gasper jj

Member
Nov 13, 2012
33
95
Wakati unakuja kuomba kura kwa awamu ya pili ya uongozi wenu 22/09/2020, nakumbuka ahadi nyingi ulizotuahidi, najua kipindi hicho 2020 ulikuwa Makamu wa Rais mtarajiwa, najua ulitoa ahadi kutoka moyoni za nini utatufanyia wana MBEYA tukiwachagua, najua ulijua mtashinda uchaguzi na mulishinda kwa kishindo.

Najua ulikuwa unaongelea ahadi mtakazotekeleza wewe na Rais jambo la faraja sana kwa wana Mbeya wewe sasa ndiye Rais na ndiye mshika mpini tunakuomba sasa utekeleze zile ahadi ulizotuahidi za barabara kutoka Igawa, Songwe mpaka Tunduma kilomita 2018 kuifumua na kuiboresha kwa kiwango cha kimataif

Pia ile barabara ya kuchepuka kwa ajili ya malori kutoka Inyala Uyole Songwe, kuboresha gridi ya Mwakibete tuwe na umeme wa uhakika, madaraja n.k

Karibu mama Mbeya tena maana nimesikia tar 01/12/2021 utatutembelea katika viwanja vilevile ulivyotumia kutupa ahadi 22/09/2020
 

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,436
2,000
Kweli Awamu hii naifagilia bila kificho.

Awamu zilizopita zilikuwa na kinyongo na Mbeya.

Hata wakuu wa mikoa walioletwa walikuwa fiksi tupu, mfano Mwakipesile na Chalamila.

Hao waliibomoa Mbeya kuliko kuijenga.

Ahadi za uchaguzi ni chache sana zilizotekekezwa, na zinazotekekezwa utafikiri serikali haitaki.

Hivyo ujio wa Mama Samia tunausubirikwa hamu.
 

Swet-R

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
4,913
2,000
Kwali Awamu hii naifagilia bila kificho.
Awamu zilizopita zilikuwa na kinyongo na Mbeya...
Basi usichokijua. JPM aliipangilia mbeya kwa nguvu. Ukanda wa huku mbeya ilikuwa kwenye ramani angekuwa JMP. Ilikuwa lazima angeanza na barabara nne kutoka mlima nyoka mpaka mbalizi. Hapo nwanjelwa ilikuwa ramani ya daraja la wavuka kwa miguu. Na ndio maana alilazimisha kumpitisha huyu mbunge mama.

Angekuwepo hayo mambo mpaka sasa yangekuwa kwenye utekelezaji 70% mpaka sasa.

Lakini kwa bahati mbaya baada ya mwendazake ramani ya huyu mama yote imebadirika kuhusu mbeya na kwingine. Na ndio maana unaona hivyo vibarabara vya vumbi vinachongwa kuzugia zugia. Huyu hana mpango na mbeya. Na bahati mbaya ingine,huyu mama na mbunge ”kya njinga nï kya igali”.
 

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
822
1,000
Kanuni za uandishi?
Kwani kuna maombi ya kazi humu.Shughulika na ujumbe unajenga au unabomoa
kila mtu na mwandiko wake wengine tulisoma sayansi hatuwezi zingatia mambo madogo kama hayo uliyoyaona mtu wa arts.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,051
2,000
Basi usichokijua. JPM aliipangilia mbeya kwa nguvu. Ukanda wa huku mbeya ilikuwa kwenye ramani angekuwa JMP. Ilikuwa lazima angeanza na barabara nne kutoka mlima nyoka mpaka mbalizi...
Hizo ni plans tuu na zitaendelea kuwa mipango na itatekelezwa kadiri ya upatikanaji wa pesa..Awamu yoyote ile lazima itatekeleza..

Mbeya ni Mkoa mkubwa na WA tatu kwa kuchangia Pato la Taifa kwa hiyo haiepukiki.Ukiboresha bandari ya Dar huwezi kiepuka Kuboresha Tanzam road na Tazara kwa maslahi ya nchi.

Ukweli ulio wazi ni kwamba awamu ya 5 ilifanya mambo machache Mbeya kulinganisha na Kanda ya Ziwa,Kati na Pwani.
 

Mpap Ndabhit

Member
Jan 15, 2014
96
125
Barabara ya mwakaleli busokelo tunaomba atamke neno nayo itakamilika, imekwama toka aingie madarakani, na huko Kuna uzalishaji wa mazao ya chakula mwaka mzima bila Hata kutegemea mvua
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,934
2,000
Tuseme wazi Maguguli sliunyanyapaa mkoa wa Mbeya kiasi hata chamatawala mkoani kikawa hakina hata sauti.
Dar yenyewe 2015 alinyimwa kura karibu jiji Zima nae kwa kuwakomesha akahamishia shughuli zote Dom huku akizuga anafanya hivyo kisa uzalendo.Kwa visasi alikua ameshindikana yule.Ni vile tu Dar haikwepeki lkn angeigeuza kua kijiji.
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
6,157
2,000
kila mtu na mwandiko wake wengine tulisoma sayansi hatuwezi zingatia mambo madogo kama hayo uliyoyaona mtu wa arts.
Acha kutetea ujinga, sayansi gani inasema uanze na herufi ndogo? Halafu mnalalamika hakuna kazi kumbe hamna mlichosoma!!
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,657
2,000
Barabara ya mwakaleli busokelo tunaomba atamke neno nayo itakamilika, imekwama toka aingie madarakani, na huko Kuna uzalishaji wa mazao ya chakula mwaka mzima bila Hata kutegemea mvua
Na Gesi pia ipo huko kwenu ...kazini sauti naona Mwakyenbe Mwamdosya walishindwa binafsi wao
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
6,157
2,000
Basi usichokijua. JPM aliipangilia mbeya kwa nguvu. Ukanda wa huku mbeya ilikuwa kwenye ramani angekuwa JMP. Ilikuwa lazima angeanza na barabara nne kutoka mlima nyoka mpaka mbalizi. Hapo nwanjelwa ilikuwa ramani ya daraja la wavuka kwa miguu. Na ndio maana alilazimisha kumpitisha huyu mbunge mama...
Hii hoja ya kipuuzi sana. Yaani Magufuli hakuleta miradi ya miundombinu Mbeya kwa sababu ya SUGU kuwa Mbunge wa Mbeya?

Nanyi Mbeya mwaka 2020 Oktoba mukalegea mkakubali awaletee kinyago cha mpapure kutoka Tukuyu ili awe Mbunge wa Mbeya Mjini? Mkitgemea atawaletea maendeleo.

Hicho ni kiwango cha juu cha UPUMBAVU kama mnamchagua Mbunge kwa ahadi ya barabara wakati kodi ni zenu. Wana Mbeya mlipaswa mkomae na Mbunge mnayemtaka hata mkinyimwa kujengwa hata darasa moja au zahanati moja
 

gasper jj

Member
Nov 13, 2012
33
95
Acha kutetea ujinga, sayansi gani inasema uanze na herufi ndogo? Halafu mnalalamika hakuna kazi kumbe hamna mlichosoma!!
nalalamika mimi na nani juu ya hakuna kazi, unaonaje ukajisemea wewe na hali yako maana mm nilishapambana na hali yangu na ya uzao wangu.
 

Swet-R

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
4,913
2,000
Hii hoja ya kipuuzi sana. Yaani Magufuli hakuleta miradi ya miundombinu Mbeya kwa sababu ya SUGU kuwa Mbunge wa Mbeya?...
Yaani umeonyesha ni jinsi gani ulivyo ng'ombe,una akili ya KIPUMBAVU,hujaelewa hata nilichoeleza mimi. Wapi nimekuambia tulimchagua huyo mbunge aliepo sasa mbeya?

Niambie kulikuwa na uchaguzi huo mwaka? Au wagombea wa ccm kupitishwa?. Niambie we ng'ombe ni wapi ambako hamkulegea mlichagua upinzani na akapita? Kwa akili yako bado umelala usingizi kwamba huo kulikuwa na uchaguzi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom