50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 3,875
- 3,730
Mheshimiwa Rais
Nianze kwa kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo ni lile lile la kazi iendee.
Tumekuwa na mijadala nchini mwetu kwa nyakati tofauti kuhusu namna Jeshi letu la Polisi linavyofanya kazi. Mara nyingi Jeshi limekuwa likishutumiwa kwa masuala kadhaa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya Rushwa, kubambikia watu kesi, kushirikiana na wahalifu na masuala mengine kama hayo. Pengine sio rahisi sana kuthibitisha tuhuma hizi.
Hivyo basi, napenda nitumie fursa hii kupendekeza kwako ulifumue na kuliunda upya Jeshi la Polisi. Kwamba Polisi iwe ni huduma kama huduma za uhamiaji. Kwa mfano, badala ya kuwa na Jeshi la Polisi tuwe na Huduma ya Polisi. Vivyo hivyo tuwe na Huduma ya Magereza etc.
Mambo ya Kijeshi yabaki kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Imani yangu ni kwamba tukiwa na Huduma ya Polisi chombo hiki kitajikita kuelimisha Raia huku kikitekeleza majukumu ya ulinzi wa Raia na Mali zao. Kwenye jumuiya yetu ya SADC wenzetu wa Botswana hawana Jeshi la Polisi badala yake Wana huduma ya Polisi. Natumai tunaweza kujifunza kwao.
Hivyo basi ikikupendeza Mheshimiwa Rais waweza kuelekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi na utafiti zaidi kuhusu hili kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu na maendeleo yetu. Kisha utujalie tupate chombo hiki cha Huduma ya Polisi.
Nawasilisha.