu ilipaswa kuwekeza kwa nguvu kubwa sana kwenye sekta ya ujenzi, sayansi na teknolojia na uzalishaji ili kupunguza matatizo ya ajira kwa vijana wetu. Kutoa huduma za jamii kama Afya na elimu bila kujenga misingi madhubuti ya kuwafanya vijana wakapata skills na uzoefu wa kazi na badala yake kuwasweka kwenya biashara za uchuuzi (umachinga) za kuuza cheep comodities za kutoka Asia pindi wanapo maliza masomo yao, sijui kama in the long run ni busara. Hili ni bomu Rais wetu.

Ili tuweze piga hatua kubwa kwa mda mfupi nchi yetu haina budi kuwa na viwanda mama. Mpaka hivi sasa Tanzania kama nchi yenye chuma nyingi, gesi asilia nyingi na Helium nyingi ina uwezo wa kuanzisha hivi viwanda kwa nguvu zetu wenyewe. Lazima tuwe na viwanda vya kuzalisha steel, Liquified Natural Gas na Helium. Bila hayo Mama hata ufanye nini, hatutafika kokote.

Products hizi tatu (steel, LNG, Helium) zitakuwa chachu kwa vijana kuweza pata maarifa ya kubuni na ku-create products mbali mbali za kuwa manufactured nchini na hivyo kuzalisha ajira kwa vijana wetu. Tusipo fanya hivyo Mama, unafikiri watapata wapi uzoefu wa ku-practice knowledge walizo zipata kinadharia shuleni na vyuoni? Ni Lazima tuwe na viwanda ambavyo products zake zitatoa products nyingine kem kem. Chuma na LNG ndiyo products pekee tulizo nazo kwa sasa ambazo zinaweza toa products nyingine nyingi za kuzalisha ajira.

Mpaka hivi sasa nikiliangalia deni letu la nje ni ca. 30% ambalo ni sawa na TZS 12.3 Trilioni. Tukiongeza TZS 8.2 Trilioni ambalo ni sawa sawa na 20%. Na kwa mahesbu yagu ya haraka haraka tutakuwa na deni la jumla ya TZS 20.5 Trilioni, ambalo ni 50%. Bado litakuwa ni himilivu.

Ongezeko la deni hili la TZS 8.2 Trilioni tukijumlisha na reserve yetu ya USD 4.5 Bilioni, tunapata TZS 18.6 Trilioni.

Fedha hizi zitamaliza miradi yetu yote ya kimkakati tuliyo nayo kwa haraka zaidi na pia kujenga SGR zetu mpya (Mtwara - Mbamba Bay) (Dar - Arusha na Tanga) na hata kuwa na fedha za kuwekeza kwenye share ya Mtambo wa ku-process Helium yetu kwa ajili ya kuuza ili tupate hela ya haraka haraka.

Sijajua kwanini kuwekeza kwenye helium yetu nayo iwe kikwazo wakati sisi tunaingia ubia na mgunduaji?

Kulingana na takwimu za dunia katika soko la madini ya chuma (Iron ore), inaonekana chuma yetu haina market kabisa. Tunapoteza mda tukisema tumsubiri mwekezaji ndiyo aichimbe na kuiuza kwenye soko la dunia. Ningependa kuishauri serikali yangu kuachana kabisa kabisa na wazo hili. Mimi natambua kuwa hakuna mwekezaji mwenye interest ya kuchimba chuma yetu na kupeleka kwenye soko la dunia. Hayuko!

Hiyo kampuni ya Australia ambayo inatutesa mda wote huu, nina uhakika haina lengo hata moja la kuchimba madini yetu ya chuma, kwani huko kwao, kama ambavyo Mama mwenyewe umekuwa ukisema, kwamba kuna chuma nyingi sana. Na kama haitoshi, nchi yao inaongoza kwa kuuza chuma duniani na vile vile sababu nyingine zinazo mfanya asichimbe chuma yetu ni kukosekana kwa infrastructure ya kuisafirisha chuma yetu kuipeleka bandarini kwa reli.

Kwa hali hii sitegemei kuwa ana nia ya kuhangaika na uchimbaji wa chuma yetu na kuifanyia process tayari kwa kuisafirisha. Mwekezaji hatajenga reli ya kutoka Liganga mpaka Mtwara na hatajenga mtambo wa kufanya process ya kuitayarisha hii chuma kuwa kwenye Kocks hata siku moja. Tutasubiri sana, mpaka tuwe weupeee! Yeye anataka sisi tumjengee, yeye awe mtumiaji tu. Hayo makampuni makubwa yanawaza profit tu. Hayana fikra za maendeleo ya nchi wala watu.

Ndiyo maana haoni haja ya kuhangaika na chuma yetu kwa haraka kihivyo, wakati kwake tayari miundo mbinu hiyo iko. Tusipo chukua hatua za kuihangaikia chuma yetu wenyewe, itakula kwetu Mama. Yeye anazuga tu ili sisi tusichimbe chuma yetu na kumharibia soko. Hiyo ndiyo intention yake. Nashukuru umelitambua hilo Mama. Lakini Mama, kwanini sisi tusiingie ubia naye tukajenga mitambo ya ku-process chuma yetu wenyewe?

Mimi kusema kweli Mama, hata hivyo, hainiingii akirini kuona nchi kubwa na yenye contingent kubwa ya rasilimali watu, wasomi na walio bobea kama Tanzania kushindwa kuitumia potential hii kuupeleka mbele uchumi wetu wenyewe ili kuleta matokeo chanya ya maendeleo yetu? Kwanini unang'ang'ania viongozi ambao hawana vision kuwaweka madarakani Mama?

Kitendo cha kuwasweka vijana wetu kwenye mambo ya uchuuzi na kuifanya nchi yetu iwe jalala la wawekezaji wasio na tija, sidhani kama huo ni mpango wa maana ambao utatuwezesha sisi kufikia malengo tunayo yakusudia. Miradi yetu ya miundo mbinu ambayo serikali inaifanya kwa hivi sasa bado ni midogo sana na nathubutu kusema kuwa haina impact kubwa kwenye ku-ongeza skills au tuseme maarifa mapana katika uzalishaji wa products mbali mbali.

Hili wazo la kuuza chuma kama raw material Mama, kulingana na uzoefu wangu, utanisamehe sana, ni wazo potofu na lisilo na tija kweye maisha yetu. Sijui ni mtu gani ambaye yuko nyuma yako anaye kushauri vitu kama hivyo. Ningependa kumjua. Huyo mshauri wako katika maswala kama haya atakuwa, aidha, haelewi mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi duniani au ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu. Sina maelezo mengine zaidi ya hayo.

Kila mmoja anajua kuwa Australia ni nchi inayo uza chuma (Iron ore) nyingi duniani ikifuatiwa na Brasil, China na India. Lakini Australia na Brasil sio nchi tajiri dunia. China, Amerika, Germany na Japan ni nchi tajiri duniani, kwa sababu zinauza products ambazo zinatengenezwa kutokana na chuma. China sio tu inauza chuma (Iron ore) bali ni manufacturer mzuri wa products zinazotokana na madini ya chuma wanayo chimba wenyewe.

Na sisi tunafanya nini? Tunauza chuma yetu badala ya kuuza steel na products nyingine zinazo tokana na chuma yetu. Hivi nani Mama anatuzuia sisi kuwekeza kwenye Blast furnace yetu wenyewe? Kwanini hatuchukui mfano wa Uganda kuchimba mafuta yao wenyewe? Tanzania kwa bahati nzuri tunazo raw materials zote zinazo hitajika kwenye kuoka chuma yetu wenyewe (Iron Ore, coal, Crom, Nickel na Mangan).

Rais Samia Suluhu Hasanai nchi yetu inahitaji creativity na production of goods na sio mechants peke yake. Why?

Sijaona nchi ambayo imejikita kwenye uuzaji wa raw meterial na biashara peke yake imetajirika na kuwa na uwezo wa kutekeleza mambo mengi ya maendeleo bila msaada kutoka nje. Nchi yenye rasilimali nyingi kama yetu lazima iwe na uwezo wa kiteknolojia bila hili hatufiki mbali na ongezeko kubwa la watu tulilo nalo mwaka hadi mwaka.

Na vile vile hatuwezi tukawa tunaimba wimbo ule ule wa kuwategemea wafanya bishara wa sekta binafsi. Narudia tena kusema kuwa Sekta binafsi nchini haina uwezo wa ku-initiate technological transformation bila assistance ya serikali. Hicho kitu hakipo! Tumeona sisi wenyewe huko nyuma serikali ya Mkapa ilivyodiriki ku-privatize kila kitu. Matokeo yake tukajikuta hatuna ndege, wala treni, wala meli. Kwa maana nyingine watanzania tulibaki kuwa wachuuzi na watumishi.

Tuwachukue watu kama Mohamed Dewj na Barlsessa ambao ni matajiri wetu wakubwa nchini kwa mfano, technological transformation gani wameifanya mpaka sasa, mbali na kuongeza uzalishaji kwa ku-install automaic mashines? Natambua kuna ajira ndogo wamezalisha, sawa, lakini je, tujiulize ni ajira za aina gani hizo? Ni sahihi kuwa na asilimia kubwa ya wafanya kazi ambao maisha yao yote wako kweye production lines upande mmoja na umachinga upande mwingine ? Ndiyo tunataka taifa lenye nguvu kazi za aina hiyo, maadam ni ajira? Ina maana sisi hiyo mifano dunia hautuioni au tunajifanya sisi kuwa ni vipofu?

Mimi nafikiri wote tumeshuhudia, japo kwa kusoma vitabu, jinsi England karne ya 19 na ya 20 ilivyopanda kiuchumi na sasa je, iko wapi? England ilipanda kiuchumi na kiteknolojia kwa sababu ya chuma na uzalishaji wa bidhaa ambazo zinatokana, aidha, na chuma au kutegemea chuma. Toka England ijikite kuwa taifa la watu wafanya biashara la kutoa huduma za kifedha tunaona wapi sasa lina kwenda? Ina maana Wajerumani kiteknolojia wako better zaidi kuliko Waingereza? Sidhani, Waingereza wamepoteza ile spirit yao ya akina James Watt, George Stephenson na wengeineo

Hii clip hapa chini inaonyesha jinsi gani chuma ni muhimu katika productivity. Vitu vyote vinavyo zalishwa kwenye hii clip mtaona vinatokana na aidha, chuma yenyewe, (steel) au nyenzo zinazotokana na chuma. Lakini nyuma ya hivyo vyote ni technology ndiyo imejificha. Na hiyo technology imeletwa na watu ambao ni creative na wenye maarifa mapana (knowledge) ya kufahamu nini cha kufanya. Watanzania wangapi tuna uwezo huo ?

Je, hao wazalishaji wa kwenye viwanda vya matajiri wetu hao wawili wanauwezo huo? Mbali na kuoperate hizo mashine za uzalishaji? Jibu litakuwa hapana. Kwa sababu hatuna material. Lakini kama material ingepatikana nchini wangeweza ku-experiment vitu walivyo visoma na kuviona. Hii ndiyo njia moja wapo ya kuwajengea uwezo vijana wa kuthubutu.

Hakuna mtu anaweza akaleta technological transformation ulimwengu huu, hasa kwenye nchi changa kama yetu bila mkono wa serikali. Werner von Brown ambition yake ya kutengeneza rocket alisaidiwa na serikali ya Hitler na baadae waamerika Marekani. Huyo mwanzilishi wa kampuni ya HUAWEI mwenyewe anasaidiwa na serikali yake.

Nilitegemea matajiri wetu hao wawili kwa kushirikiana na serikali, kuja na ideas kabambe za kuwekeza kwenye teknolijia nchini kama; treni za mitaani, sky trains, utengenezaji wa maboti ya michezo na free style hata mtambo wa kuchakachua gesi asilia (LNG). Lakini kwa vile mawazo na fikra zao ziko katika profit maximization tu na sio kingine, sidhani kama wanahangaika na hayo.

Aliko Dangote kwa kushirikiana na serikali yake ya Nigeria anawekeza nchini kwake kwenye Oil refinary. Kwenye hii project, sio tu ajira zitazalishwa, bali technological transformation itatokea na hivyo kuufanya mfumo wa maisha kubadilika. Na hapa inaonyesha kuwa serikali ndiyo inawawezesha watu wake.

Hizi moves zote tunazo ziona kutoka Amerika, kwa mfano, na hasa actions za kijeshi, mnafikiri bila Pentagon kushirikiana na hayo makampuni ya kutengeneza hizo movies wangeweza peke yao? Amerika ina wekeza mabilion ya fedha kwenye hizo movies kama propaganda za kuitangaza nchi yao na kuwaattrackt watu wenye vichwa na pesa kuwekeza nchini kwao. Nilitegemea Mawaziri na watendaji kwenye serikali yako wanakuwa innovative kwenye maswala haya.

Kitu gani kinaizuia TANAPA kwa mfano, kuzinadi mbuga zetu kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kama; CNN, BBC, Al Jezeera, DW na kadhalika? Kwani kutoa matangazo ya kibiashara kwenye hiyo mitandao inacost kiasi gani? Huko ndiyo kukosa maarifa mapana. Ni kitu so simple. Lazima taasisi za serikali husika kuwekeza kwenye hili. Bila hivyo hatutavuna kitu. Tutabaki kuimba ngonjera kwenye majukwaa ya mikutano ya mbuga zetu ambazo hakuna atakaye zitambua. Nchi yetu yenyewe imetambulika dunia kwa hivi sasa kwa ujasiri wa Hayati Magufuli.

Ombi langu kwako Mama, tafadhali wahamasishe watendaji wa serikali yako wakishirikiana na sekta binafsi na Diaspora kuchukua hatua stahiki za haraka kuwekeza kwenye rasilimali watu (kwa kuzingatia swala la kuwa na watu wenye knowledge) na viwanda vya kuchakachua madini yetu ili kukabiliana na changamoto kubwa iliyoko mbeleni ya vijana kukosa ajira.

Naomba kuwasilisha!

Huyu bibi hafai tena.
 
90 ya wabunge hawatatoboa maana sio kwa kuwachoka huku ..mfano mtu yuko bungeni miaka 20 yy wazo analotoa ni kukata kodi kwenye miamala huyo nae ndo wakumchagua kweli wakati Tanzania tuna mali asili kibao tu mkuu km wangetunga sera safi leo Watanzania tusingekua tunalia na ajira wala makato ya miamala.
Kabasa. Wanafikiri bado wanamda. Hawajui kusoma nyakati.
 
Back
Top Bottom