Rais Samia, ikitupendeza futa Jeshi la Polisi, Tuletee Huduma ya Polisi

Kwa huduma ya loss report bonyeza moja, kwa huduma ya kutapeliwa bonyeza mbili, kama umebakwa bonyeza tatu, kwa taarifa ya kupotelewa na mali bonyeza nne, kuongea na muhudumu wetu bonyeza tano......

"kama vodacom yaani huduma kwa wateja."

Unajua polisi hawanaga maana mpaka siku wakikuokoa kwenye mikono ya watesi wako na familia yako.

Tuboreshe mfumo wa askari wetu na maslahi. Wanafanya kazi nzuri pamoja na mapungufu mengi yaliyopo
 
Polisi wana kazi kubwa sana ndani ya nchi, kuhakjkisha amani ya ndani ya nchi inadumishwa, hata uhuru ulio nao ukashika simu yako na kuandika huu uzi na hakuna aliyekuja kukupora ni kazi yao, na jeshi la wananchi lina majukumu yake makubwa,kuzuia maadui wavamizi,waasi n.k Jwtz kuchukua kazi ya polisi ni kuwabebesha mizigo mikubwa itakayowafanya washindwe kutimiza majukumu yao. Hebu elezea tofauti ya jeshi la polisi na huduma ya polisi.
 
Hilo suala wameona halina tija maana hata wakiitwa service,bado matumizi ya force yatakuwepo tu. Rejea hapo nchini Kenya walifanya mabadiliko ila bado wameona umuhimu mkubwa wa polisi kuwa militarized.
 
Au alibadilishe tu jina na kuliita Jeshi la Kupokea Mlungula Tanzania JKMT!!
 
Mfumo wa polisi ni kunyanyasa raia na kuchukua mali zao hakuna ulinzi hapo yaani wakati wowote polisi wanawatamani Raia na kuwatengenezea mazingira ya kesi ili wachukue fedha ya dhuluma...
 
Mkuu wa Kibiti

Aya yangu ya mwisho ni PhD thesis kabisa. Isome tena.
Sikupingi mkuu,nilicho maanisha ni watu kuelewa ili kupata watu wengi zaidi watakao upigia upatu mfumo unao upendekeza.Bila uelewa historia ni mwalimu mzuri.Wanasiasa wetu ni mahiri wa kudandia hoja bila kuelewa sawasawa ndio maana nikashauri uuchambue mfumo kwa kina japo kidogo
 
Mheshimiwa Rais

Nianze kwa kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo ni lile lile la kazi iendee.

Tumekuwa na mijadala nchini mwetu kwa nyakati tofauti kuhusu namna Jeshi letu la Polisi linavyofanya kazi. Mara nyingi Jeshi limekuwa likishutumiwa kwa masuala kadhaa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya Rushwa, kubambikia watu kesi, kushirikiana na wahalifu na masuala mengine kama hayo. Pengine sio rahisi sana kuthibitisha tuhuma hizi.

Hivyo basi, napenda nitumie fursa hii kupendekeza kwako ulifumue na kuliunda upya Jeshi la Polisi. Kwamba Polisi iwe ni huduma kama huduma za uhamiaji. Kwa mfano, badala ya kuwa na Jeshi la Polisi tuwe na Huduma ya Polisi. Vivyo hivyo tuwe na Huduma ya Magereza etc.

Mambo ya Kijeshi yabaki kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Imani yangu ni kwamba tukiwa na Huduma ya Polisi chombo hiki kitajikita kuelimisha Raia huku kikitekeleza majukumu ya ulinzi wa Raia na Mali zao. Kwenye jumuiya yetu ya SADC wenzetu wa Botswana hawana Jeshi la Polisi badala yake Wana huduma ya Polisi. Natumai tunaweza kujifunza kwao.

Hivyo basi ikikupendeza Mheshimiwa Rais waweza kuelekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi na utafiti zaidi kuhusu hili kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu na maendeleo yetu. Kisha utujalie tupate chombo hiki cha Huduma ya Polisi.

Nawasilisha.
Nimecheka kweli.Siku kaza tu Mmesema watu waachiwe wamebambikiwa kesi wameachiwa ile wamerudi kitaa ujambazi umerudi.Sasa jiulize walibambikiwa au wanafanya siasa kwenye Ulinzi.
"Kazi iendelee"
Mambo ya Ulinzi tuwaachie wenyewe walinzi mambo ya kuwaingilia ingilia tutaanza kuishi tena kwa hofu wakati tulishasahau.
 
Police Service ni bora zaidi katika nchi yetu, mbona botswana wameweza sisi tunakwama wapi?
 
Police Service ni bora zaidi katika nchi yetu, mbona botswana wameweza sisi tunakwama wapi?
Tumepishana sana Mila na desturi .Bostwana ina Wandebele na Washona tu ila Bongo tunayo Makabila 120 kule umasaini na Ukurya ukiiba ng'ombe unaleta Nyumbani ukoo unakuwa tajiri wewe unaonekana tajiri ila kule Kwa Wadigo na Wapemba Hapo utatengwa hata na Mkeo.sasa usijifananishe.Kumbuka siasa zetu pale congo, Burundi,Msumbiji, bado wanaendelea na vita za wenyewe wakati huko Botswana kila kona kupo shwari.
 
Wazo limetoka,kama ungeandika pia mfumo huo unafanyaje kazi,tofauti ya kuwa jeshi na huduma ni ipi japo umedokeza kidogo lakini ungeeleza zaidi hizo faida kulinganisha na changamoto zilizopo.Ukifanya hivyo hoja yako itapata mashiko hata na wale ambao wanatarajia kukupinga pasi na kujua unacho jengea hoja watakao kupinga ni wale majuao unacho simamia.Ngoja wakuu waje nami ntarudi....
Ni kweli mkuu, kama kubadili tu jina na staff wakabakia ni wale wale, hakuna kitu kitakachokuwa kimefanyika.

Halafu mbona majirani zetu Kenya nao washabadili neno force kwenye polisi yao na kuita service, je kunamabadiliko ya kimantiki katika utendaji wa hiyo police servise badala ya police force?
 
Tumepishana sana Mila na desturi .Bostwana ina Wandebele na Washona tu ila Bongo tunayo Makabila 120 kule umasaini na Ukurya ukiiba ng'ombe unaleta Nyumbani ukoo unakuwa tajiri wewe unaonekana tajiri ila kule Kwa Wadigo na Wapemba Hapo utatengwa hata na Mkeo.sasa usijifananishe.Kumbuka siasa zetu pale congo, Burundi,Msumbiji, bado wanaendelea na vita za wenyewe wakati huko Botswana kila kona kupo shwari.
Mkuu

Botswanana hawana Ndebele na Shona.

Kweli historia na mazingira ya nchi yetu hayafanani na wengine. Botswana crime rate ipo Chini Sana ukilinganisha na Africa Kusini. Wote Wana police service.

Fikra za kuwa na polisi ya Kijeshi ni fikra za kikolonii. Kukandamiza Raia wako mwenyewe. Jeshi libaki JWTZ.
 
Back
Top Bottom