Ni ushauri tu!
Kwa kasi sana tunaona wanavyojitahidi, kutengengeneza mazingira ya kukusogelea zaidi.
Walianza na Mechi ya kumchangia yule mtoto mgonjwa.
Na kwa mara ya kwanza tangu uingie madarakani kama Raisi.
Ulipiga simu live uwanjani,ambapo pamoja na kutoa Pongezi,lakini pia ulichangia kiasi cha Milioni 15.
Jambo la thawabu kusaidia wasio na uwezo na wenye mahitaji.
*siku iliyofuatia pale baada ya mechi,kiwanda chao kikaungua moto wenye chanzo tata mpaka sasa.
*Na siku moja kabla ya hiyo mechi ya hisani,kulikuwa na tukio la mmoja wa wakurugenzi GSM,
Kuhusika na ufyatuaji ovyo risasi,mbele ya maafisa Polisi,bila kuchukuliwa hatua.
Ilikuwa katika tukio la ugomvi wa kugombea eneo na jengo huko Mikocheni kati yao na Ex-RC Paul Makonda.
Movie iliendelea tena Jana pale uwanja wa Taifa.
GSM waliandaa na kuitumia mechi ya ligi kuu ya NBC-PREMIERE.
BainaYanga na KMC.
Kama tukio maalumu la kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani.
Tukio lenye heri pia.
Yanga walicheza mechi ile wakivalia jezi maalumu zenye picha ya Samia
(Rais wa JMT [emoji1241]).
Hapo sijui sheria za FIFA na TFF zinasemaje kuhusu kuchanganya Michezo na Siasa.
Tuwaachie wenyewe kwa hilo.
Nimeyatumia hayo machache kama mfano.
Maoni yangu mimi!
Inavyoelekea hawa wanajaribu kutaka kuwa karibu na Ikulu kama walivyowahi kufanya huko nyuma,katika awamu ya nne.
Kipindi hicho wakijulikana kama Home Shopping Centre.
Bado tuna kumbukumbu na matukio yao.
Ikiwemo yale ya kupiga watu risasi hadharani wakiwemo wafanyakazi wao na hata wapita njia tu.
Haya mambo yalipelekea mmoja wa kaka wa huyo Gharib kuikimbia nchi baada ya ujio wa serikali ya awamu ya Tano ya JPM (R.I.P).
Na mpaka sasa yuko ughaibuni.
Waathirika wa matukio yao wapo mpaka sasa mitaani.
Kuanzia wa kashfa za makontena mpaka hao wa risasi miguuni.
Sasa wamerudi upya na nembo mpya ya GSM.
Mambo ya sasa na ya wakati ule wa HSC ni kama yanataka kujirudia kwa mtindo mpya.
Bado kuna mgogoro wa udhamini wa ligi kuu ya NBC-PREMIERE kati ya GSM na TFF Uko mezani.
Ambapo GSM wamejitoa na kuuvunja mkataba kinyemela huku wakiwa wamekwishazitumikisha timu za ligi kuu kwa miezi mitatu bila ya malipo,kama mkataba unavyotamka.
Hatujui kama washauri wa Ikulu na vyombo vya usalama haviwajibiki ipasavyo ili kuyaona haya na kun'gamua na kutoa ushauri pale mh Rais anapoelekea kupotoshwa namna hii.
Lakini ieleweke kwamba, kwa kutochukua hatua mapema na kujitenga na Uhuni.
Basi huko tuendako....kama ikitokea GSM wakachafuka kwa kashfa yoyote ile iwayo.
Hii pia Itakuwa inamhusu au kumchafua pia yeyote aliyeko madarakani kwa sasa,ambaye ataonekana kuwa nao karibu katika kipindi chake cha uongozi.
Kutokana na matukio kadhaa yatakayo waweka kuonekana kuwa karibu zaidi kwa jamii.
Naye atachafuka nao.......
Na itakuwa na gharama kubwa sana kujisafisha kwa wakati huo.........
Nimewakilisha kama....
commonmwananchi
10101.