Rais Samia kuitikisa Mwanza Tarehe 30 Januari

Rais Samia kuitikisa Mwanza Tarehe 30 Januari

Unatujazia uzwazwa navihoja vyakipambe humu,hili jukwaa ni international... Majukwaa ya wasomi nchi zinazojitambua hukuti hoja zakujipendekeza kitoto kama hizi zako. Ukiweka kitu humu nichetu sote kuchangia sasa weka vyamaana au tuliza niaje!!
Kama uwezo wako ni mdogo ni ngumu kuelewa.hata hivyo naheshimu mawazo yako na upo huru na uwe huru kunikosoa kwa lugha ya aina yoyote ile utakayo wewe.nami nitakujibu kwa uungwana kabisa. Kikubwa hata wewe uwe huru kuandika hapa jukwaani hoja zako unazoona ni nzito na za maana kuliko zangu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa kuitikisa na kuliteka jiji la Mwanza Tarehe 30 januari.

Kwa hiyo wana Mwanza kaeni mkao wa kumpokea Mama yetu na Shujaa Wetu ambaye wakati wote ametuongoza kwa ujasiri ,uimara , umadhubuti na uhodari wa hali juu sana.ametimiza ile kauli yake ya kwamba tutizame mbele kwa matumaini na siyo hofu.

Kwa kweli na kwa hakika katika mikono ya Rais Samia kila mtazania amejaa matumaini tele katika imani ya kutimiza ndoto zake. Ni kweli ndugu zangu nakubali kuwa changamoto huwa hazikosekani kwa nchi yoyote ile.lakini Watanzania wenzangu kwa macho yetu tunajionea juhudi kubwa sana na zenye dhamira njema zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kikubwa tuendelee kumuunga mkono,kumpa ushirikiano na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania. Mama yetu ni binadamu kama tulivyo sisi .ni mtumishi wetu mwaminifu ,mkweli na mnyenyekevu wa hali ya juu sana .tusikubali na tusikae kimya tuonapo wachache wenye maslahi binafsi wanamshambulia kwa lugha za matusi na kudhalilisha na wanataka kumkwamisha na kuwa kikwazo katika kututumikia watanzania.

Wakati wote tuwe upande wa Rais wetu kwa kuwa sote tunajionea namna anavyofanya kazi kwa ajili yetu.tunapoona tuna neno au ushauri wa vipi angefanya katika jambo fulani, basi tumshauri kwa lugha za staha,adabu ,hekima na uungwana .kwa kwa sababu Rais wetu ni Mama msikivu,mpole, mnyenyekevu,muungwana na mwenye upendo wa hali ya juu sana kwetu watanzania.ndio maana amekuwa akitushirikisha na kutuweka wazi kwa kila hatua au maamuzi ambayo serikali yetu inafanya na kwanini inafanya.

Hii ndio sababu katika awamu hii wengi wa watanzania tunakuwa tunaelewa na kufahamu kila kitu kinachokuwa kinaendelea katika serikali yetu juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu ni serikali ya UWAZI Na UKWELI. Ni serikali inayoendeshwa na kufanya mambo yake hadharani na siyo gizani. Tunataka nini tena kwa mama huyu mzalendo wa kweli? Afanye nini tena cha ziada ndugu zangu? Mama ni mwanadamu lakini katika uwanadanamu wake amejitahidi katika kila njia kuhakikisha ya kuwa kila mmoja wetu anajivunia kuzaliwa Tanzania na kuwa mtanzania na kujiona anathamani kubwa katika Taifa hili.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Machawa ndio mnaomharibia Rais. Baadhi wakiona tu maandiko yenye ujinga mwingi kama huu ulioweka, mara sijui chuma cha reli, mara sijui komandoo wa vita, na upumbavu mwingine mwingi, unakuwa tayari umewachefua.

Kwani hakuna watu wenye busara la akili timamu ambao wanaweza kutangaza juu ya hiyo ziara, kuliko ninyi mchawa njaa mnaoandika vioja?

Kama kuna mwenye akili timamu anayejua hii ziara ya Rais inahusu nini, na maeneo gani atatembelea, mwombe aje aandike kwa ufasaha na busara.
 
Rais wetu hata asipopiga kampeni 2025 na kukaa tu ikulu akiendelea kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili yetu watanzania, bado atapita na kushinda kwa kishindo kitakacho itetemesha Dunia nzima.kwa sababu kila utakako kwenda ni lazima ukutane na alama zake.
Unakili za kuku wewe

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
MATARAJIO YATAKAYO TOKEA ZIARA HII YA KIHISTORIA KUBATIZWA AZIMIO LA MWANZA 2024

Mhimili wa Bunge tarehe 30 January 2024 Bunge la Dodoma kujadili miswada iliyokataliwa na umma.

Mhimili wa dola (state) kupitia kiongozi mkuu, utakuwa Mwanza kuwahi kutangaza ipo sikivu kwa kutumia 4Rs na kuamua kuondoa miswada ya sheria za uchaguzi na sheria ya Tume ya Uchaguzi kutokana na hoja mpya zilizoletwa mbele ya kamati ya Bunge, mkutano wa Vyama vya siasa na wadau wa demokrasia bila kusahau madai yaliyotolewa kupitia maandamano ya tarehe 24 January 2024

Wananchi watashangilia sana na hivyo wahafidhina waliokuwa wanamtia hofu rais kuwa maandamano yatageuka kuleta uvunjifu au kupindua nchi wataanguka kwa kuishiwa nguvu.

Kutokana na msimamo wa kiongozi wao mkuu wa CCM kuona umuhimu wa madai ya raia wengi walio na mawazo tofauti na ya wanaojiita msimamo mkali wa kimapinduzi bila kusahau machawa wa kisiasa waliokuwa wamejianda kwa kila hila kulipeleka jahazi la nchi na nahodha wake rais mrama akwae mwamba na chombo kivunjike vipande vipande ..

AZIMIO LA MWANZA JANUARY 30 litaasisiwa na kuwa moja ya maazimio ya kihistoria ktk taifa letu kwa miaka 200 ijayo huku legacy ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan ikikumbukwa kuwa na kiongozi shupavu, msikivu asiye na woga aliyeliivusha taifa toka mikononi kwa wachache walinda maslahi ya vyeo vyao badala ya maslahi mapana ya taifa letu. .


Hali halisi inavyokuwa bungeni mawaziri wanavuja jasho kuelekea January 30 2024

TOKA MAKTABA :

1706289912766.png

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 16 Januari, 2024

Source: kamati-ya-bunge-ya-utawala-katiba-na-sheria-yajadili-taarifa-ya-utekelezaji-wa-maazimio-ya-mkutano-wa-bunge
 
Usiwaamini wasukuma wanchosena nitofauti na wanachotenda. Watakwambia ndoho tabu ila kiuhalisia tabu ipo. Kwahiyo hangaya akiwaamini wanamwanza itakula kwake
Ebu rudia tena. Wiyomba kinehe?
 
Rais wetu hata asipopiga kampeni 2025 na kukaa tu ikulu akiendelea kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili yetu watanzania, bado atapita na kushinda kwa kishindo kitakacho itetemesha Dunia nzima.kwa sababu kila utakako kwenda ni lazima ukutane na alama zake.

Kama alama ndio zinaweka chama madarakani, Hadi Leo ilitakiwa makaburu wa africa kusini wawe madarakani.
 
Mwanza wanapendwa sana na Mama nina hakika hakuna sehemu amekwenda mara nyungi kama Mwanza!
 
Acha uchawa
Rais wetu mpendwa anawapenda Watanzania wote na wala hana mawazo wala fikira za kikabila .ndio maana anafanya kazi na kuteua watu wa makabila yote,dini zote,jinsia zote bila ubaguzi wa aina yoyote ile kwa misingi ya aina yoyote ile. Nchi yetu siyo ya kikabila na hatupaswi kuwaza kikabila.
 
Kama uwezo wako ni mdogo ni ngumu kuelewa.hata hivyo naheshimu mawazo yako na upo huru na uwe huru kunikosoa kwa lugha ya aina yoyote ile utakayo wewe.nami nitakujibu kwa uungwana kabisa. Kikubwa hata wewe uwe huru kuandika hapa jukwaani hoja zako unazoona ni nzito na za maana kuliko zangu.
BE A GENTLEMAN!! DON'T GET FAKE IN ORDER TO SEARCH CHANCES. Hivi weka Yako namba kilasiku hujatafutwaga tuu?? Uskate tamaa ikosiku wapendasifa watakuona...
Shkuru sisi tunaokuchana tunaweza sababisha uonewe huruma utafutwe kupewa kacheo ndugu mkimbiza teuzi
 
AZIMIO LA MWANZA JANUARY 30 litaasisiwa na kuwa moja ya maazimio ya kihistoria ktk taifa letu kwa miaka 200 ijayo huku legacy ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan ikikumbukwa kuwa na kiongozi shupavu, msikivu asiye na woga aliyeliivusha taifa toka mikononi kwa wachache walinda maslahi ya vyeo vyao badala ya maslahi mapana ya taifa letu

Hali inavyokuwa wakipata maagizo toka juu, usiku na mchana wanapambana kufuata maelekezo mapya

  1. Habari

Habari​

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAJADILI TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA BUNGE​


1706290125048.png

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kamati hiyo na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ktk ofisi za Bunge jijini Dodoma tarehe 16 Januari, 2024
Source : news/kamati-ya-bunge-ya-utawala-katiba-na-sheria-yajadili-taarifa-ya-utekelezaji-wa-maazimio-ya-mkutano-wa-bunge
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa kuitikisa na kuliteka jiji la Mwanza Tarehe 30 januari.

0742-676627.
Mwanza Mwanza kwanini sio rukwa!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini anatarajiwa

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Akija Rais mwingine huyu mtakavyomponda sasa...
Sio kwa kusifia huko
 
Mwanza Mwanza kwanini sio rukwa!
Mwanza kwa sababu ndo kunafikika kirahisi kuliko Rukwa na kumbuka mwanza kuna watanzania wengi kuliko Rukwa. Hivyo ukihtaji kuongea / kuonana na watanzania wengi ukiachana na dsm basi nenda mwanza.
 
Sidhani kuna anayetaka kukutukana lakini uandishi wako unakosa weledi na hekima. Nadhani unaamini kuwa unamsifia Rais lakini ukweli ni kwamba unamdhihaki kwa kumwaandika kwa namna usiyomwakilisha. Hiyo Inakuwa ni kumkejeli.

Ni sawa leo hii niandike:

Kesho jioni bilionea wa karne, tajiri wa kwanza Afrika Mashariki, ustaadhi Mwashambwa, ataingia atatua mjini kwa ndege aina ya Concord toleo jipya, na akifika tu huyu shujaa mpiga kungfu wa pekee Duniani, mara baada ya kuhutubia atasikiliza matatizo ya kila mwananchi hapo hapo.

Hapo nitakuwa nimekusifu?
😀😀😀Mimi simdhihaki Mheshimiwa Rais wangu bali naaongea ukweli.nimecheka huo mfano wako
 
BE A GENTLEMAN!! DON'T GET FAKE IN ORDER TO SEARCH CHANCES. Hivi weka Yako namba kilasiku hujatafutwaga tuu?? Uskate tamaa ikosiku wapendasifa watakuona...
Shkuru sisi tunaokuchana tunaweza sababisha uonewe huruma utafutwe kupewa kacheo ndugu mkimbiza teuzi
Mimi sitafuti uteuzi hapa jukwaani ndugu yangu mtanzania
 
Back
Top Bottom