Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Mtu yeyote mwenye kujua sheria anapoona tu kichwa cha thread hii, atasema sio sahihi, Rais Samia hapaswi kuingilia kati suala la mashitaka ya Mbowe ya Ugaidi kwa kuwa hapaswi kuingilia kati mhimili wa Mahakama. Ni kweli.

Lakini pia, Watanzania wengi sana wanaamini kwa dhati kwamba kesi ya uagaidi dhidi ya Mbowe ina mkono au baraka za Raisi Samia. Labda kweli.

Na wanasheria makini, watakuambia kwamba kesi ya ugaidi dhidi ya Mboewe, pamoja na kelele nyingi sana za Polisi, haina mshiko wa kisheria na kama kweli itasikilizwa kwa haki basi ni rahisi kwesi hiyo kutupwa au Mbowe na washitakiwa wenzake wote kushinda kesi.

Sasa unajiuliza, hivi ilikuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali asimshauri Rais Samia kwamba kesi kama hii dhidi ya Mbowe haitakuwa na mshindi? Kwanza inaiweka Tanzania katika darubini ya mataifa makubwa ya nje.

Pili inafanya idadi kubwa ya watu kuamini kwamba Mbowe alikamatwa kwa ajili ya makongamano ya Katiba na ugaidi ni kisingizio tu.

Tatu inaonyesha wazi kwa watu wa ndani na nje kwamba CCM wanaogopa Katiba mpya kwa kuwa wanahofia uchaguzi ukifanywa katika mazingira ya kidemokrasia CCM hawatashinda.

Nne Mbowe akifungwa kwa mashitaka kama haya ambayo yapoyapo tu itampa umaarufu zaidi ndani na nje ya nchi, atakuwa Mandela wa Tanzania.

Tano Mbowe akiachiwa Rais Samia na CCM wataonekana wanabambikia wapinzani kesi.

Sasa kama Mwanasheria Mkuu alishindwa kuona haya na kumshauri Rais Samia dhidi ya kesi ya Mbowe, nina mashaka sana na uwezo wake wa kumshauri Rais, au lengo lake la ushauri aliotoa kwa Rais Samia.

Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.

Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku, lakini pia akiliacha liendelee mahakamani, matokeo yake yoyote, ya kesi kutupwa nje, au Mbowe na wenzake kufungwa au kuachiwa huru, hayatakuwa mazuri kwake Rais Samia na chama chake CCM
Kwanini aingilie kati, wacha sheria zichukue mkondo wake, akiingilia kati si ndio mnasema anaingilia uhuru wa mahakama? kila siku mnadai serikali isiingilie mahakama au ndio mnajitoa ufahamu, haki haipatikani kwa raisi kuingilia kati bali haki hupatikana mahakamni.
 
Kama kujipanga ndiyo ticket ya uhakika kwa asilimia 100 ya kushinda kesi mahakamani wote waliojipanga wangekuwa wanashinda vyesi vyao. Hivi hujawahi kujiuliza pamoja na wingi wa mawakili wote wa Mbowe kwa nini wanashinikiza aachiwa kabla ya kesi kusikilizwa?. Kuna kitu haukijui. Wao wanaelewa potential risk iliyo mbele ya Mbowe. Usifanye utani na sheria
Umesikiliza mahojiano ya BBC leo!!..ulimsikia na mkuu wa police vizuri!!..narudia tena Mbowe akifungwa,akiachiwa huru whatever the case is Bado atakua mshindi!!..
 
Nawaza tu..
Muelekeo wa kesi ukionesha tu upande wa Jamhuri kushindwa ama kesi ikaonekana ni ya kubumba kulingana na ushahidi wenye mashaka basi walioko pale juu hawataweza kukubali kuaibika kitakachofuata kuna watu watabebeshwa zigo la lawama na kutolewa kafara kwamba hawakutenda majukumu yao kwa weledi..
 
Hili jambo uwezekano wa kuisha kwa namna ya kumuaibisha Raisi Samia ni mkubwa sana. Na mbaya zaidi ameanza kuliongelea kishabiki. Namuonea huruma, hajui siasa huyu.
 
Kwanini aingilie kati, wacha sheria zichukue mkondo wake, akiingilia kati si ndio mnasema anaingilia uhuru wa mahakama? kila siku mnadai serikali isiingilie mahakama au ndio mnajitoa ufahamu, haki haipatikani kwa raisi kuingilia kati bali haki hupatikana mahakamni.
Aingilie kati kwa sababu atakuja kuaibika na kupoteza heshima yake
 
Hili jambo uwezekano wa kuisha kwa namna ya kumuaibisha Raisi Samia ni mkubwa sana. Na mbaya zaidi ameanza kuliongelea kishabiki. Namuonea huruma, hajui siasa huyu.
Yaani leo Chadema ndiyo mnamhurumia Rais Samia asiaibike.? Subirini aibike mfurahi. Kelele nyingi za nini. Huku mnasema kesi inamharibia hapo hapo mnataka afute kesi? Acheni kesi imharibie ili mchukue advantage hiyo kisiasa.
 
Umesikiliza mahojiano ya BBC leo!!..ulimsikia na mkuu wa police vizuri!!..narudia tena Mbowe akifungwa,akiachiwa huru whatever the case is Bado atakua mshindi!!..
Kama ni hivyo kweli na Chadema mnaamini hivyo, kwa nini mna lia lia aachiwe kwa huruma ya Rais. Acheni gaidi afungwe miaka 20 jela ili awe mshindi. Ndiyo mtajua kama kufungwa ni ushindi au la. Na wewe andaman a ufungwe ili ukajiunge naye uwe mshindi
 
Mpaka hapa mama kashachafuka, aingilie asiingilie, amfunge amuache huru kosa la kiufundi limeshafanyika na hakuna njia yoyote ya kujisafisha. Walikuwa wakimsifu mama anaupiga mwingi mpaka nje ya uwanja kumbe ndio walimaanisha haya?
 
Kama ni hivyo kweli na Chadema mnaamini hivyo, kwa nini mna lia lia aachiwe kwa huruma ya Rais. Acheni gaidi afungwe miaka 20 jela ili awe mshindi. Ndiyo mtajua kama kufungwa ni ushindi au la. Na wewe andaman a ufungwe ili ukajiunge naye uwe mshindi

..ccm kutumia polisi na mahakama kupambana na wapinzani siyo jambo jema kwa nchi yetu.

..tunaweza tukafika mahali wananchi wakawa hawana imani na polisi na mahakama zetu.

..vyama vya siasa vingeachwa vipambane kwenye majukwaa kwa hoja bila polisi kuingilia kwa niaba ya chama tawala / ccm.
 
Kama ni hivyo kweli na Chadema mnaamini hivyo, kwa nini mna lia lia aachiwe kwa huruma ya Rais. Acheni gaidi afungwe miaka 20 jela ili awe mshindi. Ndiyo mtajua kama kufungwa ni ushindi au la. Na wewe andaman a ufungwe ili ukajiunge naye uwe mshindi
Hata mjadala huu hujui unaongelea nini kwasababu umeshaonyesha interest ya chama wacha nikuache great thinking siyo siasa tu Rafiki yangu siyo kila mwenye mawazo mbadala ni mwanasiasa wa upinzani
 
Umemaliza kila kitu
Hakuna lolote lenye mantiki kutoka kwenye hiyo post ya TOHATO . Amemaliza kila kitu???? You guys are joking...

Mabadiliko ya namna Mama anavyoendesha nchi hayatokani na kusoma risala yoyote ile na CCM.

Kuna msemo wa kiarabu unasema "Punda haendi isipokuwa kwa magongo"

Tafakari
 
Kama kwa kuchukua msimamo huu ndiyo umaarufu wake utashuka na kufanya upinzani kuchukua urais 2025, nadhani hii ni habari njema kwa upinzani. Kwa nini mnalilia sasa. Subirini mpate hiyo advantage. Yaani wewe ni mpinzania lakini unataka Rais asifanye vitu vya kumwangusha 2025, hiyo ni akili kweli?
Wanajitekenya na kucheka wenyewe hawa watu hahahahahahaahahahaa
 
Hujasoma vizuri, na labda umesoma kichwa cha thread tu. Singeweza kukirefusha zaidi ya hapo. Ukiangalia thread yote nimesema Mbowe ashinde au ashindwe, au kesi itupwe, yote ni mbaya kwa Samia

Nisawa na kukutwa shambani kwa Mmakonde na kuambiwa ukikimbia nchale, ukichimama nchale, ukikaa nchale!
Si ndio vizuri iwe mbaya kwa Mheshimiwa Rais Samia ili 2025 wapinzani washinde uchaguzi hahaahahahahahaha
 
Una mshauri Rais aingilie mhimili wa Mahakama ili mseme Mahakama zetu sio huru? Mbowe akiachiwa kwa order ya Rais hawezi kuwa huru sababu Mahakama ndio inayotakiwa kuthibitishia umma kwamba hakutenda kosa.

Mimi naona Selikari inataka kumlipa Mbowe fidia kwa uharibifu wa mali zake lakini wakaona njia nyepesi ni hii wampe kesi ashinde afungue kesi ya kudai fidia wamlipe mabilion.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Kweli kabisa ndugu
 
Mtu ambae hataki kujiingiza kwenye siasa hawezi kutoa ushauri wa kipuuzi hivi. Mbona haukumshauri raisi aingilie kati kesi ya Sabaya au yeye sio mtanzania? Sirro ashasema kwamba police wana uhakika wa kutosha na kile walichomkamatia Mbowe, sasa ww ni nani kumtaka raisi aingilie kuzuia haki isitendeke? Fikiria kwamba kabla mahakama haijathibitisha kupitia ushahidi kuwa fulan kama kosa, hakuna mtu ambae yuko tayar kukubali kwamba alifanya hiki au kile. Sasa raisi akiingilia mahakama ili Mbowe aachiwe, kesho Sabaya na yeye atataka hivyo hivyo maana na yeye ana watu wake wanaoona kuwa ameonewa. So Sabaya akiachiwa na wengine pia watafuatia. Matokeo yake mahakama zetu zitakuwa hazina kazi za kufanya zaidi ya kuwashtaki watu na kuwaachia kiholela olela.
Hawa vijana akili zao ni fupi sana.

Hapa umejaribu kumuelewesha unadhani hata amekuelewa???
 
Serikali ya Marekani imetoa ushauri serikali ya ccm wakae na chadema meza ya mazungumzo, je serikali ya cccm watakubali? wanaweza kuwakatalia Marekani? kwa hili la Mbowe serikali imejiweka pagumu sana?
Jidanganyeni tu hahahahahaha.

Eti serikali ya Marekani imetoa ushauri.

Kesho ukiambiwa serikali ya China imetoa ushauri watu wanaotaka kuvuruga amani si wa kuchekea utasema nini???
 
Kama umemsikiliza Samia akihojiwa na Salim Kikeke, kuna kitu kimoja utakuwa umeelewa…. kitu gani hicho?
 
Umeongea point sana, na ndio maana nikasema mtu anaejua sheria ataona kwamba si vema kuingilia kesi iliyoko Mahakamani.

Lakini kuna njia nyingi za busara na hekima kwa raisi kuingilia kesi iliyoko mahakamani, na hilo ndilo ninalomwambia Raisi Samia afanye.

Kwa mfano, suala la kusema watu wenye kesi za uhujumu uchumi mahakamani wanaweza kukubaliana na DPP, ilikuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama, lakini lilifanyika. Sembuse hili?

Kuna ugumu gani kwa Raisi Samia kusema tumefanya mkutano na watu wa upinzani na kwa maslahi ya utaifa wetu tumekubaliana kuiomba ofisi ya DPP kufuta kesi zote za kisiasa nchini ili tuanze ukurasa mpya wa uhusiano kati ya CCM na vyama vya upinzani
Ukurasa mpya mnautaka leo???

Kwani sio yeye aliyewaambia hivyo??? Akasema apewe muda kidogo halafu atakaa nanyi muongee, kilichotokea ni nini?? Matusi ya nguoni sio??

Kesi na iendelee, alishasema mapema ukimzingua anakuzingua. Hatutaki kelele na lawama hapa
 
Back
Top Bottom