Rais Samia karibu Tanga na wasaidie Wanatanga kero zifuatazo

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,408
1,818
Rais Samia nakusalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninayokila sababu ya kukuambia karibu Tanga lakini uwe makini maana viongozi waliopo bado hawajajua unacho kitaka.

Ninasema hivo kwasababu zifuatazo
1: Hela asilimia 10 kwaajili ya wanawake,vijana na walemavu Tanga ni hadithi ya kufikirika. Kama wamekopesha labda iwe nikwausiri lakini waliowengi wamefuatilia hamna kitu.

2: Kuna mtumishi wa kike ameshtakiwa na DPP kwa kesi ya uhujumu uchumi lakini bado ni afisaelimu kata alichukua mshahara na posho ya madaraka. Tena eti amemkaimisha mtu ofisi maana anaumwa. Wasaidie tamisemi wamechoka

3: Hospitali ya Bombo rushwa ndio nyumbani. Eti mtu akipewa rufaa aende muhimbili anatakiwa atoe laki tano ya ambulance. Maskini watakufa bila matibabu. Wiki iliyopita kuna mgonjwa amefariki kwa kushindwa kulipia ambulance

4: Waulize kuhusu wale makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Tanga jiji na Mkinga zile fedha walizosaini kinyemela wenyewe wawili bila kuwashirikisha watumishi wengine kwenye ofisi zao je walizilipa. TSC makao makuu kwanini hawakuchukua hatua wakati walituma timu yao na walibaini makosa? Tamisemi wanalea wala rushwa na taarifa wanayo.

5: Kuhusu anuani za makaazi mpaka ninapoandika siotu kwamba baadhi ya mitaa haijawekwa vibao vya majina hata nyumba baadhi hazina namba. Hao viongozi wanakulatu viyoyozi na nimadikteta hawataki kuhojiwa.Nape ametembea na lihelkopta lake lakini hawajali wala hawana aibu

6:Barabara za mitaa baadhi hazipitiki.

7: Halmashauri Tanga jiji inanuka ngono. Waliokataa kuvuliwa nguo wamenyanyasika sana.

8: Waandishi wa habari Tanga hawapo. Walishanunuliwa jumla na aliyekua mkurugenzi bwana Mayeji na ndugu yake Shigela. Hao madikteta walikua hawataki wanahabari kabisa. Hata hiyo TBC yako mama Tanga hatuwaoni. Tanga jiji inashindwa hata na Handeni huko kuna waandishi wa habari wa channel ten akina Mbezi. Hii ni aibu

9: Migogoro ya ardhi imetamalaki. Watu wa ardhi ndio madalali bila woga. Wamekua wanyang'anyi wa kupora haki za watu. Hili linatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

10: Katibu tawala amechoka fanya umsaidie. Hebu mbadilishie mazingira yule mama mkoa huu umemshinda.

Amepelekewa kero kibao hataki kuzifanyia kazi. Ameshindwa hata kuchukua hatua kwa watumishi wabadhirifu tena ndio wanapandishwa vyeo kwakuatu ni makada. Kwani kuna uhusiano wa wizi na ukada?

Mh. Rais mstue RAS amelala hamna kitu
 
TANGA WAVIVU
Wavivu wa kutupa! hawafai katu, hasa hawa Wadigo. Wao hawafanyikazi katu, wanategea wapi kumepikwa wali wadoee, hawana aibu KUOMBA... hawana maendeleo.

Anataka ukiwa na gari say, iharibike mfanane na siyo kuwa naye akazane apate gari kama wewe! watu wa ajabu kabisa sijawahi ona! Ummy Mwalimu anzisha programme maalum ya kuwaamsha kielimu.

Wao elimu wanayoijua ni madrasa eti CHUO! hapo mtoto atachapwa afe kama hajaenda chuo. lakini elimu ya kawaida, is rubbish to them!

Mnisamehe maana ukweli utawaumiza.
 
Tanga Kunani Pale, Mbona Kila Kitu Pale Kimekufa
Railway Kimya, Wenyewe Tushajizoelea Mijihoni
Viongozi Wanamkwamisha Mama, Wanalamba Asali Tu
 
Utani wa ngumi huu..!
siyo utani, kule dini imekuwa so internalized kiasi mtu hawezi ku make sense out of those instructions which seem to be outdated hata kama ni dini. Maisha yao yanaongozwa na dini by 100%.
Bado wako "primitive" sana, kuna ngoma za mashetani, wanacheza mchana kweupe bila aibu. Wanaamini ushirikina sana....kupitiliza
 
Mh. Rais nakusalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ninayokila sababu ya kukuambia karibu Tanga lakini uwe makini maana viongozi waliopo bado hawajajua unacho kitaka...
Hicho ndiyo kipimo halisi cha uwajibikaji wa Rais Samia ktk ziara zake. Asante sana. Tulitegemea hata Mbeya alipaswa kuwa na watu wa kumuuma masikio ili afanyie kazi kero kweli za wananchi.

Mungu ambariki Rais Samia, kwa sababu dhamira yake kwa watanzania ni njema kabisa.
 
Hicho ndiyo kipimo halisi cha uwajibikaji wa Rais Samia ktk ziara zake. Asante sana. Tulitegemea hata Mbeya alipaswa kuwa na watu wa kumuuma masikio ili afanyie kazi kero kweli za wananchi. Mungu ambariki Rais Samia, kwa sababu dhamira yake kwa watanzania ni njema kabisa.
Mrembo Mudawote nakusalimu, nakupenda... hili nalo nenda ukalitizame.
 
Hao Takukuru naona walishanunuliwa na hao viongozi wanaomlinda huyo mwanamke. Vinginevyo wangeshakamata na kusukuma ndani mkurugenzi,afisaelimu na RAS. Hiyo ni dharau kwa Mh. Rais, DPP na mahakama
 
Back
Top Bottom