Rais Samia kufungua Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), Juni 19, 2025

Rais Samia kufungua Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), Juni 19, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 utakaofanyika tarehe 19 Juni, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 19 Mei, 2025 wakati alipokagua daraja hilo ambalo limekamilika kujengwa na litakuwa daraja refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
WhatsApp Image 2025-05-19 at 17.18.48_5b64a4a5.jpg

WhatsApp Image 2025-05-19 at 17.18.47_822577f7.jpg

WhatsApp Image 2025-05-19 at 17.18.50_a9a7f749.jpg
"Jitayarisheni kwa wingi kumpokea kiongozi wetu mkuu atakapokuja kulifungua daraja hili Juni 19, 2025 ", amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ameeleza kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Daraja hilo linalopita juu ya maji kwa kutumia fedha za ndani ikiwa ni jambo la kihistoria kwa nchi yetu.

Ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 700 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalounganisha mji wa Kigongo na Busisi katika Ziwa Victoria ambalo ni la tatu kwa ukubwa duniani.

Aidha, Waziri Ulega amewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Sengerema kuwa Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara ya Segerema - Nyehunge (km 54.5) na Kamanga - Sengerema (km 32) kwa kiwango cha lami ili ziweze kuifungua Wilaya hiyo na kuchochea uchumi.
WhatsApp Image 2025-05-19 at 17.18.50_e2241cdb.jpg

WhatsApp Image 2025-05-19 at 17.18.51_b480392f.jpg
Pia soma:
~
Daraja la jp magufuli (kigongo-busisi ) lafikia asilimia 96.3, kukamilika februari 2025
~ NINAISHAURI SERIKALI KWAMBA DARAJA LA KIGONGO -BUSISI LITAKAPOANZA KUTUMIKA KUWEPO NA TOZO
~ Vivuko vya Kigongo-Busisi havifanyi kazi leo. Daraja lifunguliwe kwa dharura kuruhusu magari
 
Hapo walevi tunasaidiwaje? Ninahofia mimi na hiki ki-IST nitakuwa chakula cha sangara jamani.
 
Mimi nisaidiwe kitu...daraja la km 3 na bara bara zake 1.69km....bilion 700.

Lile la Tanzanite nafikiri halifiki km 2...
1.4Trilioni....wataalam wa engineer huu utofauti unaletwa na nn hasa.



Kumbe inawezekana pale jangwani zikajitajika bilioni 300 tu daraja likakamilika.
 
Hii nchi kuna shida katika utendaji,Mwanza kwa sasa watu wanapitia changamoto kubwa sana ya kukaa kwenye foleni muda mrefu kutokana na ujenzi wa madaraja mawili(mabatini na mkuyuni).
Muda mwingi unapotea barabarani badala ya watu kuwa kwenye uzalishaji mali. Uongozi uone umuhimu wa haraka kuboresha barabara hizi zinazotumika kwa kumwaga zege kwenye njia zote ili kuondoa adha kwa wananchi na mali zao(magari yaalibika sana). Ikumbukwe ujenzi huu unatarajiwa kukamilika mwakani,hivyo ikiendelea hivi athali itakuwa kubwa zaidi maana mpaka sasa kuna ajali nyingi zisizo na ulazima zimeshatokea na kughalimu maisha ya raia.
 
Back
Top Bottom