Rais Samia kuitikisa Mwanza Tarehe 30 Januari

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa kuitikisa na kuliteka jiji la Mwanza Tarehe 30 januari.

Kwa hiyo wana Mwanza kaeni mkao wa kumpokea Mama yetu na Shujaa Wetu ambaye wakati wote ametuongoza kwa ujasiri ,uimara , umadhubuti na uhodari wa hali juu sana.ametimiza ile kauli yake ya kwamba tutizame mbele kwa matumaini na siyo hofu.

Kwa kweli na kwa hakika katika mikono ya Rais Samia kila mtazania amejaa matumaini tele katika imani ya kutimiza ndoto zake. Ni kweli ndugu zangu nakubali kuwa changamoto huwa hazikosekani kwa nchi yoyote ile.lakini Watanzania wenzangu kwa macho yetu tunajionea juhudi kubwa sana na zenye dhamira njema zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kikubwa tuendelee kumuunga mkono,kumpa ushirikiano na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania. Mama yetu ni binadamu kama tulivyo sisi .ni mtumishi wetu mwaminifu ,mkweli na mnyenyekevu wa hali ya juu sana .tusikubali na tusikae kimya tuonapo wachache wenye maslahi binafsi wanamshambulia kwa lugha za matusi na kudhalilisha na wanataka kumkwamisha na kuwa kikwazo katika kututumikia watanzania.

Wakati wote tuwe upande wa Rais wetu kwa kuwa sote tunajionea namna anavyofanya kazi kwa ajili yetu.tunapoona tuna neno au ushauri wa vipi angefanya katika jambo fulani, basi tumshauri kwa lugha za staha,adabu ,hekima na uungwana .kwa sababu Rais wetu ni Mama msikivu,mpole, mnyenyekevu,muungwana na mwenye upendo wa hali ya juu sana kwetu watanzania.ndio maana amekuwa akitushirikisha na kutuweka wazi kwa kila hatua au maamuzi ambayo serikali yetu inafanya na kwanini inafanya.

Hii ndio sababu katika awamu hii wengi wa watanzania tunakuwa tunaelewa na kufahamu kila kitu kinachokuwa kinaendelea katika serikali yetu juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu ni serikali ya UWAZI Na UKWELI. Ni serikali inayoendeshwa na kufanya mambo yake hadharani na siyo gizani. Tunataka nini tena Watanzania kwa mama huyu mzalendo wa kweli? Afanye nini tena cha ziada ndugu zangu? Mama ni mwanadamu lakini katika uwanadanamu wake amejitahidi katika kila njia kuhakikisha ya kuwa kila mmoja wetu anajivunia kuzaliwa Tanzania na kuwa mtanzania na kujiona anathamani kubwa katika Taifa hili.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Daima tunamuunga mkono katika makundi yetu mbalimbali na kumuombea Baraka na Neema za Mungu kwenye kazi na majukumu yake ya kuwaletea wanainchi maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumu...
 
Kimbunga cha 24 watu wanapiga MAYOWE !!!
Yaani mnajipaga matumaini hewa nyie hadi huruma. Ndio maana Mbowe anawaburuza huko kama manyumbu. Aliwaambia atastaafu 2015 endapo CHADEMA itashindwa uchaguzi ila hadi saizi anadunda tu na kuwabadilishia gia tu nyumbu wake.
 
Usiwaamini wasukuma wanchosena nitofauti na wanachotenda. Watakwambia ndoho tabu ila kiuhalisia tabu ipo. Kwahiyo hangaya akiwaamini wanamwanza itakula kwake
 
Rais wetu mpendwa anawapenda Watanzania wote na wala hana mawazo wala fikira za kikabila .ndio maana anafanya kazi na kuteua watu wa makabila yote,dini zote,jinsia zote bila ubaguzi wa aina yoyote ile kwa misingi ya aina yoyote ile. Nchi yetu siyo ya kikabila na hatupaswi kuwaza kikabila.
 
Daima tunamuunga mkono katika makundi yetu mbalimbali na kumuombea Baraka na Neema za Mungu kwenye kazi na majukumu yake ya kuwaletea wanainchi maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumu...
Kweli kabisa tuendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa kuitikisa na kuliteka jiji la Mwanza Tarehe 30 januari.

Kwa hiyo wana Mwanza kaeni mkao wa kumpokea Mama yetu na Shujaa Wetu ambaye wakati wote ametuongoza kwa ujasiri ,uimara , umadhubuti na uhodari wa hali juu sana.ametimiza ile kauli yake ya kwamba tutizame mbele kwa matumaini na siyo hofu.

Kwa kweli na kwa hakika katika mikono ya Rais Samia kila mtazania amejaa matumaini tele katika imani ya kutimiza ndoto zake. Ni kweli ndugu zangu nakubali kuwa changamoto huwa hazikosekani kwa nchi yoyote ile.lakini Watanzania wenzangu kwa macho yetu tunajionea juhudi kubwa sana na zenye dhamira njema zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kikubwa tuendelee kumuunga mkono,kumpa ushirikiano na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania. Mama yetu ni binadamu kama tulivyo sisi .ni mtumishi wetu mwaminifu ,mkweli na mnyenyekevu wa hali ya juu sana .tusikubali na tusikae kimya tuonapo wachache wenye maslahi binafsi wanamshambulia kwa lugha za matusi na kudhalilisha na wanataka kumkwamisha na kuwa kikwazo katika kututumikia watanzania.

Wakati wote tuwe upande wa Rais wetu kwa kuwa sote tunajionea namna anavyofanya kazi kwa ajili yetu.tunapoona tuna neno au ushauri wa vipi angefanya katika jambo fulani, basi tumshauri kwa lugha za staha,adabu ,hekima na uungwana .kwa kwa sababu Rais wetu ni Mama msikivu,mpole, mnyenyekevu,muungwana na mwenye upendo wa hali ya juu sana kwetu watanzania.ndio maana amekuwa akitushirikisha na kutuweka wazi kwa kila hatua au maamuzi ambayo serikali yetu inafanya na kwanini inafanya.

Hii ndio sababu katika awamu hii wengi wa watanzania tunakuwa tunaelewa na kufahamu kila kitu kinachokuwa kinaendelea katika serikali yetu juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu ni serikali ya UWAZI Na UKWELI. Ni serikali inayoendeshwa na kufanya mambo yake hadharani na siyo gizani. Tunataka nini tena kwa mama huyu mzalendo wa kweli? Afanye nini tena cha ziada ndugu zangu? Mama ni mwanadamu lakini katika uwanadanamu wake amejitahidi katika kila njia kuhakikisha ya kuwa kila mmoja wetu anajivunia kuzaliwa Tanzania na kuwa mtanzania na kujiona anathamani kubwa katika Taifa hili.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Anatafuta kula maana mwanza ndio kila kitu

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Rais wetu mpendwa anawapenda Watanzania wote na wala hana mawazo wala fikira za kikabila .ndio maana anafanya kazi na kuteua watu wa makabila yote,dini zote,jinsia zote bila ubaguzi wa aina yoyote ile kwa misingi ya aina yoyote ile. Nchi yetu siyo ya kikabila na hatupaswi kuwaza kikabila.
Basi jua mwanza hakubaliki. Kama huamini leo basi utaniamini 2025 kama atagombea. Kanda ya ziwa ni habari nyingine mkuu
 
Anatafuta kula maana mwanza ndio kila kitu

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
Rais wetu hata asipopiga kampeni 2025 na kukaa tu ikulu akiendelea kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili yetu watanzania, bado atapita na kushinda kwa kishindo kitakacho itetemesha Dunia nzima.kwa sababu kila utakako kwenda ni lazima ukutane na alama zake.
 
Atashinda yeye au inashinda Ccm?
 
Basi jua mwanza hakubaliki. Kama huamini leo basi utaniamini 2025 kama atagombea. Kanda ya ziwa ni habari nyingine mkuu
Hakuna mahali na ukanda ambao unaweza kusema Rais Samia hakubaliki. Maana kila ukanda utakaokwenda unakuta wananchi wakimzungumzia vyema sana Mheshimiwa Rais na kusubili sana muda ufike ili waje wampe kura zao za ndio kwa kishindo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom