Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,668
- 10,092
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa kuitikisa na kuliteka jiji la Mwanza Tarehe 30 januari.
Kwa hiyo wana Mwanza kaeni mkao wa kumpokea Mama yetu na Shujaa Wetu ambaye wakati wote ametuongoza kwa ujasiri ,uimara , umadhubuti na uhodari wa hali juu sana.ametimiza ile kauli yake ya kwamba tutizame mbele kwa matumaini na siyo hofu.
Kwa kweli na kwa hakika katika mikono ya Rais Samia kila mtazania amejaa matumaini tele katika imani ya kutimiza ndoto zake. Ni kweli ndugu zangu nakubali kuwa changamoto huwa hazikosekani kwa nchi yoyote ile.lakini Watanzania wenzangu kwa macho yetu tunajionea juhudi kubwa sana na zenye dhamira njema zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa katika kutatua changamoto mbalimbali.
Kikubwa tuendelee kumuunga mkono,kumpa ushirikiano na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania. Mama yetu ni binadamu kama tulivyo sisi .ni mtumishi wetu mwaminifu ,mkweli na mnyenyekevu wa hali ya juu sana .tusikubali na tusikae kimya tuonapo wachache wenye maslahi binafsi wanamshambulia kwa lugha za matusi na kudhalilisha na wanataka kumkwamisha na kuwa kikwazo katika kututumikia watanzania.
Wakati wote tuwe upande wa Rais wetu kwa kuwa sote tunajionea namna anavyofanya kazi kwa ajili yetu.tunapoona tuna neno au ushauri wa vipi angefanya katika jambo fulani, basi tumshauri kwa lugha za staha,adabu ,hekima na uungwana .kwa sababu Rais wetu ni Mama msikivu,mpole, mnyenyekevu,muungwana na mwenye upendo wa hali ya juu sana kwetu watanzania.ndio maana amekuwa akitushirikisha na kutuweka wazi kwa kila hatua au maamuzi ambayo serikali yetu inafanya na kwanini inafanya.
Hii ndio sababu katika awamu hii wengi wa watanzania tunakuwa tunaelewa na kufahamu kila kitu kinachokuwa kinaendelea katika serikali yetu juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu ni serikali ya UWAZI Na UKWELI. Ni serikali inayoendeshwa na kufanya mambo yake hadharani na siyo gizani. Tunataka nini tena Watanzania kwa mama huyu mzalendo wa kweli? Afanye nini tena cha ziada ndugu zangu? Mama ni mwanadamu lakini katika uwanadanamu wake amejitahidi katika kila njia kuhakikisha ya kuwa kila mmoja wetu anajivunia kuzaliwa Tanzania na kuwa mtanzania na kujiona anathamani kubwa katika Taifa hili.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.